Marehemu Jeremia Aduram Mkumi (44) |
Mkazi wa Soweto, mjini Moshi aliyefahamika kwa jina la Jeremia Aduram amefariki dunia baada ya kujiua kwa kujinyonga kwa kamba nyumbani kwake.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea Novemba 15 mwaka huu
katika mtaa wa Furahisha, eneo la Sabasaba mjini Moshi ambapo marehemu ambaye
alikuwa mjasiriamali katika soko la Maimoria.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema chanzo cha tukio hilo ni
msongo wa mawazo aliokuwa nao marehemu huyo, na mtoto wake anayefahamika kwa
jina la Acram ndiye aliyekuwa wa kwanza kumuona baba yake akiwa chooni
akining’inia.
“Namfahamu Jeremiah kama Makamu wa soko aliyemaliza muda wake
alikuwa mpambana, ametusikitisha alikuwa jasiri anaongea mbele za watu,kama ni
deni basi sidhani,”
JAIZMELA imezungumza na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Karanga
Augustina Massawe ambako marehemu alikuwa ni Mwenyekiti wa Shule hiyo.
“Tumepokea kwa masikitiko makubwa amekuwa hapa shuleni muda
mrefuJeremiah alikuwa mwema sana sana hata kabla hajawa Mwenyekiti wa Shule
alikuwa na moyo wa kujitolea na alikuwa na huruma,” amesema Mwalimu Massawe.
Aidha Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama wa eneo la Sabasaba Geofrey
Shayo amesema huenda alikuwa na changamoto zake ziliziojificha moyo hivyo
alipaswa kuzungumza na watu badala ya kuchukua uamuzi huo.
“Kwa kweli imeleta mtafuruku, kwasababu mimi ni
mfanyabiashara mwenzangu na angejaribu kuishirikisha jamii haya yote
yasingetokea,” amesema Shayo
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa Juma Mmanga amesema
taarifa za kifo cha mkazi wake alipokea kutoka kwa wananchi wema, ambao
walimchunguza na kuona bado anapumua hivyo kuchukua jukumu la kumpeleka
hospitalini.
“Majira ya saa 10 kumi nilifika hapa nyumbani nikapewa
taarifa, bahati nzuri alikuwa hajafa, lakini wakamwahisha hospitali ambako
alifia, baadhi ya watu wanadai kuwa Jeremiah amechukau uamuzi huo kwasababu ya
madeni, kwasababu ya madeni si kweli Jeremiah mi ni rafiki yangu na mikopo yake
mimi nimekuwa nikisaini,” amesema Mmanga.
Marehemu amefariki akiwa na umri wa miaka 44 ameacha watoto
wawili na mwili waka unatarajiwa kusafirishwa kwenda mkoani Mara siku chache
zijazo.
0 Comments:
Post a Comment