Ukweli na Kuheshimiana ni kiini ujenzi wa jamii zetu

Ulimwenguni kwa sasa kumejaa habari potofu na upotoshaji, ni muhimu kuhakikisha kwamba ukweli na kuheshimiana vinakuwa kiini kwa ujenzi wa jamii zetu.

Mapambano dhidi ya Habari za Uongo hayapaswi kukoma

Habari za uongo, habari za uongo zinazosambazwa kwa lengo la kumdhuru mtu au jambo fulani, huifanya jamii kuwa na sintofahamu. Zinaweza kutumika kwa madhumuni ya kiitikadi, kisiasa au hata uhalifu, kama vile ulaghai mtandaoni unaolenga kuiba data ya kibinafsi.

Utandawazi na Athari zake katika Uandishi wa Habari

Katika jamii yetu ya kisasa, ambapo habari ziko kila mahali na zinaweza kupatikana kwa kila mtu, mara nyingi ni ngumu kutofautisha kati ya vyanzo vya kuaminika na habari bandia.

Uandishi wa Habari nguzo msingi mkuu kwa ujenzi wa jamii inayojitambua

JAIZMELA blog ni miongoni mwa vyanzo vya habari, zilizochakatwa kwa kuzingatia miiko ya uandishi wa habari.

Mila na Desturi ni nguzo muhimu

Mila na desturi ni nguzo muhimu sana katika utamaduni wa jamii yoyote ile; mila ni sawa na sheria zisizoandikwa. Mila ni taratibu za maisha na mwenendo zinazofuatwa na jamii fulani katika utendaji kulingana na historia na utamaduni wao. Mila zinatambulisha maadili ya jamii husika, huelezea namna jamii inavyoendesha mambo yake.

Wednesday, March 22, 2017

Shahidi Na. 6 Kesi ya Scorpion: Huyu ni raia mwema

DAR ES SALAAM
Salum Njwete (kushoto)
akitolewa mahabusu
Machi 22, 2017
Kesi inayomkabili Salum Njwete maarufu Scorpion imeendelea tena leo katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kwa shahidi wa sita kutoa ushahidi wake.
Shahidi huyu ambaye ni Meneja wa Baa ya Kimboka ya Buguruni jijini Dar es Salaam Hussein Rashid mwenye miaka 41 ameiambia mahakama kuwa Scorpion anamfahamu kuwa raia mwema.
Awali mbele ya Hakimu Mkazi Flora Haule, Mwendesha Mashtaka Nassoro Katuga amedai kuwa shahidi huyo yupo tayari kuisaidia mahakama.
Shahidi huyo ameiambia mahakama kuwa anamfahamu Scorpion kama ‘Ticha’  na kwamba ni mlinzi wa amani wa wafanyabiashara wadogo wa Buguruni aambao huwa wanampatia Shilingi 10,000 kila siku kwa ajili ya kuwalindia bidhaa zao.
Pia ameiambia mahakama hiyo kuwa tangu aanze kufanya ulinzi katika maeneo ya wafanyabiashara wadogo wezi, wakabaji na wale wanaouza vitu vya wizi wametoweka.
Aidha shahidi huyo amedai kuwa siku ya tukio ‘Scorpion’ alikwenda kwa meneja huyo kwamba kuna mwizi kapigwa eneo la Shell.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa Septemba 6 mwaka jana Scorpion mwenye miaka 34 akiwa Buguruni Shell alimchoma kwa kisu mlalamikaji Said Mrisho machoni, mabegani na tumboni kisha kumnyang’anya vitu vya thamani na fedha taslimu.
Kesi hiyo itatajwa tena Aprili 3, mwaka huu.
Salum Njwete baada ya kusikiliza ushahidi wa kesi inayomkabili akirudishwa mahabusu.

Phonia Bundala , Bplus, Felister Henry in Star TV

Watangazaji wa Sahara Media Group Phonia Bundala, BPlus na Felister Henry

Kituko cha Mjasiriamali huyu

Hatukatai kuwa mjasiriamali lakini katika kila jambo lina kiasi. Hata kama maisha yanakwenda kombo ni vema kutumia utashi ili kuepukana na usumbufu usiotarajiwa. Pichani mjasiriamali akiiuza maji na juisi zake katika barabara ya mwendo wa haraka (UDART) maeneo ya mataa ya Magomeni jijini Dar es Salaam kama alivyokutwa. 


Tuesday, March 21, 2017

Polepole: Tunamlia ‘Timing’

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) akisoma magazeti muda mfupi kabla ya mahojiano maalum na RFA
 WITO umetolewa kwa wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), kuwa wasipozingatia maadili ya chama hicho watakuwa kwenye wakati mgumu kuwahi kutokea katika maisha yao.

