Mzee Chifu Omary Athuman Mwariko kwa jina maarufu “Mhelamwana” ni Msanii wa uchongaji vinyago ambaye pia aliwahi kuchonga fimbo alichokuwa akikitumia Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, maarufu kama ‘Kifimbo cha Mwalimu’.
Chifu Mwariko, jana alimkabidhi fimbo nyingine na kumkabidhi Mbunge mteule wa Jimbo la Moshi Mjini Priscus Tarimo kama alama ya Uongozi.
Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ameacha alama nyingi zinazodumu hadi leo, moja wapo ikiwa ni kifimbo ambacho mara kwa mara alikuwa akitembea nacho kiasi cha kumpa umaarufu na kikaitwa Kifimbo cha Mwalimu.
Inawezekana Mwalimu Nyerere alikuwa na vifimbo vingi, alivyokuwa akivitumia , lakini Mzee maarufu wa uchongaji vinyago na uchoraji Chifu Omary athuman Mwariko kwa jina maarufu “Mhelamwana” ambaye kwa sasa anaishi maeneo ya Maili sita wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro.
Mwariko alisema ameamua kumchongea kifimbo Mbunge mteule wa Jimbo la Moshi Priscus Tarimo kama heshima ya uongozi kutokana na jimbo hilo kuwa ndani ya upinzani toka mfumo wa vyama vingi kuanzishwa mwaka 1995.
Alisema tangu kuasisiwa kwa mfumo wa vyama vingi, Jimbo la Moshi mjini, lilikuwa ngome ya upinzani, ambapo mwaka 1995 hadi 2000, Chama Cha NCCR-Mageuzi kilianza kulishikilia jimbo hilo.
“Tangu mfumo wa uchaguzi wa vyama vingi kuanzishwa hapa nchini Mwaka 1995, Cha cha NCCR-Mageuzi kilichukua jimbo la Moshi mjini kuanzia kipindi cha 1995 hadi 2000 na mwaka 2000 hadi 2020 Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) lilishikilia jimbo hilo kwa vipindi vinne mfululizo,”alisema.
Anafafanua kuwa “Fimbo hii atakuwa akiitumia kila aendako iwe kwenye Bunge, mikutano yeke na wananchi wa jimbo lake, fimbo hiyo pia itakuwa ikimlinda , popote itakuwa inang’aa, alisema na kuongeza kuwa fimbo hiyo inajulikana kama “Nyangasi Mwana Mnungu” ikiwa na maana kwamba Fimbo ya Mungu.
Mwaliko anasema Kila kiongozi ni sharti awe na fimbo ya kuongozea, ameongeza kusema kuwa alimtengenezea Hayati Mwalimu Nyerere fimbo yake ya kwanza wakati akianza uongozi mwaka 1960 na baadaye alimkabidhi fimbo hiyo mwaka 1967 alipotembelea Mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
“Mimi ndiye nina siri ya mti uliotumika kuchongea fimbo hiyo na wala hakuna nguvu za ziada au muujiza kama watu wanavyozusha,”anasema Chifu Mwariko.
Kwa upande wake Mbunge mteule wa Jimbo la Moshi Priscus Tarimo, nimeipokea kwa heshima kubwa sana, fimbo hiyo,
Mwariko alikuwa mgombea mwenzangu, hata kile kifimbo cha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ni yeye alikitengeneza hivyo na mimi kifimbo hiki ninaamini kitakuwa na Baraka kubwa kwangu katika utendaji kazi wa majumu yangu kwa wananchi.
“Fimbo hii itakuwa na baraka kubwa kwangu itanisaidia kwenye majukumu yangu, nimshukuru sana Chifu Mwariko kwa kunipatia fimbo hii,”alisema.
Aidha Chifu Mwariko amempongeza Rais Mteule Dkt. John pombe magufuli kwa ushindi wa kishindo baada ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa Oktoba 28 mwaka huu.
0 Comments:
Post a Comment