Monday, October 16, 2023

NIMRI yaongeza nguvu Kibong'oto Hospital





Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMRI) imekabidhi mashine ya Kifua kikuu ya kisasa yenye thamani ya Sh milioni 60, katika Hospitali Maalumu Ngazi ya Taifa ya Magonjwa Ambukizi ya Kibong’oto iliyopo Wilaya ya Siha Mkoa wa Kilimanjaro.



Akikabidhi mashine hiyo  juzi Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya (NIMRI) Profesa Said Aboud,  alisema mashine hiyo ina uwezo wa kutambua usugu wa dawa na kwamba pia itasaidia katika kutambua mapema TB sugu na kumwezesha mgonjwa kupata tiba sahihi ambayo itamwezesha kupona haraka.


"Katika kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuboresha huduma za afya kwa wananchi, Shirika la Maendeleo ya Watu wa Marekani (USAID) kupitia mradi wa Tifa, hospitali  ya Kibong'oto ni moja kati ya hospitali ambayo imebahatika kupata mashine hiyo,"alisema Prof. Aboud.


Profesa Aboud  alisema mashine nyingine wameikabidhi  katika Hospitali ya Mkoa ya Rufaa Jijini Dodoma na mashine nyingine imekabidhiwa katika Hospitali ya Kanda Mbeya, huku moja ikiwa katika Maabara Kuu ya Taifa ya Kifua Kikuu.


Alisema mashine hizo zitasaidia katika kutambua mapema kifua kikuu sugu na kupelekea wagojwa kupata tiba sahihi ambayo itampa mgonjwa wa TB kupona  haraka.


"Mashine hii ina uwezo wa kutamabua dawa za aina nyingi zaidi katika kuboresha huduma na afya kwa wagonjwa,"alisema Prof. Aboud.


Akipokea mashine hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa hospitali ya Kibong’oto Dkt. Leonard Subi, Kaimu Mkurugenzi wa hospitali hiyo Magreth Chipeta; 

Aliushukuru uongozi wa Taasisi ya NIMRI kwa kuwawezesha kifaa hicho na kuomba endepo zitapatikana fursa za  mashine zingine wasisite kuwapatia ili waendelee kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi.

"Malengi ya Hospitali Maalumu Ngazi ya Taifa ya Magonjwa Ambukizi ya Kibong’oto ni kuendelea kutoa huduma bora kwa jamii, tuwaombe kama itatokea fursa nyingine msisite kutupatia,"alisema.



0 Comments:

Post a Comment