Ukweli na Kuheshimiana ni kiini ujenzi wa jamii zetu

Ulimwenguni kwa sasa kumejaa habari potofu na upotoshaji, ni muhimu kuhakikisha kwamba ukweli na kuheshimiana vinakuwa kiini kwa ujenzi wa jamii zetu.

Mapambano dhidi ya Habari za Uongo hayapaswi kukoma

Habari za uongo, habari za uongo zinazosambazwa kwa lengo la kumdhuru mtu au jambo fulani, huifanya jamii kuwa na sintofahamu. Zinaweza kutumika kwa madhumuni ya kiitikadi, kisiasa au hata uhalifu, kama vile ulaghai mtandaoni unaolenga kuiba data ya kibinafsi.

Utandawazi na Athari zake katika Uandishi wa Habari

Katika jamii yetu ya kisasa, ambapo habari ziko kila mahali na zinaweza kupatikana kwa kila mtu, mara nyingi ni ngumu kutofautisha kati ya vyanzo vya kuaminika na habari bandia.

Uandishi wa Habari nguzo msingi mkuu kwa ujenzi wa jamii inayojitambua

JAIZMELA blog ni miongoni mwa vyanzo vya habari, zilizochakatwa kwa kuzingatia miiko ya uandishi wa habari.

Mila na Desturi ni nguzo muhimu

Mila na desturi ni nguzo muhimu sana katika utamaduni wa jamii yoyote ile; mila ni sawa na sheria zisizoandikwa. Mila ni taratibu za maisha na mwenendo zinazofuatwa na jamii fulani katika utendaji kulingana na historia na utamaduni wao. Mila zinatambulisha maadili ya jamii husika, huelezea namna jamii inavyoendesha mambo yake.

Saturday, February 4, 2023

CCM Mwanga yaandikisha Wanachama Wapya 124

Mwenyekiti wa CCM  Wilaya ya Mwanga  Mwl.  Ibrahim  Mnzava akimkabidhi mwanachama mpya kadi ya kielektroniki kwenye hafla ya kuadhimisha miaka 46 ya kuzaliwa kwa chama hicho, katika Ofisi ya Kata ya Lang’ata,Mwanga. (Picha na Kija Elias)



Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mwanga, kimeandikisha wanachama wapya 124 hafla ambayo imeenda sambamba na upandaji wa miti 50 kwenye kituocha Afya Lang’ata. 

Hayo yanajiri ikiwa ni maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa kwa CCM ambayo kila kata, wilaya mkoani hapa zimeadhimisha kwa kufanya shughuli mbalimbali katika maeneoyao huku ikitarajiwa kimkoa kufanyika wilayani Same. 

kimesema maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa kwa CCM ni kielelezo cha umoja wa kitaifa uliokengwa kwa misingi ya Amani, mshikamano na utulivu uliopo hapanchini Tanzania. 

Akizungumza katikamaadhimisho hayo Mwenyekiti wa CCM  Wilaya ya Mwanga  Mwl.  Ibrahim  Mnzava, alisema ni jukumu la kila mwanachama kuzielekeza katika kukiimarisha na kukijenga chama kwani mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 46 ya CCM  ni mengi. 

Kwa upande wake Kaimu Katibu wa CCM Wilaya ya Mwanga Paulo Bina, amesema katika maadhimisho hayo wamefanikiwa kupanda miti 50 kwenye  kituo cha afya Lang'ata,  kuingiza wanachama wapya 124 pamoja na kuwapatia kadi mpya za kieletroniki wanachama 74.









 

Thursday, February 2, 2023

KUELEKEA MIAKA 46 YA CCM: UPANDAJI MITI WAFANYIKA KATA YA MAWENZI,MOSHI

Mwalimu wa Mazingira katika shule ya Msingi  Uhuru, Fadhila Mvungi; alisema

 ● Kuna faida nyingi za upandaji miti kwenye maeneo ya shule ambayo yanawafanya watoto waweze kusoma katika mazingira mazuri, safi na kupata hewa safi. 

● Mazingira mazuri yanawafanya watoto waipende shule yao na pia inakuwa na kuvutio kwa wanafunzi wengine na wazazi kupenda kuwaleta watoto kusoma katika shule yetu, kutokana na kuwa na mandhari mazuri. 

