Mchezaji wa Gofu maarufu duniani Tiger Woods yupo njiapanda baada ya kupata ajali siku ya Jumanne aliyoipata Kusini mwa California.
Wachambuzi wa michezo duniani nao wapo njiapanda kutokana na nyota huyo mwenye umri wa miaka 45 kupata majeruhi ambayo haijaulikana baada ya kupona kama atarudi katika kiwango chake.
Baada ya ajali hiyo Rais wa zamani wa Marekani Barrack Obama aliandika katika akaunti yake ya twitter; GOAT ikiwa na maana Nyota wa zama zote na kuongeza “ Kama tutakuwa tumejifunza kitu chochote kwa miaka mingi, basi huwezi kumweka pembeni Tiger.”
Mwaka 2019 Woods alitwaa taji la 15 kwenye michuano ya Masters kwenye viunga vya Augusta; licha ya kuzidiwa na Mmarekani mwenzake Jack Nicklaus ambaye amefikisha mataji 18. Nyota huyo amekuwa katika ubora kwenye mchezo huo kwa miaka 25 na kupata mafanikio makubwa.
0 Comments:
Post a Comment