Mgodi wa North Mara |
Kampuni ya Madini ya Acacia imeona matokeo ya
kushtua ikiwa ni saa chache baada ya Kamati ya Pili ya Rais iliyoundwa na Rais
John Pombe Magufuli kuwasilisha ripoti ambayo imeangazia nyanja za historia ya
kiuchumi na kisheria ya mauzo ya nje ya makanikia ya madini.
Ripoti ya Tume iliyoundwa mwezi Machi mwaka huu na
Rais John Magufuli iliyojikita kueleza kiasi cha madini na fedha ambazo Tanzania hupoteza kutokana na usafirishaji wa
mchanga wenye madini imedai kuwa Kampuni ya madini yenye makazi yake nchini Canada , Acacia
ambayo ni kampuni kubwa zaidi ya madini haikuwahi kusajiliwa nchini, hivyo
imekuwa ikifanya kazi kinyume cha sheria.
Katika matangazo ya moja kwa moja ya Televisheni
kutoka Ikulu, Rais Magufuli amesema Tanzania
imepoteza takriban shilingi trilioni 188 katika kipindi cha miaka 19 kati ya
mwaka 1998 na mwaka 2017 kupitia usafirishaji wamakinikia ya dhahabu na shaba .
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Acacia
imesema kwa mujibu wa data za zaidi ya miaka 20 tulizonazo ni vigumu kuoanisha
matokeo yao na
yaliyokutwa na kamati, kwani kamati imetoa thamani ya juu kwa zaidi ya mara 10
kuliko thamani halisi ya makanikia.
Tume hiyo imetoa mapendekezo imefanya ikiwamo ya
Acacia kulipa kodi inayodaiwa na mirahaba, kufanya majadiliano upya ya mikataba
mikubwa ya uchimbaji madini, umiliki wa Serikali katika migodi, na muendelezo
wa marufuku ya kuuza nje tuhuma ambazo imekanusha vikali.
Aidha Acacia imesema imekuwa ikifanya biashara kwa
kufuata utaratibu na sheria za Tanzania
na kuongeza kuwa tangu kuanza kwa uchimbaji wa madini wamekuwa wakilipa
mirahaba yote inayotakiwa kulipwa na kukaguliwa kila mwaka kwa viwango vya
Kimataifa.
Hata hivyo Acacia imekaribisha mazungumzo na
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mgodi wa Bulyahulu |
0 Comments:
Post a Comment