● "Namshukuru sana Diwani wa Kata ya Mawenzi Apaikunda Naburi, kwa mchango wake katika suala la mazingira kwenye shule yetu ya msingi Uhuru, awali kulikuwa na jangwa kubwa sana kwenye shule.yetu lakini diwani amejitahidi kila mwaka kutuletea miti ya vivuli na matunda  na kushiriki kupanda,"

 




HOTUBA YA DIWANI WA KATA YA MAWENZI APAIKUNDA NABURI MANISPAA YA MOSHI MJINI KATIKA KAMPENI YA UPANDAJI MITI KUELEKEA MAADHIMISHO YA MIAKA.46 TANGU KUANZISHWA KWA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) INAYAOFANYIKA LEO TAREHE 02 JANUARI 2023.


Shule ya Msingi Mawenzi iliyopo Manispaa ya Moshi miongoni mwa maeneo zoezi la upandaji miti lilifanyika kuelekea miaka 46 ya kuanzishwa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM).



UTANGULIZI; 

NDUGU Wananchi wa Kata ya Mawenzi na vuinga vyake kwanza napenda kuchukua fursa hiikumshukuru Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema na upendo, kumiwezesha kuwa nanyi hii leo.katika zoezi la upandaji wa miti ili kukabiliana na mabadiliko ya taiba nchi,.

Pia naishukuru kwa dhati Serikali ya awamu ya sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  chini ya Mhe; Dkt. Samia Suluhu Hassan na chama cha Mapinduzi  (CCM) kunipa ridhaa tena ya kuwahudumia wakazi wa kata hii ya Mawenzi.

Vilevile napenda kuwashukuru Makamu wa Rais Dkt. Philip Mapango na Waziri Mkuu Mhe; Kasim Majaliwa (Mb) pia Mstahiki Meya wa Ma ispaa ya Moshi.Injinia Zubery Abdallah Kidumo, kwa miongozo na.maelekezo wanayoyatoa kuhakikisha mangira yanaendelea kutunzwa.

Ndugu Wananchi baada ya maelezo haya ya utangulizi,  Sote tunafahamu duniani kwa sasa inahangaika kutafuta suluhisho namna ya kulinda safari hii dhidi ya mabadiliko ya tabia ya nchi,  kutokana na matukio mengi ya ukame na mafuriko kupindukia kiwango kinachotakiwa.

Mabadiliko ya tabia nchi  yapo na husababishwa haswa na shughuli za kibinadamu, kwa sasa kumekuwa na mkusanyiko wa gesi ya hewa ukaa kwenye mazingira duniani ambako kunahusishwa moja kwa.moja na wastani wa kiwango cha joto duniani.

Shirika la Kimataifa la Mpango wa mazingira (UNEP) linasema asilimia 30 ya idadi ya watu ulimwenguni wanakabiliwa na mawimbi ya joto yanayotokea 

Ndugu Wananchi, upandaji wa miti katika mazingira yetu unachangia kwa kiwango kikubwa katika kutunza.mazingira kwa.kuzuia kuenea hali ya jangwa kupitia kuleta mvua na pia kutunza vyanzo vya maji ardhini.

Ndugu Wananchi; Mkoa wetu wa Kilimanjaro sote tunafahamu hapo awali ulikuwa na hali ya hewa nzuri , mvua za kutosha lakini kwa sasa kama mnavyoona hali imebadilika mkoa wetu ulikuwa na misimu miwili ya mvua tulikuwa na mvua za vuli na masika lakini kwa sasa mvua za.vuli.imetoweka kwasababu ya uharibifu wa mazingira na ukataji wa miti hovyo.

Wote mnashuhudia kwa sasa Manispaa yetu ya Moshi, tumeshuhudia mgao wa maji ambao.umeanza leo hii ni miongoni mwa  mabadiliko makubwa ya tabia nchi, jambo kama hili halikuwqhi kuwepo katika mazingira yetu.

Ndugu Wananchi, leo tunapanda miti takribani 100 kwa ajili ya kukabiliana na hali mbaya ya hewa katika siku za usoni kama tusipochukua hatua madhubuti jambo la.msingi ni kuitunza , tumeanza leo lakini uangalizi madhubuti unapaswa kuzingatiwa ili miti hii iwe chachu ya kutunza vyanzo vya maji na viumbe wa majini na nchi kavu ambao ni muhimu kwa maendeleo ya taifa letu.

Mimi na wewe ndio chanzo cha yote haya, lakini pia mimi na wewe ndio suluhisho  muhimu katika kuirudisha Kilimanjaro ya zamani yenye hali ya hewa nzuri ya kuvutia.

