Nyama ikiwa katika machinjio |
Machinjio ya tatu punda nchini Kenya imefunguliwa katika eneo la
Nakwaalele mjini Lodwar,katika kaunti ya Turkana. Machinjio hiyo ya kampuni ya
Zilzha kutoka China itasindika
nyama ya punda pamoja na ngozi kwa ajili ya usafirishaji hadi China na nchi
nyingine za mashariki ya mbali.
Kufunguliwa kwa machinjio hiyo utaleta ushindani wa machinjio nyingine
mbili za Maraigushu,mjini Naivasha
katika kaunti ya Nakuru,na ile iliyopo Mogotio katika kaunti ya Baringo.
Shu Jing Long,mmojawapo wa wachina wanaoendesha kichinjio cha Zilzha
cha Turkana amesema machinjio hicho itatoa ajira kwa wenyeji zaidi ya 200.
Aidha Long amesema hamu yao hasa ipo katika
ngozi ya punda ambayo ina soko kubwa nchini China .
Afisa wa Afya kutoka Wizara ya Mifugo nchini Kenya Dkt Jonathan Tanui msimamizi
wa shughuli za uchinjaji katika machinjio cha Zilzha amesema machinjio hiyo
imefikia viwango vinavyotakiwa na kuongeza kuwa wanyama hao kabla ya kuchinjwa
ni lazima wapimwe ili kuhakikisha kuwa ni salama kwa kuliwa.
Punda mmoja anauzwa katika ya shilingi 8,000 hadi 10,000 za Kenya .
0 Comments:
Post a Comment