Ukweli na Kuheshimiana ni kiini ujenzi wa jamii zetu

Ulimwenguni kwa sasa kumejaa habari potofu na upotoshaji, ni muhimu kuhakikisha kwamba ukweli na kuheshimiana vinakuwa kiini kwa ujenzi wa jamii zetu.

Mapambano dhidi ya Habari za Uongo hayapaswi kukoma

Habari za uongo, habari za uongo zinazosambazwa kwa lengo la kumdhuru mtu au jambo fulani, huifanya jamii kuwa na sintofahamu. Zinaweza kutumika kwa madhumuni ya kiitikadi, kisiasa au hata uhalifu, kama vile ulaghai mtandaoni unaolenga kuiba data ya kibinafsi.

Utandawazi na Athari zake katika Uandishi wa Habari

Katika jamii yetu ya kisasa, ambapo habari ziko kila mahali na zinaweza kupatikana kwa kila mtu, mara nyingi ni ngumu kutofautisha kati ya vyanzo vya kuaminika na habari bandia.

Uandishi wa Habari nguzo msingi mkuu kwa ujenzi wa jamii inayojitambua

JAIZMELA blog ni miongoni mwa vyanzo vya habari, zilizochakatwa kwa kuzingatia miiko ya uandishi wa habari.

Mila na Desturi ni nguzo muhimu

Mila na desturi ni nguzo muhimu sana katika utamaduni wa jamii yoyote ile; mila ni sawa na sheria zisizoandikwa. Mila ni taratibu za maisha na mwenendo zinazofuatwa na jamii fulani katika utendaji kulingana na historia na utamaduni wao. Mila zinatambulisha maadili ya jamii husika, huelezea namna jamii inavyoendesha mambo yake.

Sunday, February 26, 2023

Nestory Njatile Mwangoka na Kili Marathon 2023

Mzee Nestory Mwangoka akiwa mjini Moshi baada ya kushiriki mbio za Kili Marathon 2023 kilometa 21 akitumia dakika 100 kumaliza. (Picha zote na Kija Elias)

Meneja wa Shirika la Posta Mkoa wa Kilimanjaro Deodatus Ako akimpongeza Mzee Mwangoka baada ya kufika ofisini hapo alipoanzia kazi yake. 

 

Safari ya Maisha ni ya pekee na Kila mtu hupitia mambo kwa majira yake unaweza kusema  “Kila Mtu na Wakati wake”.

Unapojua safari ya maisha ni ya upekee basi unajifunza kufurahia hatua zako kila inapoitwa leo.

Utafurahia mafanikio unayofanikiwa, utafurahia unavyopitia changamoto na magumu maana unajua ni sehemu ya hadithi ya maisha yako.

Hivyo ndivyo Mzee Nestory Njatile Mwangoka alivyofurahia kukimbia kilometa 21 za Kili Marathon 2023 iliyofanyika mjini Moshi mnamo Februari 26, 2023.

Mwangoka (64) alikuwa imara katika mbio hizo akikimbia kwa dakika 100 sawa na saa moja na dakika 40.

Kinachovutia kwa mzee huyo ni pale anapokusimulia maisha ya mjii wa Moshi ulivyokuwa sehemu ya mafanikio ya maisha yake.

Mzee Mwangoka anasema, “Nimekuja Kilimanjaro kushiriki mbio za marathon kwasababu mwaka 1985 nilikuja hapa Kilimanjaro  nikiwa kijana mdogo na kuanza kazi hapa katika Shirika la Posta.”

Mwangoka anakumbusha kuwa wakati akitua katika viunga vya Moshi hakuwa kufikiri kama siku moja kutafanyika mbio za Kimataifa na kuvuta mamia ya watu kote ulimwenguni kama ilivyo sasa.

Mfanyakazi huyo wa zamani wa Shirika la Posta ameweka rekodi yake binafsi kwa furaha tele kwa mara ya kwanza alipokimbia mbio hizo akitokea mjini Mbeya.

“Nimeonyesha kwamba wazee tunaweza, natoa wito kwa wafanyakazi kote nchini kushiriki mazoezi kusaidia kuweka miili yetu vizuri na kuondokana na maradhi,” anasema Mwangoka.

Mwangoka anaweka bayana kuwa mbio za mwaka huu ni za kwanza katika miaka 21 ya Kili Marathon, licha ya ushiriki wake wa mbio nyingine za kilometa 21 zinapofanyika nchini hususani mkoani kwake Mbeya.