Ndugu wananchi wa Kata  ya Mawenzi nihitimishe kwa kusema ili kukabikiana na hali ya hewa na mabadiliko ya tabia nchi inatupasa sote tufanye kwa vitendo sio kuzungumza pekee.

Shughuli za kibinadamu utupaji wa taka zikiwemo za plasitiki zinabadilisha hali ya hewa na mazingira kwa ujumla. Tusaidiane kudhibiti ili kuitengeneza kata yetu Mawenzi,  Moshi  yetu, Kilimanjaro  yetu, Tanzania yetu na dunia kwa ujumla

AHSANTE  KWA KUNISIKILIZA.


Tuesday, January 31, 2023

Mwalimu Nyerere: Shule ni Kiwanda au Shamba


 "Shule ni mahali pa kujifunza, hatutaki kubadili wazo hili, Haifai shule iwe kiwanda au shamba. Lakini lazima shule iwe kiwanda au shamba. Lakini ni lazima tuone kuwa kazi katika kiwanda cha shule au katika shamba la shule ni jambo la kawaida katika shughuli za kujifunza kuishi."

Saturday, January 28, 2023

Simba fans trust new appointed CEO Imani Kajula

 

Imani Kajula, new CEO of Simba SC

Trust is of utmost importance and an integral part of happy and fulfilling relationships, for both professional as well as personal relationships. 

Without trust, relationships are like a life without oxygen. You will feel suffocated and fail to maintain because one or both parties feel insecure or let down.

Lincoln Davenport Chafee is an American politician. He was mayor of Warwick, Rhode Island, from 1993 to 1999, a United States Senator from 1999 to 2007, and the 74th Governor of Rhode Island from 2011 to 2015.

Chafee said, “Trust is built with consistency.”



UWT Moshi vijijini yajitayarisha kujenga Chuo cha Ushonaji

Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Moshi Vijini imekusudia kujenga Chuo cha Ushonaji ili kuwawezesha wanafunzi walioshindwa kuendelea na masomo ya elimu ya juu ili waweze kujiimarisha kiuchumi. 

Hayo yalisemwa Januari 27,2023 na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Rwaichi Kaale kwenye mkutano  mkuu wa kwanza wa Baraza la Jumuiya hiyo uliofanyika kwenye ukumbi wa chama hicho Wilayani humo. 

Akizungumzia mpango kazi wa miaka mia Tano 2022-2027 Kaale amesema Jumuiya hiyo inakusudia kuwa na miradi ya kitegauchumi ili kuiwezesha Jumuiya hiyo kujiendeleza pasipo kutegemea wafadhili. 

Kaale aliitàja miradi hiyo ni pamoja na Chuo  cha ushonaji, kuanzisha kikundi cha mapishi, kuwa na mgahawa wa chakula na vinywaji pamoja na vyombo vya usafri kama vile bajaji. 

Katika hatua nyingine  Mwenyekiti wa UWT  Moshi Vijijini aliwaomba Wajumbe wa Baraza hilo kuvunja makundi na kuwataka kufanya kazi kwa pamoja ili kuendelea kuijenga Jumuiya hiyo na chama kwa ujumla. 

Kwa upande wake Katibu wa UWT Moshi Vijijini Shakila Singano, alisema katika kuadhimisha miaka 46 ya kuzaliwa kwa CCM  Jumuiya hiyo imeshiriki upandaji wa miti pamoja na kuwasajili wanachama wapya 500 kwa mfumo wa Kieletroniki ambapo matarajio ni kusajili wanachama 3,000 kwa mwaka 2023. 

Akifungua kikao hicho Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya Moshi Vijijini Ramadhan Mahanyu amesema Serikali ya awamu ya sita imeipatia Wilaya hiyo kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni mbili ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya chama. 

Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la UWT  Moshi Vijijini Gladness Mbwambo na Arapita Lyimo, wamesema uanzishwaji wa miradi ya kiuchumi ndani ya Jumuiya hiyo itaiwezesha UWT kuondokana na utegemezi sambamba na kuwasaidia vijana wa kike kujiepusha na ndoa za utotoni.




 

 

Polisi, DC Mwaipaya wafanya usafi kituo cha Afya Mwirange-Mwanga

 

Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Watumishi wa kituo cha afya Mwirange, Januari 28,2023 wameshiriki zoezi la usafi wa mazingira katika baadhi ya maeneo yanayozunguka kituo hicho cha afya  ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mahusiano baina yao na wananchi ili kukabiliana na vitendo vya uhalifu. 

