Wananchi wametakiwa kuilinda miradi inayotekelezwa na
serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ili iweze
kuwanufaisha kwa muda mrefu.
Mwenyekiti
wa (CCM), Mkoa wa Kilimanjaro Patrick Boisafi,
aliyasema hayo Oktoba Nne wakati
akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya NgareNairobi Wilayani Siha mkoani humo.
"Miradi
yote inayotekelezwa na Serikali
inahitaji kutunzwa, hivyo niwaombe wananchi wa wilaya ya Siha na mkoa wa
Kilimanjaro kwa ujumla, hakikisheni miradi hiyo inatunzwa kwani imetumia fedha
nyingi kuweza kutekelezwa,"alisema.
Aidha
aliwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za uchaguzi wa Serikali
za Mitaa ndani ya chama hicho na uchaguzi mkuu utakao fanyika mwaka 2025 waweze kumpa
kura nyingi za kishindo Rais Samia Suluhu Hassan.
Kwa
upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Siha Dkt. Haji Mnasi,
ameishukuru kamati y siasaa mkoa kwa kuweza kufika, kukagua na kutembelea
miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ili ya afya, elimu, maji na barabara.
"Namshukuru
sana Rais Samia kwa namna ambavyo
ameendelea kufungua uchumi wa wananchi kupitia miradi hiyo ya maendeleo
inayojengwa ndani ya wilaya ya Siha,"alisema Dkt. Mnasi.
Akizungumzia
mafanikio waliyoyapata ndani ya muda mfupi wa uongozi wa Rais Samia Diwani wa
kata ya Ngare Nairobi Patrick Boisafi, amesema kwenye sekta ya elimu kata hiyo
imepokea kiasi cha bilioni 1.3 ambazo zimewezesha kujenga shule mpya, mabweni, vyumba vya madarasa
pamoja na matundu ya vyoo.
Kamati
ya siasa mkoa ilianza ziara ya kikazi Oktoba 4, 2023 katika majimbo yote tisa
ya mkoa wa Kilimanjaro kwa lengo la kukagua uhai wa chama na Jumuiya zake ,
maandaalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa
pamoja na Utekelezeji wa Ilani ya
CCM ya mwaka 2020-2025 inatarajiwa kuhitimisha mnamo Oktoba 18, 2023.
0 Comments:
Post a Comment