Joto la maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) yanayotarajiwa kufanyika Aprili 30, 2024 linazidi kupanda mjini Moshi ambapo wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro wametakiwa kutambua kuwa maandamano hayo sio kelele za wahuni bali ni ya Amani kwa Ustawi wa Tanzania
Akizungumza na vyombo vya habari mjini Moshi Leo Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini Amani Golugwa amesema watanzania wanaaminishwa kuwa maandamano hayo ni ya wahuni na wapiga kelele na kwamba huko ni kuwakosea watanzania wanaokabiliwa na hali ngumu za Maisha.
"Kama unanunua sukari kilo shilingi 1000 usiandamane kaa nyumbani, maandamano haya hayatakoma, tutaandamana pia katika ngazi za wilaya mpaka serikali ielewe," amesema Golugwa.
Golugwa amesema Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro limetoa ushirikiano mzuri ambapo njia zilizoruhusiwa ni tatu na mkutano wa hadhara utafanyika katika Viwanja vya Mashujaa ambako viongozi wa Chadema watakuwepo.
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, ataongozana na Boniphace Mwabukusi, Peter Msigwa, Godbless Lema, Raymond Mboya, John Heche na Japhary Michael pamoja na viongozi wengine wa ngazi za Kijiji, Kata na. Wilaya.
0 Comments:
Post a Comment