Thursday, November 19, 2020

Tume ya Ushindani yafukua madudu Simba SC

 

Kikosi cha Simba msimu wa 2020/2021

Mnamo Novemba 18, 2020 Tume ya Ushindani (FCC) ilitoa taarifa yake kwa umma kuhusu uchunguzi juu ya mchakato  wa kubadili mfumo wa uendeshaji {transformation) wa klabu ya Simba kutoka wanachama kwenda kwenye umiliki wa hisa chini ya kampuni.

Pamoja na mambo mengine FCC ilisema kuwa ucheleweshwaji wa mchakato (transformation) wa kubadili mfumo wa uendeshaji wa Klabu ya Simba unatokana na mwitikio hafifu wa kampuni ya Simba Sports Club Company Limited wa kuwasilisha taarifa kamilifu na kwa wakati mbele ya Turne katika kufanikisha uchunguzi tajwa hapo juu.

Pia ilisisitiza kuwa haihusiki na ucheleweshwaji wa mchakato kama ilivyoetezwa na viongozi wa Timu ya Simba hapo juu bali inatekeleza wajibu wake kwa mujibu wa sheria na kwamba hadi ilipofika Novemba 18 mwaka huu hakukuwa na taarifa zozote kutoka katika klabu ya Simba.

FCC iliongeza kuwa sakata hilo imetekeleza kwa mujibu wa Kanuni ya 10 (9) ya Kanuni za Ushindani za Mwaka 2018.

Tume hiyo iliweka bayana namna mchakato huo unavyocheleweshwa na Wana Simba wenyewe kuwa, mnamo Aprili 24, 2019, Turne ilipokea ombi kutoka kwa Simba Sports Club Company Limited la kupatiwa mwongozo wa kisheria chini ya Sheria ya Ushindani kuhusu namna ya kushughulikia mchakato wa  rnabadiliko  (transformation)  ya  Klabu ya Simba unaohusisha karnpuni za Simba Sports Club Holding Company Limited, Mo Simba Company Limited, Simba Sports Club Company Limited na Klabu ya Simba (wadaawa );

Kufuatia ombi tajwa hapo juu , Tume ilifanya vikao viwili baina yake na Simba Sports Club Company Limited hadi Julai 24, 2020 ambapo wadaawa walioonekana kuelewa  mwongozo wa kisheria na kuahidi kuutekeleza  kama walivyoelekezwa na Turne. Baada ya ukimya wa muda mrefu wa wadaawa, mnarno Oktoba 4, 2019, Tume iliutoa mwongozo wake kama ilivyoombwa na wadaawa kwa maandishi. Wadaawa walitegemewa kwa mujibu wa sheria, wangejitathmini wenyewe (self-assessment) na kuleta maornbi husika kwa Turne kwa mujibu wa maelekezo ya kisheria yaliyorno kwenye mwongozo wa Turne;

FCC katika ufuatiliaji wake wa kila siku, Turne ilibaini viashiria kuwa Simba Sports Club (Klabu ya Simba) inaongozwa  na Simba Sports  Club Company Limited chini ya uenyekiti wa Mohamed Dewji (Mo Dewji) kabla ya wadaawa  hawajawasilisha maombi yao ya muungano (merger application) mbele ya Turne. Kitendo hiki, kwa mujibu wa mwenendo wa uchunguzi wa masuala ya ushindani ni kiashiria cha uvunjifu wa Kifungu cha 11 (2) cha Sheria ya Ushindani. Hivyo, mnamo Januari 23, 2020, Tumee ilianzisha uchunguzi (investigation) juu ya jambo hili kwa mujlbu  wa Sheria ya Ushindani;

Wakati uchunguzi unaendelea, mnamo Julai 23, 2020, FCC ilipokea maombi ya muungano wa makampuni (merger application) kutoka kwa wadaawa, wakiijulisha Tume nia yao ya kuichukua Klabu ya Simba na kuiendesha kama kampuni chini ya kampuni mpya waliyoianzisha ya Simba Sports Club Company Limited;

