TaSUBa ni Wakala wa serikali iliyoanzishwa kwa mujibu wa
sheria ya Wakala wa Serikali Na. 30 ya mwaka 1997 kama ilivyofanyiwa
marekebisho mwaka 2009, kupitia tangazo la Serikali Na. 220 la Novemba 2, 2007.
Taasisi hii inatokana na kilichokuwa Chuo cha Sanaa Bagamoyo ambacho
kilianzishwa mwaka 1981 baada ya kuvunjwa kwa kikundi cha Sanaa za Maonesho cha
Taifa mwaka 1980.
Rashidi M. Masimbi ndiye aliyekuwa mkuu wa kwanza wa chuo cha
Sanaa na Utamaduni Bagamoyo kabla hakibadilishwa na kuitwa TaSUBa kuanzia mwaka
1981-1987 akafutiwa na J. Mwakipesile (1987-1987), R. Mashimbi (1989-1997), P.
Nyambasi (1997-2007) na Juma A. Bakari (2003-2007).
Baada ya kuundwa kwa Wizara ya Utamaduni mwaka 1962,
kilianzishwa kikundi cha Sanaa za Maonesho cha Taifa ambacho kilianza na fani
ya ngoma (1963), Sarakasi (1969) na Tamthilia (1974). Kazi kubwa ya Kikundi
hiki ilikuwa kufanya maonesho sehemu mbali mbali nchini ili kukuza mwamko wa
kuupenda na kuutukuza utamaduni wa Watanzania ambao mkoloni alijitahidi kwa
nguvu zake zote kuukandamiza.
Kazi za kikundi hicho ni kuwahamasisha Watanzania wajivunie
utamaduni wao na washiriki kikamilifu kuufufua, kuukuza na kuulinda. Makazi ya
Kikundi yalikuwa Shariff Shamba- Ilala, Dar es Salaam, mahali zilipo ofisi za
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).
Mtendaji Mkuu wa TaSUBa, Dk Herbert Makoye katika mahojiano
maalumu na anasema wamejipanga kuhakikisha Taasisi hiyo inakuwa kituo cha
mafunzo ya Sanaa na Utamaduni chenye ubora uliotukuka Afrika.
Bango la TaSUBa |
|
|
Hivyo ndivyo unaweza kusema kuhusu TaSUBa. Umaarufu wake
umekwenda mbali zaidi kwa kutoa manguli katika Sanaa ambao wamesambaa duniani
kufanya kazi hizo.
0 Comments:
Post a Comment