Ilala, Dar es Salaam
MFANYABIASHARA aliyefahamika kwa jina la Kalunde Waijuba mwenye miaka
42 mkazi wa Kisota, Kigamboni jijini Dar es Salaam amepandishwa kortini katika
mahakama ya Hakimu Mkazi Ilala akituhumiwa kufanya shambulio la kudhuru mwili.
Akisoma mashtaka Karani Lucy Lutabazi alisema mtuhumiwa alitenda kosa
hilo Agosti 10 mwaka huu saa 9:40 alasiri katika mtaa wa Mkunguni jijini hapa.
Ilidaiwa na mbele ya Hakimu Mkazi Asha Mpunga kuwa mtuhumiwa alitenda
kosa hilo wakati mlalamikaji Bi. Upendo alipokwenda kudai Sh. 250,000/-.
“Mtuhumiwa alimvamia mlalamikaji na kumpiga ngumi kumi za kifua,
alimpiga mgongoni, mdomo mateke ya tumboni kisha kumkanyaga, pia alimng’ata
meno bega na kumsukumiza chini huku akijua
kufanya hivyo ni kukiuka kifungu cha
sheria Na. 241(16) cha kanuni ya adhabu,” alidai Mwendesha Mashtaka.
Aidha Hakimu Mkazi alimtaka mlalamikaji kupata dhamana ya Sh. 800,000/-
kutoka kwa wadhamini wawili kisha aliahirisha kesi hadi Agosti 31 mwaka huu
itakapotajwa tena.
Katika shauri lingine kijana aliyefahamika kwa jina la Said Omary mwenye miaka
19 mkazi wa Kibondeni mjini Zanzibar amepandishwa mahakamani kwa wizi wa waya
wenye thamani ya Sh. 10,000.
Akisoma Mwendesha Mashtaka alisema Agosti 13 mwaka huu saa 3:20 usiku maeneo Upanga jijini hapa kwenye Ofisi za Stamico aliiba
waya huo kinyume na kifungu cha sheria Na. 265 (16) cha kanuni ya adhabu.
Mtuhumiwa amekubali kosa amerudishwa rumande baada ya kukosa wadhamini
mpaka Agosti 31 mwaka huu itakapotajwa tena.
0 Comments:
Post a Comment