“Shukrani zangu za dhati ni kwa Shirika la Posta Tanzania kwa kuniwezesha kushiriki mbio za mwaka huu ni mfano wa kuigwa kwa uongozi mzima kwa maendeleo ya taifa,” aliongeza Mwangoka.  

Licha ya ujio wake katika Kili Marathon 2023, Mwangoka hakusita kufika katika Ofisi za Shirika la Posta mkoa wa Kilimanjaro ambako alikutana na Meneja wa Posta mkoani humo kwa sasa Ndugu Deodatus Silaa Ako.

Ako aliongeza, “ Ari na Hamasa alio nayo mzee Mwangoka ni somo kwetu, hata mwaka huu tumeshiriki mbio hizo hii imetokana na mwongozo ambao Shirika letu la Posta limekuwa na mwongozo kwa wafanyakazi wake kufanya mazoezi kila Ijumaa baada ya masaa ya kazi.”

Meneja huyo alisisitiza kuwa vijana wanapaswa kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi pamoja kuimaraisha umoja wa kitaifa na maeneo ya kazi.”

Mataifa 55 yameshiriki mbio hizo mwaka huu katika kilometa 5, 21k na 42k, huku Waziri wa Maliasili na Utalii Mohammmed Mchengerwa akiwa mgeni wa heshima.







Tuesday, February 21, 2023

Afisa Tarafa Moshi Magharibi kikwazo upanuzi wa barabara ya Mwembeni

Miti inayozuia utoaji wa kibali cha upanuzi wa barabaraya Longuo B,Moshi 

IMEELEZWA Afisa Tarafa Moshi Magharibi, Moshi mkoani hapa ni kikwazo cha upanuzi wa barabara baada ya kudaiwa kuomba rushwa ya miti ili kitolewe kibali cha ukataji wa miti hiyo kupisha ujenzi wa barabara.

Hayo yanajiri wakati wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Moshi kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya chama hicho huku jina laAfisa Tarafahuyo anayefahamika kwa jina la Senzia Masafiri Lushino likitajwa kuwa kikwazo cha ujenzi huo.

Akichangia hoja ya upanuzi wa barabara ya Longuo B,Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro Jonathan Mabhiya alisema kumekuwa na vikwazo kutoka wilayani kuhusu utekelezaji wa upanuzi wa barabara hiyo.

“Niliwahi kutembelea Kata ya Longuo B kuna ufunguzi wa barabara mpya, wananchi wako tayari kutoa baadhi ya miti yao ikatwe barabara iweze kufunguliwa ili Tarura waanzematengenezo na Tarura wako tayari, lakini tatizo ni kikwazo kikubwa ni viongozi kutoka ofisi ya Mkuu wa Wilaya,” alisema Mabhiya.

Aidha Mabhiya aliweka bayana kuwa muhtasari wa upanuzi wa barabara hiyo umefungiwa katika makabati ya wilayani tangu mwaka 2017 bila utekelezaji wowote hali inayotia ugumu kutekeleza mipango ya chama iliyojiwekea ifikapo 2025.

“Waliandika mhutasari uko ofisini kwako toka mwaka 2017 lakini tatizo ni kibali ambacho kimekuwa kikwazo kupatikana,” aliongeza Mabhiya.

Hata hivyo Mabhiya aliiomba ofisi ya mkuu wa Wilaya kushughulikia changamoto hiyo hasa ikizingatiwa Afisa Tarafa wa Longuo B amekuwa akinyoshewa kidole cha lawama kwa kutaka rushwa ya miti ili achane mbao kwa ajili ya kupanulia nyumba yake.

“Tunaiomba ofisi ya mkuu wa wilaya suala hili la barabara ya Longuo ambayo taarifa ilisha letwaofisini kwako ulifanyie kazi kibali cha uvunaji miti kiweze kupatikana ili barabara hiyo iweze kuanza kutengenezwa na wananchi kutoa eneo lao huko mkoa wa Kilimanjaro hata hatua moja tu barabara iweze kutanuliwa ni shida sasa hawa waliokubali kutoa eneo lao kwa ajili ya kipisha barabara tena bila kuomba fidia,” alisisitiza.

Kwa upande wao mkazi wa Longuo B aliyejitambulisha kwa jina la Ephraim Shao alisema, “Mimi nilikuwa shahidi namba moja katika kufuatilia kupata kibali cha kuvuna miti ili kupisha ujenzi wa barabara, tunahitaji maendeleo  ili kupisha barabara.”

