Wednesday, August 24, 2016

Wembe wampeleka kortini, sahani zamtupa jela miezi minane

NA JEMA MAKAMBA
KIJANA aliyefahamika kwa jina la Chande Rashid (20) amepandishwa kortini katika Mahakama ya Mwanzo Ilala jijini Dar es Salaam kwa kosa la wizi na kudhuru mwili.

Akisomewa mashtaka na karani Lucy Lutabazi mbele ya Hakimu Asha Mpunga ilidaiwa mshtakiwa alitenda kosa Agosti 8 mwaka huu saa 4 usiku kinyume na Kifungu cha Sheria Na. 241(16) cha kanuni ya adhabu maeneo ya Uhonda na Raha.

Ilidaiwa mshtakiwa ambaye kazi yake ni kubeba mizigo walipishana kauli na Mohamed Mfaume ndipo alipochukua wembe na kumchana pua.

Hakimu ameahirisha kesi hadi Septemba 7 mwaka huu itakapotajwa tena.

Katika shauri lingine Sharif Fadhil (19) mkazi wa Kigogo jijini Dar es Salaam ametupwa jela miezi minane kwa wizi sahani na kuharibu mali za Noel Aloyce.

Ilidaiwa Juni 16 mwaka huu katika mtaa wa Aggrey mshtakiwa alitenda kosa kinyume na Kifungu cha Sheria Na. 265(16) na 336(16) akitumia kisu.

Hakimu alimtaka mshtakiwa atupwe jela na akishatoka atapaswa kulipa  thamani ya mali ya mshtaki.

0 Comments:

Post a Comment