Hayo yanajiri wakati ambapo jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake likiwa limefunikwa na sakata la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuvamia ofisi za Clouds Media Group akiwa na askari wenye silaha za moto.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika mahojiano na Mtangazaji wa RFA Najma Abdallah.
Katika mahojiano mubashara na kipindi cha RFA Bonanza cha Redio Free Africa asubuhi ya Machi 20, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho Humprey Polepole amesema anapoonekana mwanachama anakiuka kanuni na utaratibu huwa na subira lakini mwishowe huchukua hatua

“Hakuna aliyewahi kufikiri kama tungechukua uamuzi mkali kabisa wa kuwafukuza uanachama…unapoona kiongozi anakosea ngoja nitumie lugha ya vijana unamlia timing muda utakapokuwa tayari unakula kichwa,” anasema Polepole.

Polepole ameongeza kuwa chama hicho hakiwezi kumwacha kila mtu afanye anachotaka, bali kufanya kwa maslahi ya wananchi ndio kunasisitizwa kila wakati.


Aidha Polepole ametoa wito kwa wanachama kuelekea uchaguzi mkuu wa ndani wa chama hicho kuwa wanapaswa kupiga vita rushwa ili kuendelea kukilinda chama kwani hakiko tayari kuwa na viongozi walioingia kwa rushwa.

Mtangazaji wa Redio Free Africa, Najma Abdallah

Mtangazaji wa Redio Free Africa, Najma Abdallah akiwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Wednesday, March 15, 2017

Kortini kwa makosa ya mtandao

NA MWANDISHI WETU
Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam
Washtakiwa saba wa makosa ya Mtandao kutoka nchi za Pakistan na Sri lanka wamefikishwa mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kujibu mashtaka saba yanayowakabili.

Wamesomewa mashtaka yao kwa mara ya kwanza ambapo hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na Mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi hiyo hivyo ushahidi utakapokamilia itasikilizwa mahakama kuu kitengo cha Wahujumu Uchumi.

Washtakiwa hao saba ni pamoja na sita kutoka Pakistan ambao ni Dilshad Ahmed, Rohail Yaqoob, Khalid Mahmood, Ashfaq Ahmad, Muhamad Aneess na Imtiaz Ahmad Qammar huku Ramesh Kandasamy akitokea Pakistan.

Mashtaka yao ni kuingiza vifaa vya mawasiliano bila kibali, kuunganisha vifaa vya mawasiliano kwenye mitandao ya nchi bila kibali, kuunganisha miundombinu ya mawasiliano nchini bila kibali, kutumia vifaa vya mawasiliano kuiba fedha kwa mtandao, kuendesha vifaa vya mawasiliano bila kibali, matumizi mabaya ya mitandao ya mawasiliano na kufanya kazi bila kibali cha kazi nchini.

Mahakama Kuu ya Tanzania Kitengo cha Wahujumu Uchumi (mahakama ya mafisadi) ndio yenye uwezo wa kusikiliza kesi hii hivyo watuhumiwa hawakutakiwa kujibu chochote kwani upelelezi ukikamilika kesi hiyo itasikilizwa mahakama kuu.


Kesi hii imewekwa kwenye kitengo cha uhujumu uchumi hivyo watuhumiwa wote wamerudishwa rumande mpaka watakapoomba dhamana Mahakama kuu kitengo cha Uhujumi Uchumi

Monday, March 13, 2017

Uzalishaji tumbaku washuka Chunya

NA MWANDISHI WETU
Shamba la Tumbaku nchini Tanzania
UZALISHAJI wa zao la Tumbaku kwa wakulima Wilaya ya Chunya (CHUTCU), mkoani Mbeya umeshuka katika misimu mitatu mfululizo kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kuporomoka kwa bei ya zao hilo katika soko la dunia.
                  
Taarifa ya Chama Kikuu cha Ushirika wa zao la Tumbaku wilayani Chunya, imebainisha uzalishaji wa Tumbaku umeshuka kutoka Kilogramu Milioni 13.7 mwaka 2013/2014 mpaka kilogramu Milioni 11.4 zinazotarajiwa kuvunwa katika msimu huu.

Tumbaku likiwa ni miongoni mwa mazao makuu yanayoliingizia Taifa fedha za kigeni lakini likikosa ushindani mkubwa wa soko huria la wanunuzi ambao kwa sasa wapo wachache hapa nchini.

