Mnara wa Kumbukumbu ya Hospitali Maalumu Ngazi ya Taifa ya Magonjwa Ambukizi ya Kibong’oto umetajwa kuwa kivutio cha pekee cha Utalii kwa wageni na Wananchi wanaoendelea kuitembelea hospitali hiyo iliyopo Wilaya ya Siha Mkoa wa Kilimanjaro.
Akizungumza ofisini kwake katika mahojiano maalum na mwandishi wa gazeti la TANZANIA Leo na blogu ya JAIZMELA News Mkurugenzi wa hospitali hiyo Dkt. Leonard Subi, amesema Julai 16 mwaka 2022 Makamu wa Rais Dkt. Isdori Mpango alizindua Mnara wa kumbukumbu ambao ulikuwa unaonesha namna ya hospitali hiyo itakumbukwaje na kwamba baada ya mnara huo kuzinduliwa umekuwa kivutio cha pekee na cha ajabu kwa wageni wanaoitembelea hospitali hiyo kwa namna ambavyo umesanifiwa.
Dkt. Subi amesema nembo ya Mnara; inaonesha namna Kibong;oto inavyozingatia Utafiti , Sayansi katika kutoa huduma za matibabu.
Mapafu; Yanaashiria kwamba KIbong’oto ni moja wapo ya hospitali iliyoko ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inajishughulisha na matibabu ya magonjwa ya kuambukiza hususani Kifua kikuu na yale yanayoathiri zaidi mapafu.
Mnyoo; Watu walikuwa wakitumia kijiti katika matibabu yake ni moja ya mnyoo mrefu duniani ambaye aliwasumbua sana wananchi wa Afrika ya Magharibi ambapo alikuwa ana athari sana na kuitwa ni tatizo kubwa na nembo hiyo iliweza kuchukuwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) na kuitumia katika huduma za matibabu.
“Mnara huu ni wa aina ya pekee kwa sababu una elimu ya kutosha unaoitambulisha hospitali yetu, wageni wengi kutoka ndani na nje ya nchi wanakuja kuutembelea mnara huu ambao umekuwa ni kivutio tosha cha utalii,”amesema.
Amesema ya Kibong’oto ni hospitli iliyotumika katika utafiti wa matibabu ya ugonjwa wa kifua kikuu enzi za ukoloni na ikumbukwe kuwa ilichukua takribani miaka 60 tangu kugundulika kwa vimelea vya ugonjwa wa Kifua kikuu.
Amesema kumbukumbu ya mnara huo inaenda sambamba na “Wagonjwa wa kifua kikuu walikuwa wanatengwa na kuletwa hospitali ya kibong’oto takribani miaka 60 tangu kugunduliwa kimelea cha kifua kikuu toka mwaka 1882 na mwaka 1943 ndipo kuligundulika kwa dawa ya kifua kikuu,” amesema Dkt. Subi.
“Tangu kuanza kwa Hopsitali ya Kibong’oto mnamo mwaka 1926 wahanga wa ugonjwa huo walikuwa wakiletwa hapo na waliofariki walizikwa katika eneo lililotengwa hospitalini hapo ambayo sasa imekuwa sehemu ya kihistoria,”amesema.
Amesema mwaka 1926 ilipoanza kibong’oto ilianza kwa majaribio ya kifua kikuu na hospitali ya kibongo’oto ina sehemu ya kihistoria ambako wahanga wa ugonjwa wa kifua kikuu waliokuwa wakiletwa hapa kabla ya kugundulika kwa dawa hizo na wakati wa majaribio ya dawa wengine walikuwa wanafariki na waliokuwa wanafariki walikuwa wanazikwa hapa Kibong’oto.
Amesema enzi hizo dawa za kutibu ugonjwa wa kifua kikuu hazikuwepo, wananchi waliokuwa wakiugua ugonjwa wa kifua kikuu walikuwa wakitibiwa kwa kutumia jua pamoja na hewa safi (Fresh Air) na hospitali ya Kibong’oto itumika kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati zilizokuwa zikitawaliwa na Mwingereza.
“Mwaka 1882 na Mwanasayansi wa Kijerumani aliyefahamika kwa jina la Robert Koch alianza kufanya utafiti wa kupata dawa za kutibu ugonjwa huo, na ilipofika mwaka 1942 hadi 1943 ndipo dawa za kutibu kifua kikuu zilipoweza kugundulika rasimi na hospitali ya Kibong’oto ndiyo ilishiriki kufanya tafiti hizo hadi kupatikana kwa dawa hizo ambazo zinatumika hadi sasa.
Ameongeza kusema kuwa Hospitali Maalumu ya Taifa ya Magonjwa Ambukizi ya Kibong’oto ina eneo la hekari saba za makaburi ambapo takribani watu elfu tisa (9,000) walizikwa pale wakiwa ni wahanga mbalimbali wa ugonjwa wa kifua kikuu.
0 Comments:
Post a Comment