Wednesday, October 3, 2018

Misaada yazidi kumiminika Indonesia

Misaada inazidi kumiminika huku idadi ya watu waliofariki duniani ikifika 1,374 katika siku ya tano ya uokoaji.

Idadi ya waliokufa katika kimbunga na tetemeko nchini Indonesia imefikia 1,374. Wakati hayo yakijiri manusura wa tukio hilo wamekuwa katika wakati mgumu kutokana na misaada ya kiutu kushindwa kuwafikia kwa wakati.

Tetemeko hilo la magnitude 7.5 kwa kipimo cha Richter limeathiri pakubwa Kaskazini Mashariki mwa mjini mkuu Jakarta, mjini Palu. Misaada imekuwa ikitolewa taratibu katika maeneo yaliyoathirika tangu juhudi za uokoaji zianze siku tano zilizopita kutokana na miundombinu mibovu kuyafikia maeneo hayo. 

Jana Jumanne mamlaka husika nchini humo zilitoa taarifa ya kuwa wamezifikia wilaya nne zilizoathiriwa zaidi ambazo zote kwa ujumla zinakadiriwa kuwa na watu milioni 1.4. 

Mapema leo asubuhi kumeshuhudiwa zaidi ya ndege saba za mizigo zikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Palu zikiwa na tani za misaada iliyofungwa kwa rangi za taifa hilo nyekundu na nyeupe na kugongwa muhuri wa Ofisi ya Rais wenye maneno yanayosomeka "Msaada kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Indonesia."

0 Comments:

Post a Comment