Tuesday, January 24, 2023

UVCCM Moshi Mjini yapanda miche 3,000

 

UVCCM Moshi Mjini wakiwa na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwenge katika zoezi la upandaji wa miti kuadhimisha miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi.

Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Wilaya ya Moshi Mjini  umewataka Vijana wa Jumuiya hiyo kusimamia misingi ya jumuiya hiyo kwani ndiyo nguzo kuu ya chama inayozalisha viongozi mbalimbali wa chama na Serikali. 

Akizungumza katika zoezi la upandaji miti ya matunda katika shule ya Msingi Mwenge iliyopo kata ya Kiusa Januari 24,2022 Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Sadath Sudi Ndibalema alisema UVCCM ni nguzo kuu inayopaswa kuzingatiwa katika mustakabali wa taifa hivyo vijana walioko ndani ya chama kuhakikisha kwamba wanaendelea kusimamia misingi hiyo.

Chama cha Mapinduzi kuliundwa Februari 5,1977 baada ya kuunganishwa kwa vyama vya Tanganyika African National Union (TANU) cha iliyokuwa Tanganyika, na Afro-Shiraz cha Zanzibar.

Azma ya zoezi la uoteshaji wa miche ya miti katika shule hiyo, Ndibalema alisema lengo ni kuweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi sambamba na wanafunzi kupata lishe ya wanafunzi hao.

Mkuu wa shule ya Msingi Mwenge Hellena John alisema, shule hiyo ilikuwa na uhitaji mkubwa wa miche ya miti ya matunda na kuipongeza Jumuiya ya Umoja wa Vijana kwakuweza kuwapatia miche hiyo.

Mkuu wa Shule ya Msingi Mwenge Bi. Hellen John

Katibu wa UVCCM Wilaya ya Moshi mjini Arafati Mbiruka alisema Jumuiya hiyo ya Vijana  wameamua kuotesha miti ya matunda katika shule ya msingi Mwenge ili kuboresha mazingira ya shule hiyo sanjari na wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo kupata matunda lishe ili kuboresha afya zao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kiusa, Khalid Shekoloa aliishukuru Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa UVCCM Manispaa ya Moshi kwa kuwezakupanda miti ya matunda katika shule hiyo kwani itakwenda kusaidia utatuzi wa changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi sanjari na kuwaomba wanafunzi wa shule hiyo kuendelea kuitunza 

Aidha Shekoloa amewataka kupanda miti kwa wingi itakayosaidia utunzaji wa mazingira ili kwenda sambamba na mpango wa Serikali wa upandaji miti ili kuzuia athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Sadath Ndibalema, mwenyekiti wa UVCCM Moshi Mjini

Naye Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Moshi Mjini kutoka kundi la Vijana  Ashiraf Baraka Malya, walisema bado kuna changamoto ya uelewa kwa jamii juu ya upandaji wa miti na utunzaji wa mazingira.

“Upandaji miti ulioendeshwa na UVCCM Wilaya ya Moshi Mjini katika kuadhimisha miaka 46 ya kuzaliwa kwa CCM, itakwenda kuboresha mazingira ya shule huku akitoa wito kwa wanafunzi hao kuitunzana kuilinda ili kuwana mazingira yaliyo salama,”alisema Malya.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwenge mjini Moshi wakiwa na miche ya miti

Zoezi la upandaji wa miti ni ikiwa ni maandalizi ya kuadhimisha miaka 46 ya kuzaliwa kwa CCM. Chama cha Mapinduzi kuliundwa Februari 5,1977 baada ya kuunganishwa kwa vyama vya Tanganyika African National Union (TANU) cha iliyokuwa Tanganyika, na Afro-Shiraz cha Zanzibar.

Stempu za Posta zikionyesha mambo mbalimbali ambayo Chama cha Mapinduzi iliyoyafanya ndani ya miaka 10 baada ya kuanzishwa kwake,ikiwamo Azimio la Arusha kutoka awamu ya kwanza na mwanzoni mwa awamu ya pili enzi za utawala wa Mwalimu Juliuys Kambarage Nyerere na Ali Hassan Mwinyi.




0 Comments:

Post a Comment