Wasimamizi wa Wafanyakazi mahali pa kazi wametakiwa kufanya uchunguzi wa kina pindi Wafanyakazi wanapokiuka kanuni, taratibu na Sheria za kazi kabla ya kutoa adhabu stahiki ili kubaini makosa yaliyofanyika yametokana na Afya ya Akili au Uzembe.
Akizungumza katika Kikao cha Utekelezaji cha Baraza la Wafanyakazi la Jeshi la Uhamiaji kilichofanyika katika Chuo cha Kikanda cha Uhamiaji Tanzania (TRITA) Meneja Rasilimali watu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Miriam Mbaga amesema kumekuwa na utoaji wa adhabu Kali kwa wafanyakazi pindi wanapokiuka kanuni, taratibu na Sheria za kazi pasipo kuchunguza Kama ni Afya ya Akili au la hatua ambayo imekuwa ikileta majanga mengi kwa baadhi ya wafanyakazi kujiua.
"Kwa mujibu wa taarifa za watalaamu linaonyesha tatizo hili ni kubwa kulingana na aina maisha tunayoishi sasa, maendeleo na mambo mengine, hatutaishia hapa tunao watumishi mikoa yote tutaweka utaratibu wa kuwafikia watumishi wetu ili waelewe tatizo lipo na namna gani wanaweza kujiepusha na tatizo hilo," alisema Mbaga
Katika utoaji wa mada Dkt.Garvin Kweka kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili amesema changamoto ya Afya ya Akili nchini ni kubwa na hatua za makusudi kupambana na Hilo lazima zichukuliwe.
"Kuna watu tunaishi na watu ambao hatujawahi kuwatikisa na tunao na wana viashiria vyote vya kudhuru, siha njema ya akili ni muhimu, kila watu wanne mmoja anakuwa na changamoto ya afya ya akili," alisema Dkt. Kweka.
Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Uhamiaji Kamishna Gerald Kihinga amesema Mada ya Afya Akili imekuwa ya muhimu ili kuongeza ufahamu juu ya suala hilo ili kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza.
"Katika semina hii watu wameanza kujua, kumbe na mimi nina na tatizo la afya ya akili ni vema kuchukua hatua mapema Mtu anakuwa mlevi kupita kiasi, haendi kazini, anafanya kazi chini ya kiwango, wengine wanachukua hatua ya kujinyonga wanahitaji msaada kusaidiwa," alisema Kamishna Kihinga.
Mbali na hilo Mbaga amewataka Wafanyakazi nchini kuanza maandalizi ya Kustaafu ikiwamo kuishi na jamii vizuri wangali Bado makazi ili muda utakapofika wa kurudi uraia wawe na mahusiano mazuri na jamii zao.
Mbali na hilo Mbaga amewataka Wafanyakazi nchini kuanza maandalizi ya Kustaafu ikiwamo kuishi na jamii vizuri wangali Bado makazi ili muda utakapofika wa kurudi uraia wawe na mahusiano mazuri na jamii zao.
"Kuna wengine wanaondoka na vyeo vyao na nafasi zao , na wanapata taabu ya kuishi na jamii, wakiwa kazini akili zao hawaziweka kuwa kuna siku mishahara itakoma, posho zitakoma itabaki pensheni watahitaji kipato kingine, wanapata washauri wabaya matokeo yake maisha yao yanakuwa ni ya duni au mafupi zaidi," alisema Mbaga
Wakitoa shukrani zao za dhati kwa Uwepo wa kikao hicho cha kikatiba washiriki wamelitaka Baraza lizifanyie utatuzi wa haraka changamoto pindi zinapowafikia mezani.
0 Comments:
Post a Comment