Monday, August 29, 2016

Fundi seremala kizimbani kwa wizi

NA DIANA JOACHIM, TUDARCO

FUNDI seremala aliyefahamika kwa jina la Mrisho Iddi (29) mkazi wa Mchikichini amefikishwa mahakama ya mwanzo ya Ilala jijini Dar es Salaam kwa kosa la kuiba pochi iliyokuwa na dola 3000.

Akisomewa mashtaka na karani Blanka Shayo mbele ya Hakimu Matrona Luanda ilidaiwa mshtakiwa alitenda kosa hilo kinyume na sheria za nchi, Agosti 26 mwaka huu katika Mtaa wa Kongo, Kariakoo.

Aidha ilidaiwa kuwa mshtakiwa aliiba pochi iliyokuwa na risiti za bidhaa, vitambulisho na dola 3000 (sawa na Sh. Milioni 6 mali ya Alli Bonomali .

Hakimu alisema dhamana ipo wazi kwa mshtakiwa kwa ahadi ya Sh. Milioni 10 na wadhamini watatu wa kuaminika na aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 6 mwaka huu.




Katika shauri lingine Omary Twaha (23) na Jeremia Molel (32) wote wakazi wa jijini hapa waliiba Sh. Milioni 2 zilizokuwa dukani mali ya Boniface Gervas.

Washtakiwa walikana mashtaka hayo na kesi kuahirisha hadi Septemba 7 mwaka huku washtakiwa wakitakiwa kutoa Sh. Milioni 3 na wadhamini wawili.

0 Comments:

Post a Comment