Akizungumza mara baada ya zoezi la usafi Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Wilaya ya Mwanga (SSP) Hendry Nguvumali alisema, jeshi la polisi nchini lina kawaida ya kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi. 

SSP Nguvumali  alisema askari polisi wilaya ya Mwanga wameamua kuungana na wafanyakazi wa kituo cha afya Mwirange, ili kufanya usafi, lengo likiwa ni kuwa karibu na jamii pamoja na kutoa elimu kwa jamii itakayo lenga usalama wa Raia na mali zao, katika kuzuia na kupambana na uhalifu. 

Akishiriki zoezi la usafi Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Abdallah Mwaipaya alisema serikali wilayani humo imeungana na jeshi hilo katika kufanya usafi katika eneo ambalo linatoa huduma za afya kwa wananchi. 

Mwaipaya alisema maeneo ya kutolea huduma za afya yanapokuwa na mazingira salama yanasaidia kuepusha kuwepo kwa maambukizi mbalimbali ya magonjwa yasiyakuambukiza kwa wananchi wanaofika katika kupata huduma za kimatibabu. 

Alisema wilaya ya Mwanga inazo kata 20 na kati  ya hizo kata 16 zote zina polisi jamii na kwamba uwepo wa askari hao, umesaidia kupunguza changamoto za wananchi hao kusafiri kwenda katika kituo kikuu kupeleka mashauri mbalimbali. 

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Mwirange Dkt. Yosya Foya, alisema kwenye kituo hicho wagonjwa wengi wanaofika kwa ajili ya kupatiwa matibabu wengi wao wanasumbuliwa na ugonjwa wa homa ya mapafu, kuharisha na malaria. 

Akizungumza Dkt. Afath Mohamed na Dkt. Joyce Kangero, walisema changamoto ya maradhi ambayo wakazi wa wilaya ya Mwanga wamekuwa wakiugua  na kuletwac katika kituo hicho cha afya yanaweza kuzuilika endapo watazingatia zaidi elimu ya afya ambayo imekuwa ikitolewa na wataalamu hao wa afya. 

Zoezi la usafi wa mazingira hufanyika kila Jumamosi ya mwisho wa kila mwezi ambapo Januari 28 mwaka huu Jeshi la Polis8i Mwanga kwa kusirikiana na uongozi wa serikali ya wilaya na uongozi wa kituo cha afya Mwirange wameshiriki kufanya usafi katika kituo hicho.





Tuesday, January 24, 2023

PICHA: Namna Chifu Mwariko alivyopumzishwa katika makaburi ya Manyema mjini Moshi







CHIFU ATHUMAN Omary MWARIKO “Mhelamwa” :Huyu ni yule aliomba noti ya Tanzania ichapishwe picha ya Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli, pia ndiye huyu aliomba mlima Kilimanjaro ufunikwe pazia, ndiye huyu aliandaa kinyago na kumpelekea Rais wa Urusi Vladmir Putin kwa ajili ya kufanikisha Kombe la Dunia 2018.


Chifu Mwariko is no more

 

Chifu Athuman Mwariko enzi za uhai wake

Mwili wa marehemu Chifu Mwariko ukiwa katika jeneza kuelekea makaburini Manyema, Moshi Mjini

Mkurugenzi  wa Taasisi ya Sanaa ya Kilimanjaro Cultural Heritage  Centre ya mkoani Kilimanjaro, Chifu Athuman Omari Mwariko amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 79.

Taarifa za familia ya Chifu Mwariko zinasema alifariki dunia alfajiri ya Januari 22,2023 nyumbani kwake Maili Sita, na kuzikwa Jumatatu ya Januari 23,2023; saa 12 jioni.

Familia yake ilisema marehemu alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo ambapo siku chache kabla ya kifo chake alidai kuishiwa nguvu hadi umauti ukamkuta.

Chifu Mwariko aliwahi kufanya kazi na Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere pia Malkia Elizabeth II wa Uingereza.

Mwishoni mwa mwaka 2022 alimkabidhi Kifimbo Chifu Frank Marealle, mwenyekiti mstaafu wa Umoja wa Machifu Tanzania (UMT) na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi Mhandisi Zuberi Kidumo.

