Wananchi
wa Kata ya Ndumeti Wilayani Siha Mkoa wa Kilimanjaro wameiomba Serikali
kuwajengea kituo cha Afya ili kuondokana na adha ya kutembea umbali mrefu wa
zaidi ya KM 7 kufuata huduma hiyo katika kata jirani ya Ngara Nairobi.
Wameyasema hayo mara baada ya Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM taifa Mkoa wa Kilimanjaro Ndugu. Seleman Mfinanga wakati akitembelea katika miradi mbali mbali ya Maendeleo,
Na
kushuhudia fedha nyingi zilizotolewa na Serikali ya Dkt. Samia Suluhu
Hassan ambapo katika Shule ya Sekondari
Matadi Madarasa 10 na matundu ya vyoo 12 yamejengwa na kuanza kutumika.
"
Fedha hizo zikija ujenzi uendelee kwa kasi kubwa ilikutatua changamoto hii
inayowakabili wananchi, pia kutimiza malengo ya wananchi na kuongeza imani kwa
CCM" MNEC
Katika
hatua ingine, Mnec amesema changamoto ya kutokuwa na soka kata ya Ndumeti
imekaa vizuri na serikali itaenda kutoa kutoa tamko Rasmi la eneo kibaoni kuwa
soko la kata hiyo. " Changamoto ya soko imekaa vizuri eneo lile tamko
rasmi la serikali litakuja kutolewa, lakini kwa maelekezo ya Chama eneo lile
litaendelea kuwa soko". MNEC
Aidha Diwani wa Kata hiyo Mhe. Vicent Kileo
amesema Serikali imeombwa na kiasi cha Shilingi Milioni 30 kwaajili ya kufungua
mchepuo mmoja wa maji ili wananchi wa kijiji cha Matadi na Roseline kuondokana
na changamoto ya Maji.
Hayo
yamefanyika katika ziara ya kamati ya Siasa ya
Chama cha Mapinduzi Mkoa wa kilimanjaro katika Wilaya ya Siha na
kuwataka viongozi wa serikali kuja kata ya Ndumeti kutoa majibu ya uhakika kwa
wananchi iliwaendelee kukiamini chama chao.
0 Comments:
Post a Comment