![]() |
Muonekano wa Qatar kutoka mbali |
Tuesday, June 6, 2017
Sudan yataka kuwa msuluhishi mgogoro wa Qatar
Monday, June 5, 2017
Cisco Mtiro is no more
![]() |
Cisco Mtiro enzi za uhai wake |
Mkuu wa Itifaki mstaafu Balozi Cisco Mtiro amefariki.Taarifa ya familia
imesema Mtiro amefariki dunia katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam alikokuwa
anapatiwa matibabu. Aidha msiba upo nyumbani kwa marehemu Mikocheni B. Enzi za
uhai wake aliwahi kugombea ubunge wa Temeke akipambana vikali na Agustino
Mrema. Mwaka 2009 aliteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania
katika nchi za Malaysia , Ufilipino , Cambodia ,
Singapore na Laos .
Wednesday, May 31, 2017
Zitto atoa ya moyoni kifo cha Ndesamburo
![]() |
Philemon Ndesamburo, enzi za uhai wake |
“Salaam zangu za rambirambi Kwa dada yangu mpenzi
Lucy Owenya Kwa kupotelewa na baba mzazi Mzee Philemon Kiwelu Ndesamburo. Ni
msiba mkubwa Kwa watu wa Kilimanjaro na hasa Moshi Mjini ambapo Mzee Ndesa Pesa
alikuwa mwakilishi wake Bungeni kuanzia Mwaka 2000 mpaka Mwaka 2015.
Kilimanjaro imepoteza mtu ambaye aliweka maslahi ya mkoa wake mbele kuliko kitu
kingine chochote. Ni msiba mkubwa Kwa wanachama wa CHADEMA ambacho alikuwa
Mwenyekiti wake Wa Mkoa tangu Chama kimeanzishwa mpaka mauti yalipomkuta.
Huwezi kutaja maendeleo ya CHADEMA kwa nchi yetu bila ya kutaja jina la Mzee
Ndesamburo. Nimepata bahati ya kufanya naye kazi Kwa karibu, naweza kutamka
bila wasiwasi kwamba ni mmoja wa watu waliokipenda Chama chake Kwa dhati
Kabisa. Ni msiba mkubwa Kwa Watanzania. Mzee Ndesamburo alitumia uwezo wake Wa
kifedha na kiakili kuimarisha mfumo wa Vyama vingi nchini kwetu. Mchango wake
katika kupigania Demokrasia nchini ni wa kupigiwa mfano na Kwa Kweli wengi wetu
Leo tunafaidi matunda ya Vyama vingi Kwa sababu ya kazi kubwa ambayo Mzee
Ndesamburo na wenzake walio hai na waliotangulia mbele ya haki walifanya. Mzee
Ndesamburo amechangia Sana ukuaji wa sekta ya utalii nchini. Kupitia kampuni
zake za Keys Hotels ameweza kuchangia Sana ukuaji wa sekta ya Utalii nchini
kwetu. Bungeni alikuwa mstari wa mbele kutaka uhifadhi wa mlima Kilimanjaro
kutokana na tishio la theluji kuondoka katika uhai wetu ( in our life time).
Kwa hakika Vyuo Vikuu vyetu vya Umma vingekuwa vinatenda haki Mzee Huyu
angepewa Shahada ya Uzamivu ya Heshima Kwa mchango wake katika Maendeleo ya
sekta ya Utalii nchini kwetu. Nawapa pole Sana watoto, wajukuu na vitukuu vya
Mzee Ndesamburo. Mzee wetu aliishi maisha yake na ameacha ‘ legacy ‘ yake.
Najua maumivu yenu lakini tupo wengi tunaoumia nanyi. Mungu awavushe kwenye
mtihani huu mkubwa. Muwe wamoja na mshikamane. Poleni Sana ndugu zangu wa CHADEMA
Kwa kupotelewa na Kiongozi wenu na Kiongozi wetu pia. Poleni Sana wana Moshi
Mjini na wana Kilimanjaro wote. Poleni Sana Watanzania. Pumzika Kwa Amani
Philemon Kiwelu Ndesamburo. Hiyo ni njia yetu sote. Amina”
![]() |
Zitto Kabwe |
Monday, May 29, 2017
Kufuturisha kwapigwa marufuku Zanzibar
![]() |
Futari ya Mfungo wa Ramadhani |
Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar imepiga
marufuku kuftarisha katika
kipindi hiki cha
mwezi mtukufu wa
Ramadhan pamoja na uuzwaji
wa vyakula kiholela
hususani vilivyopikwa ikiwamo
juisi isipokuwa wa
maeneo yaliyoruhusiwa kisheria.
