Ferland Mendy (katikati) akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kuifungia bao la ushindi Real Madrid dhidi ya Atalanta. |
Mzunguko wa 16 wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya umeendelea jana kukishuhudiwa Manchester City ikiizabua Borussia Mochengladbach kwa mabao 2-0 kwenye mchezo uliochezwa jijini Budapest nchini Hungaria.
Mchezo huo ulichezwa nchini humo kutokana na vizuizi vikali dhidi ya corona nchini Ujerumani. Bernado Silva na Gabriel Jesus waliiweka katika hatua nzuri Manchester City wakikwamisha mpira wavuni katika dakika ya 29 na 65 mtawalia.
Ushindi huo ni wa 19 mfululizo kwa kikosi hicho cha Pep Guardiola ambao unaiweka katika nafasi nzuri ya kupigania taji la Ligi ya Mabingwa barani humo. Akizungumza baada ya mchezo huo kocha Guardiola alikaririwa akisema waliutawala mchezo huo, licha ya kwamba hakufanya vizuri sana katika umaliziaji kila walipofika katika lango la wapinzani wao.
Guardiola aliongeza kusema kushindwa kutumia nafasi vizuri ni jambo ambalo wanapaswa kulirekebisha katika michuano hiyo. Citizens wanapewa nafasi kubwa ya kutwaa taji hilo kwa mara ya kwanza. Ushindi huo unaifanya kuendelea kusalia katika nafasi ya sita kwa viwango vya ubora wa klabu barani Ulaya msimu huu huku Bayern Munich, Barcelona, Juventus, Real Madrid na Atletico Madrid wakishika nafasi za juu.
Katika mchezo mwingine; Real Madrid ilipata ushindi mwembamba
katika dakika za majeruhi dhidi ya Atalanta. Bao la Ferland Mendy katika dakika
za lala salama lilitosha kuipa matumaini Real Madrid katika hatua hiyo ya 16
jijini. Bernado Silva na Gabriel Jesus
Ushindi huo wa Los Blancos unaifanya Madrid kuwa timu ya kwanza kufikisha mechi 100 za mtoano barani Ulaya tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo.
Katika hatua hiyo Merengues wanakuwa timu ya kwanza kupita ushindi wa mechi 50 ikifikisha ushindi wa mechi 52, sare 17 na ikipoteza 31. Bayern inashika nafasi ya pili ikifikisha mechi 97 katika hizo ikishinda 49 ikifuatiwa na Barcelona waliofikisha mechi 96 wakishinda 46.
Aidha ushindi ulioupata katika hatua hiyo unakuwa wa kwanza baada ya miaka 25 kwa miamba hiyo kushinda kwa taabu kwa mara ya mwisho ilikuwa zama za Raul Gonzalez.
0 Comments:
Post a Comment