Thursday, October 18, 2018

Mtangazaji wa DW Isack Gamba afariki dunia


Mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW, Isack Muyenjwa Gamba amefariki dunia. 

Taarifa za awali za kifo cha mtangazaji huyo Mtanzania zilidai amekutwa amefariki dunia nyumbani kwake Oktoba 18 mwaka huu. Mmoja wa marafiki zake waliozungumza na kwa njia ya simu kutoka Ujerumani amesema jana Gamba hakuonekana kazini pamoja na juzi Jumanne ya Oktoba 16. 

Akiwa nchini Tanzania, Gamba amewahi kufanya kazi vyombo mbalimbali vya habari ikiwamo Redio Uhuru, RFA, ITV na Radio One. Alitua mjini Bonn mwaka 2015. Aidha enzi za uhai wake amewahi kufanya kazi na watangazaji mahiri wengine Maulid Kitenge, Abdallah Mwaipaya, Sam Mahera na kadhalika.

0 Comments:

Post a Comment