Pia Damas Shao alisema kuna wakati Afisa Tarafa huyoalikuja na kumtaka ampe miti baadhi ili aweze kuto kibali cha uvunaji wa miti kwa ajili ya upanuzi wa barabara

"Mimi ndio mmiliki wa eneo  hili na kukawa na masharti ya kutoa rushwa ya miti kumi bure ana ujenzi wa nyumba yake kutoka kwa afisa tarafa ili aweze kunipa kibali cha kuvuna miti yangu na mimi nilishaapa siwezi nikatoa rushwa hadi sasa sijatoa chochote," alisema Mzee Shao.

Diwani Benedict Mwashamba alisema“wakati nikiingia kama Diwani wa Longuo B Tulikuwa na malengo ya kupata huduma bora na changamoto kubwa eneo letu lilikuwa halina maeneo kabisa ilikuwa barabara tulikaa na wananchi ili kujadili na tukaandika muhtasari na kuipeleka; watendaji wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya hasa huyu Afisa Tarafa ambaye alianza kutengeneza malalamiko,wananchi hakuna aliyepeleka malalamiko,”

Mwashamba aliongeza kwa sasa kinachotakiwa ni kutolewa kwa kibali cha uvunaji wa miti ili upanuzi wa barabara ufanyike kwa maendeleo ya wananchi wenyewe.

Mkuu wa Wilaya wa Moshi Kishare Makori alisema ameshangazwa na watendaji wa ofisi yake kushindwa kutoa kibali huku wananchi wakiwa tayari kutoa maeneo yao kwa ajili ya maendeleo yao, na aliagiza kuletewa nyaraka zote (muhtasari) wa suala hilolaupanuzi wa barabara ili aweze kutoa kibali hicho.





Mzee Damas Shao anayedai kuomba rushwa ya miti na Afisa Tarafa wa Moshi Mgharibi ili kupewa kibali cha uvunaji miti kupisha ujenzi wa barabara ya Mwembeni mtaa wa Kitandu, Longuo B


Friday, February 17, 2023

Wakazi wa Njiapanda-Moshi waepukana na adha ya maji, MUWSA yakamilisha

 

Mbunge anayewawakilisha Wanawake Mkoa wa Kilimanjaro Esther Maleko  akinywa maji safi na salama baada ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa  Mazingira (MUWSA) kukamilisha mradi huo kwa wakazi wa Njiapanda, Moshi Vijijini ambao utawahudumia takribani wakazi 14,000.


Kukamilika kwa mradi wa maji kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa  Mazingira (MUWSA), kunawafanya taribani watu 14,000 wa kata ya Njia Panda, wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro kuepukana na adha ya kufuata maji umbali mrefu.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa  Mazingira (MUWSA). (MUWSA) Mhandisi Kija Limbe katika taarifa yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkurugenzi wa Usambazaji wa Maji safi na Usafi wa Mazingira wa taasisi hiyo Mhandisi Innocent Lugodisha, kwa uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Moshi Vijijini.


"Kutokana na mafanikio iliyoyapata katika kutekeleza shghuli zake Moshi Mjini, MUWSA iliongezewa eneo la kutoa huduma ambapo ilijumuisha mji mdogo wa Himo na Njia Panda pamoja na kata zingine 12 katika halmashauri ya wilaya ya Moshi", alisema.

Alisema "Hadi sasa Serikali imesha elekeza  kiasi cha shilingi bilioni 5.3 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimmbali ya kuboresha huduma ya maji katika maeneo haya mapya, ambapo zaidi ya shilingi bnilioni 2.3 zimetumika kutekeleza mradi wa maji wa kata ya Njia Panda", alisema Mhandisi Lugodisha.

Aliendelea kusema kuwa mradi  huo unatarajiwa kuhudumia takribani watu 14,000 na kwamba una uwezo wa kuzalisha jumla ya lita za ujazo  milioni 2.5 kwa siku, ambapo alisema tayari umeshakamilika kwa asilimia 100.

"Kazi zilizofanyika wakati wa kutekeleza mradi huu ni pamoja na ujenzi wa chemba ya kukusanyia maji, ujenzi wa ofisi pamoja na control panel room pamoja na ujenzi wa storage tank lenye ukubwa wa mita za ujazo 100 katika eneo la Mabungo", alisema.

Alisema kazi nyingine ilikuwa ni ile ya ununuzi wa bomba, uchimbaji wa mtaro pamoja na ulazi wa bomba wenye urefu wa kilomita 13.6 kuanzia eneo la Miwaleni hadi kwenye matangi yaliyoko eneo la Kilema Pofo.