Marufuku hiyo imekuja visiwani humo ili kukabiliana na maradhi ya
kipindupindu baada ya kutokea kwa visa 23 vya wagonjwa wa maradhi hayo hali
ilisababisha kufunguliwa kwa kambi maalum katika Hospitali ya Chumbuni kwa
wagonjwa wenye vimelea hivyo.
Akitoa taarifa hiyo
kwa waandishi wa
habari Kaimu Waziri
wa Afya Riziki
Pembe Juma amesema
kuwa ugonjwa wa
kipindupindu hususani Unguja umerejea
hivyo kuna haja ya kuweka mazingira ya usafi ili kuepuka maradhi hayo
ikiwamo kuacha kufuturisha na kuongeza kuwa maeneo yanayoongoza kwa visa vya
kipindupindu ni Mtoni Kidatu na Chumbuni.
Aidha serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeweka mikakati ya kukabiliana
na maradhi hayo ikiwamo kutoa elimu kwa wananchi juu ya maradhi hayo.
Monday, May 22, 2017
Vituko vya Machinjioni: Vingunguti
Wengi wanafahamu kuwa siku njema huonekana asubuhi. Wataalamu wa
Saikolojia wanaamini kuwa siku njema huanza siku ya nyuma yaani jana. Ikiwa na
maana kuwa ili siku iwe njema maandalizi yake huanza jana na kesho yako ni
kwasababu ya leo ulivyoiandaa. Iwe kwa jambo zuri au baya yote hayo ni kutokana
na maandalizi yako siku ya nyuma. Kama inavyoonekana picha kituko hiki
kilitokea katika machinjio ya mifugo ya Vingunguti jijini Dar es Salaam saa 3
asubuhi ya Mei 21, 2017 pale wanunuzi
wawili ambao majina yao hayakufahamika mara moja waliposhindwa kuelewana na kupeana
songombingo la hatari lililowatoa udenda hata kusukumiana kwenye uchafu wa
machinjioni hapo.
Bata wana tabia gani?
Bata dume wa kufugwa nchini Tanzania akiwa amesimamia mguu mmoja, ikiwa ni sehemu yake ya starehe. |
Mwili wote wa bata kwa ujumla ni mrefu na mpana, na bata wengi kwa
wastani wana shingo fupi lakini shingo la bata bukini na bata-maji ni ndefu.
Umbo la mwili la mabata kwa kiasi fulani hutofautiana na hawa kwa kuwa
kidogo wa duara kidogo. Miguu yenye magamba ni yenye nguvu na iliyokuwa vizuri,
na kwa kawaida, na hurushwa nyuma kabisa ya mwili, hivyo zaidi hasa kwenye
spishi za majini.
Mbawa zake ni zenye nguvu na kwa ujumla ni ndogo na zilizochongoka, na
kupaa kwa bata kunahitaji mapigo ya haraka bila ya kupumzika, hivyo kuhitaji
misuli yenye nguvu sana .
Hata hivyo spishi tatu za bata aina ya steamer hawawezi kuruka kabisa.
Spishi nyingi za bata hushindwa kuruka vizuri kipindi cha kupukutisha
manyoya ya zamani na kuotesha mapya; hutafuta mazingira salama yenye chakula
kingi wakati huo. Hivyo basi kipindi hiki hufuata baada ya kipindi cha kuhama.
Ndege hawa wana rangi mbalimbali. Spishi kubwa hutafuta chakula
aghalabu ardhini au kwa maji machache. Spishi ndogo nyingine hula mimea ya maji
na huzamia kichwa chao tu, nyingine huzamia kabisa ili kukamata samaki,
wanyamakombe au mimea ya maji, lakini spishi kadhaa hutafuta chakula ardhini.
Hujenga matago yao
ardhini, juu ya mwamba, ndani ya shimo la miti au ndani ya pango la sungura,
mhanga.
Manyoya ya spishi kadhaa hupendwa sana
kama kijazo cha mito ,
mifarishi, mafuko ya kulalia na makoti. Spishi nyingi za mabata hutumika kama chakula.
