MASHINDANO ya michezo ya Mashirika ya Umma, Kampuni na Taasisi binafsi maarufu Shimmuta yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi jijini Tanga kuanzia Novemba 20 mwaka huu katika viwanja vya Mkwakwani.
Michezo takribani 12 inatarajiwa kuchezwa kwa kipindi cha siku 14 ikiwamo mpira wa pete, kikapu, kandanda, riadha na michezo ya jadi kama karata, bao, drafti na vishale.
Taarifa ya hivi karibuni iliyotolewa Mwenyekiti wa Shimmuta Hamis Mkanachi ilisema ufunguzi wa mashindano hayo utafanywa na makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Mkanachi aliongeza kuwa timu 38 kutoka katika taasisi za umma, binafsi na makampuni zitajitupa viwanjani.
“Tumekuja Tanga kwa ajili ya mashindano haya ya kila mwaka na baada ya mwaka jana kufanyikia Mwanza leo tupo Tanga kwa ajili ya mashindano haya ambayo kwa mujibu wa kalenda yatafanyika kwa takribani siku 14,” alisema Mkanachi.
Hata hivyo Mkananchi alipata fursa ya kuzungumza mambo kadha wa kadha kuhusu mashindano hayo ikiwamo suala la udanganyifu kwa wachezaji.
“Tunatarajia kila atakayeshiriki michezo hii atakuwa ni mfanyakazi asilia na siyo vinginevyo na endapo patatokea udanganyifu wowote Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) watafanya kazi yao,” aliongeza Mkanachi.
Mwenyekiti huyo aliweka msisitizo kuhusu utumiaji huo wa wachezaji mamluki kwani kwa kufanya hivyo kutapoteza ladha ya mashindano ya Shimmuta.
Awali wakati Shimmuta wakikaribishwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigella aliwataka wasijiingize katika kashfa mbalimbali ikiwamo ya matumizi ya vitu vya ziada ili kuongeza nguvu ili waweze kupata ushindi.
“Vyombo vya dola vipo sio vitamhusu yule aliyeingizwa kucheza au atakayetumia dawa za kusisimua misuli lakini hata viongozi kwasababu walikuwa wanajua nani waliyemuingiza kwenye mashindano kwa hiyo msijiingize kwenye mchezo huo.
Kauli ya RC Shigella sio ya kuiacha hivi hivi katika ulimwengu huu wa usasa. Kampeni hii ya kutumia dawa za steroidi anaboliki maarufu dawa za kusisimua misuli ni suala la kimataifa ambalo halipaswi kuzungumzwa kwa mdomo na kuachwa hivi hivi.
Jarida American Academy of Family Physicians linasema: “Vijana milioni moja hivi [nchini Marekani] walio na umri wa kati ya miaka 12 na 17 wametumia dawa zinazoongeza nguvu mwilini.”
Mojawapo ya dawa maarufu zaidi zinazoongeza nguvu mwilini ni steroidi ambazo huongeza ukubwa wa misuli.
Ripoti moja ya Afya nchini Marekani ilisema, “Dawa za steroidi za kuongeza ukubwa wa misuli ni kemikali zinazohusiana na homoni za kiume (androgens). Dawa hizo huchochea ukuzi wa misuli ya kiunzi na kusitawi kwa maumbile ya kiume.
Steroidi zilitengenezwa viwandani kwa mara ya kwanza katika miaka ya 1930 ili kuwatibu wanaume ambao walishindwa kutokeza homoni za kutosha.
Katika zama za usasa steroidi hutumiwa kurekebisha kudhoofika kwa mwili kunakosababishwa na virusi vya Ukimwi na magonjwa mengine. Hata hivyo, steroidi hutumiwa sana na watu wasio na uhitaji wa kitiba.
Katika miaka ya 1950, steroidi zilianza kupatikana kimagendo, na wanamichezo waliojitakia sifa walianza kuzitumia kuongeza nguvu mwilini.
Hata hivyo, sio wanamichezo tu ambao hushawishiwa kutumia steroidi. Uchunguzi uliochapishwa katika jarida la kitiba Pediatrics unakadiria kwamba karibu asilimia 3 ya wavulana na wasichana nchini Marekani walio na umri wa miaka 9 hadi 13 wametumia dawa hizo.
Unaweza kujiuliza Kwa nini watu wengi zaidi wanatumia vibaya steroidi? Sababu moja ni kwamba wana-michezo wazuri wanaweza kupata sifa na utajiri haraka.
Inaonekana kwamba steroidi zinaweza kumfanya mtu apate vitu hivyo haraka zaidi. Kocha mmoja maarufu alifunua waziwazi mtazamo ambao wengi huwa nao aliposema: “Hakuna jambo jingine muhimu isipokuwa kushinda.”