"Kazi zingine zilikuwa ni zile za ujenzi wa njia kuu ya umeme pamoja na kuweka transforma eneo la Miwaleni na Mabungo, kununua na kufunga pumps za kusukuma maji eneo la Miwaleni pamoja na Mabungo Buster Station pamoja na ujenzi wa vyoo eneo la mradi ya Miwaleni na Mabungo", alisema.

Akizungumza wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa  ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Moshi Vijijini  kukagua miradi ya maendeleo ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya CCM,  Mbunge wa Mkoa wa Kilimanjaro anayewakilisha kundi la Wanawake, Esther Maleko, ameipongeza Serikali kwa kutoa fedha hizo jambo ambalo alisema litawapa wananchi wa eneo hilo hususan wanawake muda wa kufanya shughuli nyingine badala ya kutumia muda mwingi kufuatillia maji mbali.

Aidha aliupongeza uongozi wa MUWSA kwa kuutekeleza mradi huo kwa kwa wakati na kwa viwango vilivyowekwa ambapo alisema utekelezaji huo unatarajiwa kuwahudumia wananchi kwa muda mrefu ujao.

Aidha Diwani wa Kata ya Njia Panda Loveness Mfinanga alisema kuwa kukamilika kwa mradi huo wa  maji Miwaleni -Njia Panda, umewezesha kwa kiasi kikubwa kuondoa changamoto ya maji iliyokuwepo katika kata hiyo kwa kipindi kirefu.

“Naishuikuru Serikali kupitia  Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa  Mazingira (MUWSA) kwa jitihada za kutekeleza mradi huu wa maji na kuwezesha wananchi kupata huduma ya maji safi na salama  kwa wakati,”alisema Loveness.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Moshi Cyril Mushi alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha utekelezaji wa mradi huo wa Maji Miwaleni Njia Panda, kuondoa changamoto kubwa ya  maji  kwa wananchi waKata ya Njia Panda.

“Mradi huu  umeondoa changamoto kubwa ya ukosefu wa maji kwa wananchi wa eneo hili,  niwaombe wakazi wote  eneo hili kuwa waangalifu wa miundombinu ya maji kwa kuitunza na kuisimamia ili huduma  hii ya maji iendelee kupatikana muda wote,” alisema Mushi.

Naye  Mkuu wa wilaya ya Moshi Kisare  Makori, alisema kuwa kukamilika kwa mradi huo ni ukombozi kwa wananchi wa eneo la Njia Panda ambapo alielezea matumaini yake ya kuwa miradi mingine ya maji inayoendelea kutekelezwa itakamilika kwa wakati ili wananchi waendelee kunufaika na miradi inayotekelezwa na Serikali.

Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 inalenga kufikisha kiwango cha upatikanaji wa maji kufikia asilimia 90 ya maeneo ya vijijini ya idadi ya watu watakaopata maji safi na salama ifikapo mwaka 2025 sambamba na kuimarisha uwezo wa kusimamia rasilimali maji.


 






 

Thursday, February 16, 2023

Mbunge Esther Maleko achangia mil. 1.6 ununuzi wa madawati Ashira Secondary

Mbunge wa Mkoa wa Kilimanjaro anayewakilisha Wanawake, Esther Maleko, akizungumza jambo wakati wa ukaguzi wa wa miradi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Moshi Vijijini inayotekelezwa na serikali ya Awamu ya Sita.

Katika kuunga mkono juhudi za Serikali  katika kuboresha sekta ya elimu nchini Mbunge wa Mkoa wa Kilimanjaro anayewakilisha Wanawake, Esther Maleko, amechangia kiasi cha shilingi milioni 1.6 kwa ajili ya ununuzi wa madawati  kwenye shule ya Sekondari ya Wasichana Ashira iliyoko wilaya ya Moshi mkoani humo. 

Msaada huo wa madawati ni sehemu ya jitihada za Mbunge huyo katika kusaidia jamii ili kuwawezesha wanafunzi hao kusoma kwa utulivu. 

Katika ziara yake aliyoifanya Februari 16, 2023 Moshi Vijijini Mbunge Esther Maleko alisema ameamua kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan  kwa kuchangia kiasi cha Shilingi  milioni 1.6 kwa ajili ya kununua madawati ili watoto waweze kusoma vizuri. 