CHANZO: Wikipedia/Jabir Johnson
Bata jike wa kufugwa nchini Tanzania akiwa katika malisho yake |
Muonekano wa shingo ya bata na eneo la kichwa cha bata wa kufugwa wa Tanzania |
Mtoto wa miaka 12 auawa, anyofolewa viungo
![]() |
Ramani ya Mkoa wa Singida |
MTOTO wa kike mwenye miaka 12 ameuawa mkoani Singida baada ya kunyongwa
kwa kamba ya ngozi na watu wasiojulikana, kisha mwili wake kunyofolewa baadhi
ya viungo na kutoweka navyo kwa kile kinachosadikiwa kuwa ni imani za
ushirikina.
Mtoto huyo Dorcas Meshack mkazi wa Kijiji cha Matongo Wilaya ya Ikungi
aliondoka nyumbani kwao juzi majira ya saa sita mchana na kuaga kuwa anakwenda
kuvuna mahindi kwenye shamba lililopo umbali wa mita 70 lakini hakurejea tena
hadi mwili wake ulipookotwa.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Mrakibu Mwandamizi Isaya Mbughi
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo
na kwamba upelelezi unaendelea.
Hata hivyo Mrakibu Mwandamizi Mbughi ameitaka jamii mkoani humo kuweka
utaratibu wa ulinzi dhidi ya watoto na kutoa taarifa kwa mtu yeyote au kundi
lolote linalojihusisha na vitendo hivyo.
Leo ni siku ya Wabaha'I
![]() |
Alama ya Wabaha'I |
![]() |
Bahá'u'lláh_(MÃrzá_Ḥusayn-`AlÃ_NúrÃ) mwaka 1868 |
Katika taarifa yake Mwakilishi wa Vyombo vya Habari wa Baraza la Kiroho
la Wabaha’I wa Dar es Salaam Qudsiyeh Roy amesema tangazo la Bab ni mojawapo ya
siku takatifu tisa kwa mujibu wa imani yao
ambapo siku ya maadhimisho, Wabaha’I hawapaswi kwenda kazini ama Shuleni.
Ibada fupi, usomaji wa maandiko matakatifu, burudani ya nyimbo,
mazungumzo na chakula vitafanyika katika maadhimisho hayo.
Licha ya kusherehekea siku hii, wafuasi hao wa Bahaullah watakuwa
wakitimiza miaka 174 tangu kuzaliwa kwa Imani ya Baha’I, mnamo Mei 22, 1844 Bab
alikamatwa, kupigwa na kufungwa hatimaye aliuawa Julai 9, 1850 hadharani katika
uwanja wa Tabriz nchini Iran.
Wabaha’I wanaamini kuwa wadhihirishaji wote wa Mungu ni pamoja na
Ibrahimu, Krishna , Musa, Zoroasta, Budhaa,
Yesu, Muhammad, Bab na Bahaullah ambao ni waelimishaji watukufu.
Friday, May 12, 2017
Raila kufanya mkutano Mei 14 katika ngome ya Jubilee
![]() |
Raila Odinga akifanya maombi Jerusalem hivi karibuni. |
Mgombea urais kwa tiketi ya
Muungano wa Upinzani nchini Kenya (NASA), Raila Odinga anatarajiwa kuongoza
maelfu ya watu katika mkutano mkubwa wa kwanza akiwa na viongozi wa muungano
huo kwenye ngome za chama cha Jubilee kinachoongozwa na Rais Uhuru Kenyatta.
Hayo yanajiri baada ya
kumaliza safari yake ya kuhiji mjini Yerusalemu ambako Odinga alifanya maombi
katika mji huo mtakatifu kabla ya kuanza Kampeni za kuwani kiti hicho Agosti 8
mwaka huu.
Odinga anatarajiwa kurudi nchini
humo na kufanya mkutano huo Jumapili ya Mei 14 mwaka huu huko Nakuru katika
viwanja vya Afraha. NASA inaamini kwa kufanya mkutano katika eneo hilo tayari
wameshapata kura milioni 10.
Mratibu wa mkutano huo Boni
Khalwale amesema jana kuwa viongozi watano Kalonzo Musyoka, Musalia Mudavadi,
Isaac Ruto, Moses Wetangula na Raila wakitarajiwa kuhudhuria katika ngome hiyo
imara ya Jubilee.
Akiwa nchini Israel, Raila alizuru
ukingo wa Magharibi.