Hata hivyo wakulima wa tumbaku wilayani humo wameiomba Serikali kufanya mazungumzo na China ambayo inadaiwa kuwa na matumizi makubwa ya tumbaku kwa kununua asilimia 34 ya Tumbaku inayozalishwa Duniani lakini haijawahi kununua Tumbaku ya Tanzania.

Chama cha Ushirika wa Tumbaku wilayani Chunya, kina wanachama zaidi ya elfu nane wanaotoka katika vyama 23 vya msingi.


Friday, March 10, 2017

Agatha Kisimba, presenter STAR TV

Ungependa siku moja uwe kama Agatha Kisimba?
Agatha Kisimba akitangaza Machi 9, 2017
Agatha Kisimba ni nani? Huyu ni mwandishi wa habari na mtangazaji wa Star TV ambaye mara nyingi utaweza kumuona katika usomaji wa magazeti kupitia kituo hicho mahiri cha runinga nchini Tanzania. Siri kubwa ya mwanadada huyu ni kufanya kazi kwa bidii na kujituma. Kwa ujumla wake nidhamu ndio kila kitu katika mafanikio ya maisha.
Here you pose then you go, ha ha ahaaa!

Agatha Kisimba

TANESCO kuendesha operesheni 'Kata Umeme'

NA MWANDISHI WETU
Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) limetoa notisi ya siku 14 kwa wadaiwa wa Bili za Umeme na baada ya hapo wataendesha zoezi la ukataji wa umeme nchi nzima huku Wizara na Taasisi za Serikali zikidaiwa shilingi Bilioni 52,Makampuni  Binafsi na wateja wadogo shilingi Bilioni 94 pamoja na Shirika la Umeme Zanzibar(ZECO) shilingi Bilioni 127.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Dk. Tito Mwinuka alisema malimbikizo hayo ya madeni yamekuwa yakikwamisha jitihada za utekelezaji wa majukumu msingi ndani ya Shirika hilo, na kuongeza limekuwa likipitia wakati mgumu wakati Matengenezo ya miundombinu pamoja na utekeleza wa miradi mbalimbali.

Dkt. Mwinuka alisema zoezi hilo litakuwa endelevu kwa wadaiwa na watakoshindwa kulipa madeni na  hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wadaiwa hao.

Aidha Dkt. Mwinuka alisema iwapo wadaiwa hao watalipa malimbikizo ya madeni hayo Shirika litaweza kutatua kwa hatua baadhi ya changamoto ambazo zinawakabili.

Kwa muda mrefu Shirika la Umeme nchini limekuwa likilalamikia wateja wake kulimbikiza madeni na wanapoendesha zoezi la ukusanyaji wa madeni huwa hawafikii malengo.

Thursday, March 9, 2017

Once in Life Time, Kiss FM Dar es Salaam


Wafanyakazi wa Redio Kiss FM studio ya Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutembelewa na Madam Sherry Mlope wa Studio za Kiss FM Mwanza Machi 6, 2017 (Picha zote na Johnson Jabir).

Madam Sherry Mlope

Kutoka kushoto Ibrahim Jonathan, Edo Fabian, Bplus, Petro, Felister Henry, Herman Kihwili, King Sempa, Pendo Michael

Abdul Diallo ‘Chief’ (kulia) na Pendo Michael 

Kikao kikiendelea katika ukumbi wa Studio za Kiss FM, Dar es Salaam maeneo ya Morocco, Kinondoni

Madam Sherry Mlope akifuatilia jambo katika kikao hicho.

John Lupokela (wa kwanza kulia) hakuwa nyuma kufuatilia kinachoendelea

Bplus akichangia mchango wake wa mawazo kwenye kikao hicho.

Are they frustrated? Hapana, wanafuatilia 

Abdul Diallo 'Chief'

Stella Joseph (katikati), alikuwa miongoni mwa waliohudhuria kikao hicho 

Ibrahim Jonathan akichangia mchango kwenye kikao hicho

Mbwana Shomari akiwa studio wakati kikao kikiendelea

Kutoka kushoto Ibrahim Jonathan, Edo Fabian, Bplus

Madam Sherry akisisitiza jambo katika kikao hicho.