“Katika ziara yetu ya kukagua Ilani ya CCM  tumekagua miradi kadhaa ukiwemo mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa manne, mabweni mawili na bwalo moja kwenye shule ya Sekondari ya Wasichana Ashira, tumeona kazi kubwa iliyofanyika Rais Samia Suluhu Hassan  ambaye ametoa kiasi cha Sh miloni 400  na mimi katika kumuunga mkono nimeguswa kuchangia kiasi cha shilingi milioni 1.6 kwa ajili ya ununuzi wa madawati katika shule hii,” alisema. 

“Elimu yetu ya sasa ni bure ili kuwawezesha watoto wote kusoma lakini sera hii imekuja na changamoto zake ambazo jamiii ni lazima tushirikiane kuzipatia ufumbuzi, kuna uhaba wa madawati, nyumba za walimu na vitendea kazi vingine,”amesema.  

Akizungumzia changamoto ya uzio katika shule hiyo Mbunge Esther Maleko amesema atakwenda kushirikiana na uongozi wa shule hiyo ili kuweza kutatua changamoto hiyo ili waweze kumalizia ujenzi wa uzio huo. 

Kuhusu suala la mikopo Mbunge Maleko amewataka kuchangamkia fursa ya mikopo inayotolewa na serikali  kwa makundi ya Vijana, Wanawake na watu wenye ulemavu  

Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Moshi  Cyril Mushi alimpongeza Mbunge Esther Maleko  kwa kutekeleza Ilani ya CCM kwa vitendo na kuwa  Mbunge anayewajibika kikamilifu kwa jamii yake. 

Nimpongeze Mbunge Maleko kwa kazi kubwa anayoifanya kupigania maendeleo kwenye wilaya ya Moshi na mkoa wa Kilimanjaro kwa ujumla, ni matarajio yangu mchango wako wa madawati haya yatakwenda saidia kuboresha mazingira ya kujifunzia  kwa wanafunzi  na  kuchochea ongezeko la ufaulu.

Mkuu wa Wilaya ya Moshi Kisare Makori,  amempongeza Mbunge Maleko kwa msaada huo na kumhakikishia kuwa madawati hayo yatatunzwa vizuri ili yaweze kutumika kwa  muda mrefu. 

“Utaendelea kukumbukwa daima kwa msaada huu ambao una manufaa makubwa kwa watoto wetu,”amesema DC Makori.

 












 

Wednesday, February 15, 2023

Bilionea Najafi aitaka Tottenham kwa Tril. 8.75

 

Bilionea mwenye asili ya Kimarekani raia wa Iran Jahm Najafi ameripotiwa kuitaka klabu ya Tottenham kwa kitita cha pauni bil. 3.1 sawa na Trilioni 8.8 za Tanzania

Gazeti la Financial Times limeripoti kuwa Najafi ambaye ni Mwenyekiti wa MSP Sports Capital yupo mbioni kuweka kitita hicho kikubwa cha fedha.

Aidha inaelezwa kuwa wapo mbioni kumwona mmiliki wa klabu hiyo JoeLewis na mwenyekiti wake Daniel Levy katikamajuma machahce yajayo.

Najafi na MSP wana asilimia 70 ya kuweka kitita hichocha fedha  huku wengine wanaweza kuchangia asilimia 30 zilizobaki ambazo zinaweza kutolewa na mabilionea wengine kutoka ghuba na Abu Dhabi.

MAKTABA YA JAIZMELA: Zao la Miwa lilianzia wapi?

Mwandishi wa vitabu wa Ufaransa Charles de Brosses (1707-1777) analitaja kwa mara ya kwanza eneo la Kusini mwa Bahari ya Pasifiki kama Polynesia, ikiwa na maana ya eneo linaloundwa na visiwa 1,000.

De Brosses katika kitabu chake cha “Histoire des navigations aux terres australes, contenant ce que l'on sait des moeurs et des productions des contrées découvertes jusqu'à ce jour (1756)”, kinaweka bayana watu wa ukanda huo na utamaduni wao.  

Miongoni mwa visiwa ni New Zealand, Tonga, Samoa, Tuvalu, French Polynesia, Norfolk na Hawaii; eneo hilo lina historia kubwa ya Miwa/Sukari.

Unafahamu kuwa sukari ni miongoni mwa bidhaa za mwanzo kutajwa tangu kuwekwa kwa misingi ya dunia hii? Sasa kwa taarifa yako ni kwamba historia yake inaanza miaka 10,000 iliyopita katika ardhi ya Polynesia.

Unajua kuwa Miwa ni zao la kitropiki ambalo hustawi hadi kufikia kimo cha hatua 20, na kuvunwa ndani ya miezi 12?

