Chifu Marealle (kushoto) akipokea zawadi ya kifimbo cha uchifu kutoka kwa Chifu Omary Mwariko 'Mhelamwana' walipokutana Marangu, Moshi mnamo mwezi Agosti 2022. (Picha: Maktaba) |
Mwenyekiti wa Umoja wa Machifu Tanzania (UMT) anayemaliza muda wake Chifu Frank Marealle ameonya kuhusu matumizi ya fedha kwa mwenyekiti mpya atakayeongoza umoja huo.
Akizungumza
katika hafla ya kukabidhi uenyekiti wa UMT aliodumu nao kwa takribani miaka 13,
huko Marangu, Moshi mkoani Kilimanjaro; Chifu Marealle amesema matumizi ya
fedha yamekuwa changamoto kubwa kwa taasisi nyingi nchini.
“Fedha
zitumike kwa lengo lililokusudiwa la kuendeleza shughuli za umoja, msitumie
fedha hovyo, fedha kidogo inayopatikana itumike kuendeleza umoja huo,” amesema
Chifu Marealle
Aidha
Chifu Marealle amesema suala la matumizi ya fedha linapaswa kutiliwa mkazo ili kuepusha
mgongano wa kimaslahi unaoweza kufanywa endapo hakutafnyika uchaguzi wa
viongozi sahihi kuongoza UMT.
“Changamoto;
wako baadhi ya wanachama walitaka kuuvuruga umoja huo lakini aliweza kusimama
imara na kuweza kufanikiwa kuwaunganisha na kuwa wamoja,” ameongeza Chifu
Marealle.
Chifu
Marealle amesema kwa miaka yote alioongoza umoja huo amejifunza mambo mengi
kutoka kwa machifu huku akisisitiza kuwa ameachia kiti hicho kwa hiari ili Kujenga
tabia ya kuachiana madaraka.
“Watu
tujenge umoja wa kukabidhi madaraka tusiwe ving'ang'anizi na huu utaratibu
niliamua kuujenga ili pasitokee mtu yeyote kutaka kuvuruga,” amesisitiza.
Katika
miaka 13 yake ya uongozi ameweza kuwaunganisha, mshikamano, amehamasisha kila
chifu kuweza kusimamia maadili, elimu afya kusimamia Mila na desturi na
mazingira.
Chifu Marealle akisoma hotuba yake wakati wa kukabidhi madaraka kwa hiari mnamo Oktoba 8, 2022 |
0 Comments:
Post a Comment