Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi Tanzania Jumuiya ya Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Kilimanjaro Daudi Mrindoko amewapa mbinu wanachama wa Chama hicho ili kupata fedha za ujenzi wa Ofisi za Kata za Chama Cha Mapinduzi katika Kata zya Marangu Mashariki.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi Tanzania, Jumuiya ya Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Kilimanjaro Daudi Mrindoko, ameyasema hayo wakati akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Kata ya Marangu Mashariki, Wilaya ya Moshi mkoani humo.
Mpango kazi huo wa ujenzi wa ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM) ngazi ya kata, umeanza kwa kishindo baada ya kuanzisha harambee inayomfanya kila mwanacha katika kata husika kutoa kiasi cha fedha ili kutatua changamoto hiyo.
Mrindoko ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa mkoa wa Kilimanjaro, amelazimika kuanzisha harambee za ujenzi wa ofisi za chama, baada ya kupokea changamoto za ukosefu wa ofisi za chama ambapo hulazimika kuomba nyumba za jirani kufanyia mikutano yao ya kichama.
Katika kata ya Marangu Mashariki, ameunda kamati ya ujenzi wa jengo la ofisi ya chama kata, ambapo amechangia madirisha na mlango wa ukumbi ili kukamilisha ujenzi huo.
Akiwa katika kata ya Ng'ambo Mrindoko aliendesha harambee ya ujenzi wa ofisi ya chama ngazi za kata, ambapo kiasi cha Sh. Milioni 1.2 zilipatakina katika harambee hiyo.
Aidha Mrindoko ameunda Kamati ya ujenzi wa wa ofisi ya chama kata ya Masama Kati ambapo pia amewahasisha wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM kata hiyo kujenga ofisi ya chama kata kwani uhai wa chama ni kuwa na ofisi.
Amesema katika kuunga mkono juhudi za Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha Tanzania inajikomboa kiuchumi.
Katika hatua nyingine amewataka viongozi wa chama ngazi ya kata kuhakikisha wanaongeza wanachama wapya.
0 Comments:
Post a Comment