TAARIFA ZILIZOPITA  ZA CHIFU MWARIKO

BONYEZA LINKI HIZI

https://jaizmelanews.blogspot.com/2020/07/wizara-ya-fedha-yashauriwa-kuchapisha.html

https://jaizmelanews.blogspot.com/2020/11/mhelamwana-amkabidhi-kifimbo-mbunge.html

https://jaizmelanews.blogspot.com/2021/08/chifu-mwariko-ataka-chanjo-ya-uviko-19.html

https://jaizmelanews.blogspot.com/2022/06/kilimanjaro-cultural-heritage-centre.html

https://jaizmelanews.blogspot.com/2022/07/wasanii-wa-kilimanjaro-waishio-dar.html

https://jaizmelanews.blogspot.com/2022/10/chifu-marealle-akabidhi-madaraka-aonya.html

https://www.youtube.com/watch?v=8REybEtLY-4

https://www.facebook.com/johnson.jabir.735/videos/294583529107769

 

UVCCM Moshi Mjini yapanda miche 3,000

 

UVCCM Moshi Mjini wakiwa na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwenge katika zoezi la upandaji wa miti kuadhimisha miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi.

Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Wilaya ya Moshi Mjini  umewataka Vijana wa Jumuiya hiyo kusimamia misingi ya jumuiya hiyo kwani ndiyo nguzo kuu ya chama inayozalisha viongozi mbalimbali wa chama na Serikali. 

Akizungumza katika zoezi la upandaji miti ya matunda katika shule ya Msingi Mwenge iliyopo kata ya Kiusa Januari 24,2022 Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Sadath Sudi Ndibalema alisema UVCCM ni nguzo kuu inayopaswa kuzingatiwa katika mustakabali wa taifa hivyo vijana walioko ndani ya chama kuhakikisha kwamba wanaendelea kusimamia misingi hiyo.

Chama cha Mapinduzi kuliundwa Februari 5,1977 baada ya kuunganishwa kwa vyama vya Tanganyika African National Union (TANU) cha iliyokuwa Tanganyika, na Afro-Shiraz cha Zanzibar.

Azma ya zoezi la uoteshaji wa miche ya miti katika shule hiyo, Ndibalema alisema lengo ni kuweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi sambamba na wanafunzi kupata lishe ya wanafunzi hao.

Mkuu wa shule ya Msingi Mwenge Hellena John alisema, shule hiyo ilikuwa na uhitaji mkubwa wa miche ya miti ya matunda na kuipongeza Jumuiya ya Umoja wa Vijana kwakuweza kuwapatia miche hiyo.

Mkuu wa Shule ya Msingi Mwenge Bi. Hellen John

Katibu wa UVCCM Wilaya ya Moshi mjini Arafati Mbiruka alisema Jumuiya hiyo ya Vijana  wameamua kuotesha miti ya matunda katika shule ya msingi Mwenge ili kuboresha mazingira ya shule hiyo sanjari na wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo kupata matunda lishe ili kuboresha afya zao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kiusa, Khalid Shekoloa aliishukuru Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa UVCCM Manispaa ya Moshi kwa kuwezakupanda miti ya matunda katika shule hiyo kwani itakwenda kusaidia utatuzi wa changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi sanjari na kuwaomba wanafunzi wa shule hiyo kuendelea kuitunza 

Aidha Shekoloa amewataka kupanda miti kwa wingi itakayosaidia utunzaji wa mazingira ili kwenda sambamba na mpango wa Serikali wa upandaji miti ili kuzuia athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Sadath Ndibalema, mwenyekiti wa UVCCM Moshi Mjini

Naye Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Moshi Mjini kutoka kundi la Vijana  Ashiraf Baraka Malya, walisema bado kuna changamoto ya uelewa kwa jamii juu ya upandaji wa miti na utunzaji wa mazingira.

“Upandaji miti ulioendeshwa na UVCCM Wilaya ya Moshi Mjini katika kuadhimisha miaka 46 ya kuzaliwa kwa CCM, itakwenda kuboresha mazingira ya shule huku akitoa wito kwa wanafunzi hao kuitunzana kuilinda ili kuwana mazingira yaliyo salama,”alisema Malya.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwenge mjini Moshi wakiwa na miche ya miti

Zoezi la upandaji wa miti ni ikiwa ni maandalizi ya kuadhimisha miaka 46 ya kuzaliwa kwa CCM. Chama cha Mapinduzi kuliundwa Februari 5,1977 baada ya kuunganishwa kwa vyama vya Tanganyika African National Union (TANU) cha iliyokuwa Tanganyika, na Afro-Shiraz cha Zanzibar.