Tume iliyafanyia uchambuzi wa awali maombi hayo na mnamo Julai 30, 2020, FCC iliwajulisha wadaawa kwamba taarifa walizoziwasilisha mbele ya Tume hazikukidhi matakwa ya Sheria ya Ushindani  na hivyo kuwataka wawasilishe taarifa husika iii mchakato wa uchambuzi uendelee;

Mnamo Oktoba 13, 2020, Tume ilisitisha kwa muda mchakato wa uchambuzi wa maombi ya muungano wa kampuni ( merger application) na kuwajulisha wadaawa. Madhumuni ya kusitisha huko ni kupata taarifa na ufafanuzi zaidi toka kwa wadaawa na wadau wengine. Kwa mfano, taarifa zilizoombwa na Tume kutoka kwa uongozi wa Klabu ya Simba ni pamoja na (a) ufafanuzi kuhusu uteuzi wa Mtendaji Mkuu (Chief Executive Officer) wa Kiabu ya Simba kabla ya uwekezaji kufanyika; (b) kiasi halisi ambacho mwekezaji, Mohamed Dewji anatakiwa kuwekeza iii kuondokana na mkanganyiko ulioko kati ya kiasi kilichotajwa kwenye Mkataba  wa Makubaliano (Memorandum of Understanding) na kile  kinachotajwa  kwenye  vyombo  mbalimbali vya  habari;

FCC INAFANYAJE KAZI ZAKE?

Tume ya ushindani (FCC) ni Taasisi inayosaidia Soko yenye dhamana ya kuhakikisha kuwapo kwa kiwango cha uadilifu miongoni mwa washindani katika masoko yote yanayohusika kwa mujibu wa mamlaka ya FCA. Kwa nia hiyo hiyo, Tume imepewa dhamana ya kazi ya kupambana na bidhaa bandia kwenye masoko ya Tanzania kwa kuhimiza Sheria ya Alama za Kubainisha Bidhaa za biashara ya mwaka 1963 (MMA). FCC hufuata wakati wa kutekelezaji wa mamlaka yake chini ya Sheria ya Ushindani ya mwaka 2003, (Cap.285), ambayo ni kuchunguza makosa na mienendo mbalimbali ya wafanyabiashara inanayokiuka Sheria ya Ushindani.

FCC itatumia mamlaka yake, ama kutokana na malalamiko ya mlalamikaji huru (kwa mfano mshindani katika biashara, Mlaji au chama cha walaji, mtu mwingine yeyote, au kikundi cha watu, kuhusu madai ya ukiukwajia wa Sheria ya Ushindani, au kutokana na matakwa binafsi ya Tume (suo moto) mara inapobaini uwepo wa tatizo la kiushindani katika soko au uvunjifu wa dhahiri wa sheria ya ushindani.

Mbali na uwezo wa ujumla ambao Tume imekabidhiwa kisheria kuchunguza masuala ya ushindani katika uchumi wa Tanzania, kwa mujibu wa kifungu cha 65 (2) ya Sheria ya Ushindani, FCC ina mamlaka maalum ya: Kuitisha nyaraka au taarifa mahususi zinazohusu kampuni inayotuhumiwa kukiuka sheria ya ushindani; kuingia katika majengo kwa kibali maalum (warrant) kwa lengo la kutekeleza sheria ya ushindani, kuingia na kupekua kwa kibali maalum, nyumba, majengo au maeneo mengineyo, na kumwita mtu yeyote kwa minajili ya kutoa ushahidi kwa mbele ya Tume.

Mnamo Septemba 2020, Msemaji wa Klabu ya Simba Haji Manara kwenye mitandao  ya kijamii pamoja na gazeti la Mwanaspoti la Alhamisi tarehe 24 Septemba 2020 lenye kichwa cha Habari "Manara: Nitamshangaa Mo Dewji asipoweka pesa". Taarifa hizo zilisema, pamoja na mambo mengine, kwamba FCC inachelewesha mchakato wa uwekezaji ndani ya Timu ya Simba (transformation)

Makala haya yametayarishwa na Jabir Johnson, mwandishi wa habari na mtangazaji nchini Tanzania Novemba 19, 2020.

0 Comments:

Post a Comment