Friday, August 26, 2016

Kortini kwa wizi kontena la Mil. 160

NA JABIR JOHNSON
WATU watatu wamepandishwa kortini katika mahakama ya wilaya ya Ilala jijini hapa wakikabiliwa na makosa ya kula njama na kujipatia mali kwa udanganyifu ikiwamo wizi wa kontena lenye thamani ya Sh. Milioni 160
Wakisomewa mashtaka na Mwendesha Mashtaka Sylivia Mitanto mbele ya Hakimu Mkazi Wilberforce Luhwago mshtakiwa Abdallah Ndule mkazi wa Mbezi Louis (47) na Hassan Selemani mkazi wa Buguruni (49) ilidaiwa washtakiwa wakiwa na Hamis Mtitu (ambaye hakutokea mahakamani hapo) walitenda kosa hilo Mei 16, 2015 maeneo Ticts Bandarini.
Aidha Mitanto alidai walitenda kosa la kula njama kinyume na Kifungu cha Sheria Na. 384 cha Kanuni ya Adhabu kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002 na walitenda kosa la wizi wa kontena Na. MSK 435766 lenye thamani ya Sh. 160,125,433 kinyume na Kifungu cha Sheria Na. 258 na 265(16) mali ya Nyota Tanzania Ltd.

Baada ya kusomewa mashtaka yao Hakimu wa mahakama hiyo aliwapa masharti ili waweze kuachiliwa kwa dhamana kuweka Sh. Milioni 20  au Hati za Makazi zenye thamani ya Sh. Milioni 20, washtakiwa walishindwa na kurudishwa rumande hadi Agosti 30 mwaka huu itakapotajwa tena.

0 Comments:

Post a Comment