Abdul Diallo na Madam Sherry
KISS FM SLOGAN

“Sisi tunaanza, Wao wanafuata

Monday, March 6, 2017

Hospitali ya Taifa Muhimbili na changamoto zake

NA MWANDISHI WETU
Mkurugenzi wa Tiba wa MNH, Dkt. Hedwiga Swai akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani), kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji Dkt. Julieth Magandi

Imeelezwa upungufu wa rasilimali watu katika maeneo ya ubobezi na ubingwa wa juu kwenye Hospitali ya taifa ya Muhimbili ni miongoni mwa changamoto zinazoikabili hospitali hiyo kwa sasa.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari leo Mkurugenzi wa Tiba wa hospitali hiyo Dkt. Hedwiga Swai amesema wamepata mafanikio makubwa hadi sasa ikiwamo upanuzi wa eneo la wagonjwa wa dharula ambao wameongezeka kutoka 100 hadi 300 kwa siku huku vikifungwa vifaa vya kisasa kuhudumia.
Aidha Dkt. Swai amesema hospitali hiyo imefanikiwa kupeleka wataalamu nje ya nchi kwa ajili ya kujifunza upandikizaji wa figo wakifikia 19 walio tayari kuanza kazi hiyo.
Hata hivyo Dkt. Swai amesisitiza kuwa ufanisi huo unapaswa kuungwa mkono licha ya uhitaji wa maeneo mengine kuwa mkubwa na kuongeza kuwa wameomba kibali cha kuajiri wauguzi na madaktari wa kada mbalimbali ili kuongeza ufanisi.
Mbali na changamoto hiyo uchache wa vifaa tiba na uchakavu wa miundombinu  nao umekuwa ukipunguza kasi ya utoaji wa huduma licha ya kuendelea kutafuta mbinu mbalimbali za kupunguza. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji Dkt. Julieth Magandi amesema hospitali hiyo ina mpango wa kuendelea kuongeza mapato ya ndani kutoka Shilingi Bilioni 4.5 miezi sita iliyopita hadi Shilingi Bilioni 5 kwa mwezi ili kuimarisha maeneo mbalimbali kwa ukuaji wa huduma hiyo.
Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji Dkt. Julieth Magandi (kushoto) na Ofisa Uhusiano John Stephen

Friday, March 3, 2017

Godbless Lema aachiwa kwa dhamana leo

NA MWANDISHI WETU
Godbless Lema, Mbunge wa Arusha Mjini
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha leo imemuachia kwa dhamana Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema.
Awali mahakama hiyo ilimtaka mbunge huyo kuwa na wadhamini wawili na Shilingi Milioni tatu akini ikafanya marekebisho kwa kumtaka Lema kusaini bondi ya shilingi milioni 1 ambapo alikidhi vigezo na kuachiwa huru.
Katika kesi hiyo iliyotolewa maamuzi majira ya saa 7:30 mchana, Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Mjini baada ya kupitia hoja za mawakili pande zote imemwachia kwa dhamana hiyo kwa masharti ya wadhamini wawili na kusaini bondi ya shilingi milioni tatu.

Lema amekaa mahabusu kwa takribani miezi minne tangu alipokamatwa mwezi Novemba mjini Dodoma na kusafirishwa kupelekwa Arusha kisha kufunguliwa kesi ya uchochezi.
Hali ilivyokuwa baada ya Godbless kuachiwa akitokea gereza la Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha

Thursday, March 2, 2017

Sober House Zanzibar kupekuliwa

NA SHARIFA SULEIMAN

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar   imezitaka  taasisi  husika kuzifanyia utafiti Soba House  zote ili kubaini kama zinajihusisha na kuingiza dawa za kulevya visiwani humo kinyume na malengo ya uanzishwaji wake.
Akizungumza katika kikao cha Baraza la Wawakilishi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa  Rais  Mohamed  Aboud amesema kuwa serikali haiwezi kuachia chombo ambacho chochote kinajihusisha na masuala ya dawa za kulevya ili kuwaponya vijana ambao ndiyo nguvu kazi ya taifa.
Nao baadhi ya wajumbe wa baraza hilo wameliomba Jeshi la Polisi kuwajibika ipasavyo ili wale wote wanajihusisha na biashara hiyo kuchukuliwa hatua   za haraka. 
Katika kikao  hicho wawakilishi wamepitisha maazimio mbalimbali ikiwamo viongozi na jamii kwa ujumla kushirikina katika kampeni ya kuwafichua watu wanaohusika na uingizaji wa dawa hizo.


Boeing waleta kiwanda Kenya, Afrika Kusini

ILLINOIS, MAREKANI
Boeing 787
Shirika kubwa la kutengeneza ndege la Marekani Boeing limefungua ofisi mpya mjini Johannesburg Afrika Kusini na Nairobi Kenya zitakazoshughulikia biashara zake barani Afrika.
Ofisi ya Johannesburg itaongozwa na Miguel Santos, ambaye ni mkurungezi wa Boeing kwenye kanda ya Afrika ya chini ya Sahara na pia mkurungezi wa mauzo barani Afrika.

Kampuni hilo lilianzishwa miaka 100 iliyopita na William Boeing mzaliwa wa Detroit nchini Marekani.