Friday, August 26, 2016

Kizimbani kwa kuvuruga ibada

ILALA, DAR ES SALAAM

WATU 10 wamepandishwa kizimbani kwa kuvuruga ibada ya waumini wa Kanisa la Moravian Parishi ya Kitunda jijini hapa.

Wakisomewa mashtaka na Mwendesha Mashtaka Sylivia Mitanto  mbele ya Hakimu Wilberforce Luhwago ilidaiwa washtakiwa walitenda kosa hilo Agosti 14 mwaka huu.

Ilidaiwa Joachim Mwaseba (45), Obadia Mwatonoka (28), Obedi Mbotwa (28), Matthew Mwasiposya (62), Kennedy Nsangafuru (21), Geoffrey Kibona (25), Godfrey Gambi (35), Edom Kasengile (39), Boniface Disoni (35) na Martin Mwiba (35) walitenda kosa hilo kinyume na Kifungu cha Sheria Na. 126 na 35 CAP 16 R.E 2002 cha Kanuni ya Adhabu.
Washtakiwa wote walikana kuhusika na tukio hilo hivyo kuachiliwa kwa dhamana

Awali upande wa utetezi chini ya Wakili Msomi Hezron Mwankenja uliiomba mahakama kuipeleka kesi hiyo hadi Novemba 24 mwaka huu kutokana na wakili huyo kupata udhuru ambapo Hakimu Luhwago aliridhia ombi hilo.

0 Comments:

Post a Comment