Tuesday, October 17, 2023

Wazazi watakiwa mstari wa mbele kurudisha maadili

 Chifu Jani Kibacha amewataka wazazi kulinda Maadili ya Watanzania kuanzia majumbani mwao badala ya kusubiri mpaka watoto na vijana waharibike.


Chifu Jani Kibacha (wa kwanza kulia), Mzee wa Mila za Kipare Rajabu Mgonjwa, na Abdu Selemani katika picha ya pamoja muda mchache kabla ya tukio la kumkabidhi majukumu Komredi Patrick Boisafi zilizofanyika katika Ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Same katika ziara ya Kamati ya Siasa mkoa wa Kilimanjaro.


Chifu Kibacha amesema malezi yanaanzia nyumbani hivyo wazazi Wana wajibu wa kuwatunza watoto wao na kuwaelekeza mazuri wanayopaswa kuyafanya na kuyakataa mabaya.


"Mmomonyoko wa Maadili tunaupiga vita sana ili tuweze kurudi kule tulikotoka kwanza tunawashauri wazazi tuanzie Maadili kule nyumbani na tunapokuja kwenye JAMII tunaweza kufanikiwa," amesema Chifu Kibacha


Aidha Chifu Kibacha ameweka bayana kuwa utandawazi umekuwa miongoni mwa sababu zinazofanya vijana kusahau Mila na Desturi na Kama wazee wanajitahidi kuwarudisha katika asili yao.


"Mila za zamani zimeanza kupotea kwasababu ya utandawazi, wazee wakijaribu kuwarudisha vijana kwenye Mila na Desturi wanasema zimepitwa na wakati, wanapoona Mambo ya kisiasa wanaona Yale ya asili hayana maana kwako," ameongeza Chifu Kibacha


#JaizmelaTanzania






0 Comments:

Post a Comment