Mbio za Kilometa tano, na kumi za Uru Fun zinatarajiwa kufanyika Moshi Vijijini mnamo Desemba 30 mwaka huu ikiwa ni sehemu ya kufunga mwaka 2023.
Akizungumza na JAIZMELA Diwani wa Kata ya Uru Kusini Wilhad
Kitari alisema maandalizi yanaendelea.
“Tuko kwenye maandalizi ya Mbio za riadha
zinazofahamika kama Uru Fun Run, ni mbio ambazo ni za hiari
na kupitia mbio hizo zitasaidia zaidi kwa kuwaunganisha wananchi wa Uru
pamoja na Watanzania kutoka nje ya Uru kwa ajili ya kuwaleta pamoja,” alisema
Kitari.
Aidha
Kitari aliongeza kuwa mbio hizo zitakuwa sehemu ya kukuza uchumi wa wakazi wa
Moshi Vijijini
“Mbio hizi zitasaidia sana kukuza uchumi wa wakazi wa Uru
watakaokuja kushiriki mbio hipo, kwani wataweza kununua vitu mbalimbali lakini
pia na kuvifahamu vitu mbalimbali vya Ur,” aliongeza.
Hata hivyo mbio hizo zitaenda sambamba na changizo kwa ajili ya
maandalizi ya mbio za Uru Marathon ambayo itafanyika rasmi mwaka 2024 pia
kusaidia ujenzi wa matundu ya choo katika shule, wasiojiweza na wajane.
“Kupitia mbio hizi tutawahamasisha watu kuchangia kwa maana ya
kujisajili na tunategemea sehemu ya fedha hizo zitakapopatikana ziweze kwenda
kuimarisha shughuli mbalimbali za maendeleo kwenye kata yetu ya Uru. Ikiwemo
ujenzi wa miundombinu ya barabara, ujenzi wa matundu ya vyoo kwenye shule
, kusaidia watu wenye mahitaji maalumu kama vile wazee, watoto yatima na
wajane.
Vyakula mbalimbali kama vile KITOLOLO, NDUTU, VIAZI VIKUU VYA
KUCHEMSHA, NDUU, vitakuwa sehemu ya kuonyesha utamaduni wa wakazi wa Uru
“Tunarudi kuwahamasisha wananchi kurudi kwenye asili yetu,
KISUSIO, kitakuwepo pia kinywaji cha asili cha pombe aina ya MBEGE,
ili kudumisha tamaduni, mila na desturi za wachaga,” alisisitiza Kitari.
0 Comments:
Post a Comment