Monday, August 22, 2016

Kortini kwa kuchomoa Sh.200,000/-

NA MAGRETH MTAFI
MKAZI wa Magomeni Thadei Agostino(35) amefikishwa mahakama ya mwanzo Ilala kwa kukabiliwa na mashtaka ya kumchomolea Seif Mohamed kiasi cha shilingi 200,000.

Akisomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu mkazi ya mahakama  hiyo, Asha Mpunga ,Karani wa kesi hiyo Lucy Lutabazi alidai mshtakiwa alifanya kosa hilo Agosti 20 saa tatu usiku maeneo , Kariakoo Dar es Salaam.

Ilidaiwa mshtakiwa alifanya kosa hilo kwa makusudi huku akijua kuwa ni kosa kisheria, baada ya kusomewa mashtaka hayo, mshtakiwa alikana kosa hilo.

Hakimu mpunga alisema dhamana iko wazi kwa kufuata masharti, ambapo wadhamini watasaini shilingi 300,000, mshtakiwa alishindwa kukidhi masharti ya dhamana na alirudishwa rumande hadi Septemba Mosi mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.

Katika hatua nyingine washtakiwa Bernad stanley(18) na Chacha Chacha(34) walifikishwa katika mahakama hiyo kwa kosa la wizi wa fedha Sh. 60,000 mali ya Wiliam Mlenda.

Ilidaiwa washtakiwa hao walifanya kosa hilo Agosti 21 maeneo ya kariakoo Dar es Salaam.


Washtakiwa walikana kosa kosa hilo mshtakiwa namba moja Bernard Stanley alirudishwa rumande kwa kushindwa kukidhi masharti ya dhamana na Chacha ametoka kwa dhamana ambapo watarudi mahakamani hapo Semptemba mosi kesi hiyo itakapotajwa tena.         

0 Comments:

Post a Comment