Mwaka 8000 K.K, zao hilo lilionekana katika ardhi ya Polynesia, lilistawishwa kienyeji tu, sio kwa madhumuni ya kibiashara.

Familia za ukanda huo zilikuwa na utaratibu wa kustawisha kwa ajili ya matumizi ya ndani tu, mfumo ambao hadi miaka ya sasa  kwenye maeneo ya vijijini nchini Tanzania unaweza kuona miwa ikistawishwa pembezoni mwa nyumba.

Kutoka hapo tamaduni mbalimbalimbali ulimwenguni zilipoanza kufunguka na kuanza kutafuta malighafi zao ndipo zao hili lilipopata umaarufu.

Kwa mfano enzi za ustaraabu wa Warumi na Wayunani, walitumia miwa katika mfumo wa sukari kwa matibabu, hususani kwa watu waliokuwa na matatizo ya mmeng’enyo wa chakula na matatizo ya tumbo kwa ujumla. Pia walitumia kwa kutibu vidonda.

Ustaarabu wa Milima ya Himalaya kwa upande wa mashariki ikiwa na maana ya China, wenyewe mnamo mwaka 640 BK walianza kulima mashamba makubwa ya miwa wakitumia teknolojia waliyoipata kutoka Ustaarabu wa Magharibi mwa Milima ya Himalaya (India).

Miaka ile ya 1096-1099 kundi kubwa la wapiganaji waliokuwa wakirudi barani Ulaya walibeba zawadi ikiwamo miwa/sukari, ambapo watu wa Ulaya walikuwa wakiita Chumvi Tamu.

Mnamo mwaka 1390, suala la miwa/sukari lilipiga hatua nyingine kubwa kwa kuanza kuchuja miwa ili kupata juisi, yaani juisi ya miwa.

Katika visiwa vya Madeira huko Ureno kati ya mwaka 1455 na 1480  kwa mara ya kwanza barani Ulaya kulionekana mashamba makubwa ya miwa . Mwishoni mwa miaka hiyo, inaelezwa kuwa  meli 70 zilitia nanga katika kingo za kisiwa cha Madeira kwa  ajili ya biashara  ya miwa na sukari.

Kuitengeneza miwa hiyo kwa viwango vya juu na usambazaji kwingineko ilifanyika katika mji wa Antwerp nchini Ubelgiji.

Mnamo karne ya 15 kwa mara ya kwanza miwa ilionekana huko Amerika na ilianza kutua nchini Brazil ambako Wafanyabiashara wa Kireno walifika huko. Muwa wa kwanza ulipandwa nchini Marekani ikiwa  ni zawadi kutoka kwa Gavana wa Visiwa vya Canary kwa mpelelezi Christopher Columbus.

Mnamo mwaka 1813 mgunduzi Edward Charles Howard alipiga hatua kubwa katika uzalishaji wa miwa na sukari pale alipogundua njia ya kuichakata miwa kwa moto.

Maboresho yaliendelea katika maeneo  mbalimbali ikiwamo uvunaji ambapo mashine za uvunaji (16 whole-stalk harvesters) zilipotumika huko Louisiana mnamo mwaka 1938.

Matumizi ya mashine hizo yalikuja kutokana na ukosefu wa watu wakati na baada ya Vita vya Pili Dunia (1939-1945), ilipofika mwaka 1946 huko Louisiana mashine hizo zilifikia 422 na kufanya uvunaji wa miwa kufikia asilimia 63.

Kwa sasa zaidi ya nchi 80 zinalima miwa huko nchini Marekani majimbo ya Louisiana,Florida na Texas ndio maarufu kwa kilimo cha zao hilo.

Nchini Tanzania; mikoa ya Kagera, Morogoro na Kilimanjaro ndio maarufu kwa kilimo cha miwa ambapo makala haya yatajikita katika wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro kunakopatikana mashamba makubwa ya miwa ya TPC.

Kwa miongo kadhaa sasa maeneo ya karibu na mashamba hayo ya TPC unapowadia msimu wa uvunaji wa miwa ilikuwa ni  kero kubwa kutokana na moshi na majivu kuharibu mwonekano na hali ya hewa kutokana na uvunaji wa kutumia moto, ambao mashamba ya miwa yalikuwa yakichomwa na kusababisha uharibu wa mazingira na ikolojia yake.

Akizungumza na mwandishi wa makala haya, Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPC Jaffary Ali anasema uvunaji wa miwa duniani kote ni kwa kutumia wanadamu, muwa lazima uchomwe moto  kwa ajili ya kumpa fursa mvunaji kuingia kuondoa wanyama wakali na wadudu ambao wanaweza kumdhuru wakati wa uvunaji.

