Mwili wa dereva bodaboda ambao haukutambulika mara moja ukiwa umelazwa pembezoni mwa barabara mita chache kutoka kituo cha Mabasi yaendayo kwa haraka cha Morocco jijini Dar es Salaam Juni 25, 2017 |
Dereva wa bodaboda
ambaye hajafahamika jina lake na mahali anapotoka amefariki dunia baada ya kugongwa
na gari maeneo ya Kinondoni Kanisani jijini Dar es Salaam mita 200 kutoka kituo
cha mabasi yaendayo kwa haraka cha Morocco .
Mashuhuda wa tukio hilo walisema ajali hiyo ilitokea saa 1:30 usiku wa
Jumapili ya Juni 25 mwaka huu wakati dereva huyo akiwa na wenzake watatu wakiwa
katika pikipiki iliyosajiliwa kwa Na. MC 861 AHE alipogongwa na gari ambalo
lilikimbia baada ya tukio hilo .
Aidha mashuhuda hao
walisema aliokuwa amewapakiza wametokomea kusikojulikana kutokana na sheria
kukataza kupakiza ‘mshikaki’ yaani watu zaidi ya wawili.
Dereva wa bodaboda
hiyo anakadiriwa kuwa na kati ya miaka 23-30 ilishuhudiwa dimbwi la damu
barabarani hapo kutokana na kupasuka kichwa.
Jeshi la Polisi mkoa
wa Kinondoni lilifika yapata dakika tano baadaye baada ya raia wema kutoa
taarifa kuhusu tukio hilo .
Baada ya kuandika maelezo waliuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka
hospitalini kuuhifadhi huku uchunguzi zaidi ukiendelea.
Hata hivyo Maofisa wa
Jeshi hilo
walisikika wakiwataka madereva wa bodaboda kuvaa kofia za kujikinga pamoja na abiria
wao ili kupunguza madhara zaidi inapotokea ajali.
Gari la Jeshi la Polisi mkoa wa Kipolisi Kinondoni PT 4012 likiwa katika eneo la ajali Juni 25, 2017 |
Mashuhuda wa tukio hilo katika eneo la ajali Juni 25, 2017 |
Ofisa wa Jeshi la Polisi akichukua maelezo kutoka kwa mashuhuda wa tukio la ajali maeneo ya Kinondoni Kanisani Juni 25, 2017 |
Wasamaria wema wakisaidia kuupakia mwili wa marehemu katika gari la Polisi, Kinondoni Juni 25, 2017 |
0 Comments:
Post a Comment