Steroidi huwawezesha vijana wengi wajifanye kuwa wajasiri kwa sababu ya kuwa na mwili wenye misuli mikubwa.
Wasichana fulani hutumia steroidi ili wawe na nguvu na waboreshe uwezo wao wa kukimbia. Hata hivyo, inaonekana kwamba wengi wao hutumia dawa hizo wakitumaini zitawafanya wawe na maumbo membamba, yaliyo wima ambayo wanamitindo na waigizaji maarufu wa sinema leo hujivunia.
Mnamo mwaka 2005 Charles Yesalis, Profesa wa Afya na Ukuzi wa wanadamu katika Chuo Kikuu cha Jimbo la Pennsylvania alisema, “Katika miaka ya 1990 wasichana walianza kuzitumia zaidi, na sasa wanazitumia kwa kiasi kikubwa zaidi.”
Shigella ametimiza wajibu wake wa kuwakumbusha Shimmuta kuhusu matumizi ya dawa hizo lakini swali linakuja Kamati ya Olimpiki ya Tanzania (TOC) ambaye ndiye mlezi wa vyama vyote vya michezo nchini wamekuwa wakitoa elimu na kuchukua vipimo kwa wachezaji.
Mara kadhaa tumekuwa tukiona hatua zikichukuliwa kwa wachezaji wanapotaka kushiriki michuano ya kimataifa lakini humu humu nchini bado ni mwendo wa kinyonga.
Juhudi za kupambana na dawa za kusisimua misuli zinaonekana kwa vyama vya riadha na tenisi ambavyo vimekuwa vikijitahidi kutoa elimu na kuchukua hatua. Kwa mfano mnamo mwaka 2017 shirikisho la riadha Tanzania (RT) liliwafungia kushiriki mashindano yoyote wanariadha Elia Sidame na Msandeki Ikoki baada ya kugundulika kutumia dawa hizo. Adhabu ambayo itadumu hadi mwaka 2021.
Katibu Mkuu wa wakati huo wa RT, Wilhelm Gidabuday alisema wanariadha hao Sidame na Ikoki waligundulika kutumia dawa aina moja ya Norandrostorene katika mashindano waliyoshiriki mwaka 2016 na 2017 nchini China na Brazil.
Gidabuday alisema RT pamoja na kupata taarifa kutoka shirikisho la riadha la Dunia (IAAF) juu ya wanariadha hao, lakini hawa kuchukua hatua mara moja kwani nao walikuwa wanafanya uchunguzi kabla ya kutoa hukumu.
Aidha mwaka 2014, Sara Ramadhan alifungiwa miaka mitatu baada ya kugundulika kutumia dawa za kusisimua misuli akiwa Brazil kwenye mashindano ya mialiko yake kisha kurejea mwaka 2016 alipokwenya Ufaransa kushiriki mashindano ya Marathon ya International La Route du Louvre (Lens-France) ambapo alimaliza wa kwanza akitumia saa 2:45:00
Shirika la kimataifa la kupambana na matumizi ya dawa za kuongeza misuli nguvu kwa wanamichezo (WADA) limekuwa likiendelea na juhudi za kufuatilia kuhusu visa vya wanamichezo mbalimbali ulimwenguni.
Uchunguzi wa Wada umepata kuwa dawa zilizopigwa marufuku ambazo hutumiwa mara kwa mara ni nandrolone na zile za kusisimua damu EPO.
Kinachotakiwa kufanyika ili vita hivi viwe na matokeo chanya katika michezo ni vema TOC na vyama vya michezo nchini kufanya uchunguzi wa afya za wachezaji mara kwa mara pia kabla na baada ya kufika kwenye mashindano ili kuondoa udanganyifu.
Elimu ianze kutolewa mapema kwa wachezaji na jamii ya watanzania kwa ujumla kuhusu dawa hizi za kusisimua misuli ili kwenda pamoja na Wada ambao wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha michezo inasalia kwenye msisimko unaotakiwa.
Mashindano kama Shimmuta na mengine ni mfano mzuri wa kutoa hamasa na kuonyesha njia katika vita hivi kwa udanganyifu unapojitokeza inakuwa ngumu kudhibiti matukio mengine ya rushwa katika michezo hali ambayo itakuwa kikwazo cha maendeleo ya michezo nchini.
Asante Shigella kwa kulikumbusha taifa na wanamichezo kuhusu matumizi ya dawa hizo, kwani vita hivi ni kwa ajili ustawi wa michezo nchini na dunia kwa ujumla.
caraOul_he Marquita Wright Download
ReplyDeleteacsmorounjet
OconbaWrioya_1987 John Jonas Luxion Keyshot Pro 11.2.1.5
ReplyDeleteWinRar
Microsoft Powerpoint 2021
Native Instruments Maschine 2 v2.15.2
neyvolnasa