Stempu za Posta zikionyesha mambo mbalimbali ambayo Chama cha Mapinduzi iliyoyafanya ndani ya miaka 10 baada ya kuanzishwa kwake,ikiwamo Azimio la Arusha kutoka awamu ya kwanza na mwanzoni mwa awamu ya pili enzi za utawala wa Mwalimu Juliuys Kambarage Nyerere na Ali Hassan Mwinyi.




Wednesday, January 11, 2023

UVCCM Moshi Mjini yamjia juu Juma Raibu

 

Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Moshi Mjini umemjia juu aliyetimuliwa Umeya wa Manispaa Juma Raibu kuacha kukikosoa chama chake hadharani hususani katika mitandao ya kijamii na badala yake kupeleka changamoto hizo kwa kufuata utaratibu wa chama.

Akizungumza  katika Kikao cha Kamati ya Utekelezaji ya CCM wilaya ya Moshi Mjini, Mwenyekiti wa  Sadath Sudi Ndibalemwa, alisema wako baadhi ya watu wachache ambao ni wana chama, baada ya kushindwa kuchaguliwa kwenye nafasi walizokuwa wameziomba kwenye chaguzi zilizomalizika hivi karibuni ndani ya chama hicho, wameunda kikundi cha kuanza kukichafua chama na viongozi wake  kwa kutumia mitandao ya kijamii.

Licha ya Ndibalemwa kutomtaja moja kwa moja Juma Raibu lakini mitandao ya kijamii ya aliyekuwa Meya wa Manispaa hiyo na Diwani wa kataya Bomambuzi  ameonyesha ukosoaji mkubwa wa chama hususani baada ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu kutangaza kuanza kwa mikutano ya hadhara kwa vyama vyote vya siasa nchini baada ya kuzuiwa enzi za utawala wa Dkt.John Pombe Magufuli.

Sadath Sudi Ndibalemwa,Mwenyekiti wa UVCCM wilaya wa Moshi Mjini

Katika akaunti ya Juma Raibu katika Instagram mnamo Januari 9,2023 aliandika, “Nemesikitishwa sana na baadhi viongozi wa chama changu mkoa na wachache wilaya na baadhi ya wanachama, kulaumu kuhusu Mh Rais Samia Kuruhusu mikutano ya hadhara, hakika huu ni udhaifu mkubwa sana na nikukimbia majukumu walioomba kwa Kuzoea kulala usingizi hakuna ushindi bila jasho…”

Juma Raibu anayefahamika kama ‘Man of the People’ yaani mtu wa Watu aliongeza katika utoaji wake wa maoni katika Instagram kuwa, “Twendeni kwa wananchi kusema yanayofanywa na CCM yetu na sio kuogopa mikutano tujipime kwa nguvu zetu Na sio kubebwa " hongera Mama Samia…tukutane Kazini”

Katika kuunga mkono juhudi zake Juma Raibu, wafuasi wake nao wameendelea kutoa maoni yao huku wakimtaka kukaza kamba zaidi

“Hao viongozi wa CCM wanaolalamika kwa nini mama karuhusu mikutano ingekuwa bora wangejiondoa kwenye nafasi zao, wawapishe watu wanaoweza kukisemea Chama. Viongozi dizaini hiyo ni wale waliozoea : " MSEREREKO " !!!!., Wana haja gani ya kuwa kwenye nafasi zao? waache uvivu walishazoea kulala usingizi. waamke...”alisema mfuasi aliyejitambulisha kwa jinala Job Faustine.

Viongozi wengine wa CCM waliojibu hoja za Juma Raibu ni Mrindoko Mwidadi ambaye ni Mwenyekiti wa Juumuiya ya Wazazi Tanzania mkoa wa Kilimanjaro alisema, “Viongozi gani wa Mkoa na Wilaya kwani tupo Mkoani?? pima maneno ya kuandika na kusema kwani ukiambiwa uthibitishe hili usije sema unaonewa!”

Kwa upande wake Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM (W) Moshi Mjini, Issa Bulilo alisema, “Hii sio sawa mkuu Viongozi wa Chama ngazi ya Mkoa na Wilaya wamelalamika wapi kufuatia Mh Rais kuruhusu mikutano??

Mnamo Januari 3,2023 Rais Samia aliruhusu mikutano ya vyama vya siasa baada ya marufuku ya miaka zaidi ya 6 iliyowekwa na mtangulizi wake, hayati John Magufuli.