Tuesday, June 6, 2017

Sudan yataka kuwa msuluhishi mgogoro wa Qatar

Muonekano wa Qatar kutoka mbali
Sudan imejitolea kuchukua nafasi kama mpatanishi katika kutatua mgogoro unaoendelea, kati ya Qatar na mataifa mengine ya Kiarabu. Wizara ya mambo ya nje ya Sudan imetoa pendekezo hilo, baada Saudi Arabia, Misri, Umoja wa Falme za Kiarabu, Yemen na Bahrain kusitisha uhusiano na serikali ya Qatar. Nchi hizo za Kiarabu zinaishutumu Qatar kuwa inafadhili makundi ya kigaidi katika kanda ya Ghuba. Qatar imesema madai hayo ya kusaidia makundi yenye misimamo mikali si ya kweli na hayana msingi wowote. Wakati huo huo, Kuwait imeitaka Qatar kuruhusu muda wa kufanyika jitihada ambazo zinaweza kupunguza mvutano huo.


0 Comments:

Post a Comment