Mlinda mlango wa Ghana Danlad Ibrahim alikuwa shujaa wa mchezo dhidi ya Simba Wadogo Wasioshindika Cameroon baada ya kuokoa mkwaju wa penati kwenye ushindi wao wa matuta 4-2. Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya 1-1 licha ya kuongezwa dakika 30 kufikia dakika 120.
Cameroon ilipata uongozi katika dakika ya 102 baada ya Mila kukwamisha mpira wavuni. Uongozi huo ulidumu kwa sekunde 70 nyota wa Black Satelaite Boateng kuisawazishia timu yake.
Katika changamoto ya mikwaju ya penati nyota wa Cameroon Goni Ali aligongesha mwamba huku Kevin Prince Mila akishuhudia mkwaju wake ukiokolewa na Danlad. Nyota wa Ghana Daniel Afriyie, Frank Kwabena, Ivan Anokye na Percious Boah walifunga penati zao.
Katika mchezo mwingine kulishuhudiwa Uganda ikiwaadhibu Burkina Faso kwa changamoto ya mikwaju 5-3 ya penati kwenye mchezo uliochezwa katika dimba la Cheikha Boidiya.
Mlinda mlango wa Uganda Komakech aliokoa mkwaju wa Yacouba Djiga na kuwasaidia Viboko hao wa Uganda kutinga nusu fainali. Uganda itacheza nusu fainali yake siku ya Jumatatu itakapowakabili Tunisia ambao wameitandika Morocco kwa changamoto ya mikwaju ya penati 4-1 huku Gambia ikishinda kwa mabao 3-0 dhidi ya Afrika ya Kati.
0 Comments:
Post a Comment