Tuesday, May 9, 2017
NEC yapiga hatua elimu kwa njia ya Redio
![]() |
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Kailima Ramadhani |
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa wito kwa wananchi walioko kwenye
halmashauri mbalimbali nchini, kuitumia vyema fursa ya utoaji wa elimu ya mpiga
kura kupitia redio kwenye halmashauri zao ili kuondoa manung’uniko kwenye
chaguzi.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo Kailima
Ramadhani wakati akizungumzia mpango wa kutoa elimu ya mpiga kura nchi nzima
ulioanza kutekelezwa jana katika mikoa kumi nchini.
Amesema kupitia mpango huo wananchi wanaosikiliza redio za kijamii
kwenye halmashauri nchini, watapata fursa ya kujifunza elimu ya mpiga kura na
kuelewa masuala yote muhimu yanayohusu mfumo mzima wa kupiga kura.
Utekelezaji wa mpango huo umegawanyika katika makundi matatu ambapo
kundi la kwanza limeanza kutoa elimu hiyo elimu hiyo kwenye mikoa ya
Kagera,Mwanza, Kilimanjaro, Morogoro, Mbeya na Dodoma.
Mikoa mingine itakayojumuishwa kwenye kundi hilo ni Ruvuma, Mara, Pwani
na Mtwara ambapo elimu hiyo itatolewa hadi Mei 20 mwaka huu.
Kundi la pili linatarajiwa kutoa elimu hiyo kuanzia Mei 24 hadi Juni 7
mwaka huu katika mikoa ya Geita, Tanga, Singida, Shinyanga, Lindi, Arusha,
Tabora, Kigoma, Iringa, Manyara, Rukwa, Katavi, Songwe, Njombe na Simiyu.
Thursday, May 4, 2017
Mizoga ya Tembo yapungua Selous Game Reserve
![]() |
Mzoga wa tembo baada ya kuuliwa na majangili |
MAUAJI ya tembo katika Mbuga
ya Selous yamepungua kutoka mizoga 184 hadi 84.
Hayo yanajiri wakati ambapo
tembo wawili kuuawa na wananchi hivi karibuni huku mmoja aking’olewa meno yake
katika kijiji cha Wenje Tarafa ya Nalasi wilayani humo.
Akizungumza katika kikao cha
Ulinzi na Usalama cha Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Kaimu Mkurugenzi wa
Operesheni ya kuuzuia Ujangili dhidi ya wanyama Pori Robert Mande amesema takwimu hizo zinaonyesha kuwa ukubwa
wa tatizo hilo umepungua kutokana na jitihada za kupambana na majangili.
Mande amesema mizoga ya tembo
imepungua kutokana na wafanyabiashara wakubwa wa pembe za ndovu kukamatwa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi
na Usalama wilaya ya Tunduru Juma Homera amewataka watu wanaomiliki Silaha
Kiholela kuzisalimisha kwenye ofisi za vijiji na vituo vya Polisi
Homera amebainisha kuwa wananchi
wanaoishi karibu na mipaka ya nchi jirani ya Msumbiji wanapata silaha hizo kwa
kubadilishana na chakula.
Kutokana na tukio hilo watuhumiwa
8 wa ujangili wamekamatwa
Kwa upande wake Mratibu wa
Shirika la PAMS Foundation
linalojishughulisha na Mapambano dhidi ya Ujangili Maximillan Janes amesema shirika limetoa ndege mbili ambazo
zinatumika kulinda wanyama wasiingie katika makazi ya watu pia kufuatilia
mienendo ya watu wanaojihusisha na ujangili.
Tuesday, May 2, 2017
Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2017
NA MWANDISHI WETU
Wanataaluma na
Wadau wa Habari nchini, hii leo wamekutana katika Kongamano la kujadili
mafanikio na changamoto zinazoikabili tasnia hiyo ikiwa ni sehemu ya
Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2017.
Kitaifa
Maadhimisho hayo yanafanyika Jijini Mwanza ambapo kilele chake ni kesho huku
mgeni rasmi anakitarajiwa kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John
Pombe Magufuli.
Miongoni mwa
wachangia mada kwenye kongamano hilo ni Makamu wa Rais wa Umoja wa Klabu za
Waandishi wa Habari nchini, Jane Mihanji, Mtaalamu wa masuala ya teknolojia
nchini, Innocent Mungy, Mwanasheria na Mwanataaluma ya Habari, James Marenga, na
Mkurugenzi Mkuu wa Wakfu wa Vyombo vya Habari nchini (TMF), Ernest Sungura.