“Utaratibu huo  hutumika duniani kote, kutokana na mabadiliko ya mazingira na sheria za mazingira zinazohitajika kupunguza uchafuzi wa mazingira wavunaji wakulima wengi wameanza kutumia teknolojia ya kuvuna miwa bila ya kuichoma tukiwamo sisi,” anaongeza Jaffary Ali.

Monday, February 13, 2023

Maboresho yanatakiwa vivutio vya utalii Moshi DC

 

Madiwani wa Halmashauri ya Moshi katika picha ya pamoja kwenye Maporomoko ya Materuni 

Vivutio vya utalii vinavyopatikana Halmashauri ya wilaya ya Moshi mkoa wa Kilimanjro vimetakiwa kuboreshwa zaidi hususan kwenye miundombinu ya barabara za kuelekea kwenye vivutio hivyo, pamoja na kuwa na miundombinu ya vyoo na maeneo ya kutupia taka nguvu.

Ushauri huo umetolewa  hivi karibuni na madiwani wa  Halmashauri hiyo waliotembelea kivutio cha utalii  cha maporomoko ya maji Materuni kilichopo Kata ya Uru Mashariki, wilayani humo ikiwa ni sehemu ya ziara ya kuhamasisha utalii wa ndani.

Wakizungumzia kuhusu lengo la ziara hiyo  Diwani wa kata ya Old Moshi Mashariki Super Macha, Diwani  Kata ya Njia Panda Loveness  Mfinanga, na Diwani Kata ya Mwika Kaskazini Samuel shao, walisema ziara hiyo ya siku moja ilikuwa imejikita kuhamasisha utalii wa ndani  sanjari na kubaini vyanzo vipa vya mapato ya halmashauri hiyo.

Katika ziara hiyo Madiwani hao wameshauri mapato ya asilimia 40 yanapatikana katika eneo la maporomoko ya maji Materuni yarudi kuboresha miundo mbinu ya barabara vyoo pamoja na sehemu ya kutupa taka ngumu ili wageni wanaofika kutembelea eneo hilo waweze kuvutiwa na mandhari nzuri iliyopo.

Diwani wa Kata ya Uru Kusini Wilhard Kitali Diwani alisema upo umuhimu wa mkubwa wa halmashauri ya Moshi, kuhakikisha vivutio vyote vya  utalii vilivyopo wilayani humo vinatangazwa.

Kitali alisema  halmashauri ya Moshi ndio benki na kitovu cha utalii katika mkoa wa Kilimanjaro, kwani inavyo vyanzo vingi vya utalii ikiwemo soko la watumwa, mapango, mti uliotumika kumnyongea Mangi Meli, malango ya kupandia mlima Kilimanjaro, mahandaki na mti mrefu Afrika  kama vitatangazwa mapato ya halmashauri kwa upande wa utalii yataweza kuongezeka zaidi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Moris Makoi alisema ziara hiyo ilikuwa imelenga kuvitambua vivutio ili kuongeza mapato ya halmashauri sambamba na kuhamasisha Watanzania kujenga utamaduni wa kuvitembelea vivutio vinavyowazunguka kwenye maeneo yao.

Aidha Makoi alisema  halmashauri hiyo itaanzisha  program maalum ya mafunzo kwa vijana wanaojishughulisha na kuwatembeza wageni  (Waongoza watalii) ili waweze kuwaelezea vizuri historia ya wilaya ya Moshi na namna ilivyo na vivutio vingi vya utalii ili wageni wanapofika Kilimanjaro kabla ya kupanda mlima huo waweze kwanza kuvitembelea vivutio hivyo ikiwemo mti uliotumika kumnyongea Mangi mengi.

Awali Ofisa mtendaji wa Kijiji cha Uru Mashariki Robert Soka, aliwaeleza madiwani hao kuwa  maporomoko ya maji Materuni ni moja ya maporomoko ya maji yanayotoka katika mto Mware ambapo kimekuwa kivitio kibwa cha wageni kutoka nje kutembelea eneo hilo.

Alisema uwepo wa maporomoko hayo ya maji ukusanyaji wa mapato umeongezeka kutoka shilingi laki sita hadi laki nane kutokana na wageni wengi kutoka nje ya nchi kuja kutembelea kivutio hicho huku takribani ya wakazi wa kijiji hicho 2,000 wanajishughulisha na shughuli za kuwatembeza watalii hao.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Dk. Alex Kazura alisema katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha 2023-2024 halmashauri imejiwekea mkakati wa kuongeza ukusanyaji wa mapato kutoka sekta ya utalii, hivyo watakwenda kuviboresha vivutio hivyo ili kuwa na mazingira mazuri ya watalii kupenda kuyatembelea.

