Kocha wa zamani wa Timu ya Olimpiki ya Marekani John Geddert amejiua mwenyewe ikiwa ni saa chache baada ya kushtakiwa kwa unyanyasaji wa kingono na biashara haramu ya binadamu.
Geddert aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 63 alikuwa kocha mkuu wa timu ya wanawake ya Jimnastiki katikamichuano ya Olimpiki mwaka 2012. Alifanya kazi kwa karibu na daktari wa timu Larry Nasar ambaye alishtakiwa kwa kuwanyanyasa wanamichezo.
Mwanasheria Mkuu wa serikali wa Michigan Dana Nessel amethibitisha kutokea kwa kifo hicho kwamba kilitokea jana Alhamisi mchana. Nassar alishtakiwa kwenda jela hadi miaka 300 mnamo mwaka 2018 baada ya kukutwa na hatia ya kuwanyanyasa wasichana 250.
0 Comments:
Post a Comment