Wilaya ya Moshi imejaliwa kuwa na vivutio vingi vya utalii wa aina mbalimbali ndiyo maana wilaya hiyo inaitwa ni Benki ya vivutio vya utalii ambavyo bado havijatangazwa kikamilifu ili kuwa moja ya vyanzo vya mapato ya halmashauri hiyo.

TPC/FTK zatumia bil. 1.3 kuboresha shughuli za maendeleo Moshi DC

Kampuni ya kuzalisha sukari ya TPC Limited ya mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro, kwa kushirikiana na Shirika lisilo la kiserikali kutoka Uholanzi FT Kilimanjaro (FTK) inatumia zaidi ya shilingi Bilioni 1.3 kila mwaka katika kusaidia mchakato wa maendeleo ya jamii, ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa elimu.

Hayo yameelezwa katikati ya juma na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya FTK, Jaffary Ally, alipokuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za taasisi hiyo kwa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Moshi (MDC), mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Alisema  zaidi ya asilimia 50 ya fedha zinazotengwa kila mwaka, zinatumika kusaidia sekta ya elimu katika maeneo yanayozunguka kiwanda cha TPC Limited, hatua inayolenga kupongeza jitihada za serikali zinazolenga kuboresha elimu nchini.

Ally aliendelea kusema kuwa, taasisi hiyo ilitumia jumla ya milioni 300 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya elimu katika shule ya sekondari Chewe iliyopo wilayani Moshi, ambayo alisema kwa sasa ina wanafunzi 324, ambapo amesema mradi  uliotekelezwa katika shule hiyo ulihusisha ujenzi wa madarasa manne mapya, majengo mawili ya vyoo, jengo la jiko na ununuzi wa madawati 120.

“Miradi mingine inayohusiana na elimu ni pamoja na ujenzi wa shule ya msingi Miwaleni uliogharimu  shilingi milioni 73 ukarabati wa jengo la walimu wa shule ya sekondari Langasani uliogharimu shilingi milioni 26 pamoja na ukarabati wa vyumba viwili vya madarasa na ununuzi wa madawati 25 kwa shule ya msingi Chemchem kwa gharama ya  shilingi milioni 3.5,”alisema.

Ally ambaye pia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPC Limited (Utawala) aliendelea kusema kuwa mchango mwingine ni pamoja na ukarabati wa madarasa manne ya msingi katika shule ya msingi Kiungi uliogharimu jumla ya shilingi  milini 59 pamoja na ukarabati wa vyumba vya madarasa na ujenzi mpya katika shule ya msingi ya Mawalla, mradi ambao amesema gharama yake ilikuwa ni shilingi milioni 63.

Alifafanua kuwa  pamoja na hayo, FTK pia inachangia ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo yao katika ngazi ya Stashahada na Shahada ya Kwanza katika vyuo mbalimbali vya elimu ya juu kwa kuwasaidia katika kulipa ada, gharama za malazi na stationary huku wazazi na walezi wakichangia chakula na mengine muhimu.

Alisema katika mwaka wa masomo uliopita FTK ilisaidia jumla ya wanafunzi 41, msaada ambao ulikuwa wa  shilingi milioni 165,779,150/  pia jumla ya walimu 37 walipewa kazi ya kufundisha programu ya kujitolea katika shule za msingi tofauti ambapo jumla ya shilingi milioni 81.6  zilitumika kuwezesha walimu hao kwenye programu hiyo  ya kujitolea ya  kusaidia kufundisha.

Aidha Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya FTK, Jaffary Ally,  aliendelea kusema kuwa mbali na kuchangia sekta ya elimu, FTK pia iliwezesha programu ya miezi miwili ya uhamasishaji wa unyanyasaji wa watoto ambayo iligharimu shilingi milioni 7 programu ilianza kwa kikao cha uwezeshaji kikihusisha maofisa wa tawala ngazi ya wilaya, viongozi waliopo ngazi ya uongozi wa kata za Arusha Chini, Kahe na Msitu wa Tembo, pamoja na viongozi wa vijiji vinavyozunguka kampuni ya TPC Limited. , maofisa wa jeshi la polisi, wawakilishi kutoka taasisi za dini na wadau wengine katika jamii.