Wanachama wa Chama cha Washehereshaji Tanzania (SAA) katika picha ya pamoja na familia ya Mzee Sixtus Mhagama Juni 19, 2017 maeneo ya Boko inapoishi familia hiyo inayougua ugonjwa wa ajabu. |
Wanachama wa SAA katika kuwatia moyo familia ya Mzee Sixtus Mhagama. |
Mzee Sixtus Mhagama akipokea fedha taslimu kutoka kwa wanachama wa SAA. |
Mtoto wa kwanza wa Mzee Sixtus Mhagama, Schola ambaye hajaathirika na ugonjwa huo akiwashukuru SAA kwa msaada walioutoa. |
Schola akiwa na mama yake ambaye kwa sasa haoni kutokana na matatizo yaliyomkuta. |
Chama cha Washereheshaji Tanzania (SAA) kimetoa msaada wa shilingi
milioni mbili zikiwamo fedha taslimu shilingi milioni 1.3 jana kwa familia moja
inayougua ugonjwa wa ajabu uliothibitishwa na madaktari kuwa haiwezekani
kutibika.
Familia hiyo watu sita ya Mzee Sixtus Mhagama ya kijiji cha Litoho
kutoka Wilayani Mbinga mkoani Ruvuma
iliyohamia jijini Dar es Salaam imepatwa na ugonjwa wa ajabu unaowafanya watoto
wao kila wanapofikisha miaka mitano huanza kupata ulemavu.
Katika ushuhuda wake wakati akikabidhiwa msaada huo vikiwamo vitu
mbalimbali kama nguo, mafuta, sukari Mzee Mhagama amesema walitoka kijijini
kwao Litoho mwaka 2006 na kuja Dar es Salaam katika hospitali ya Taifa ya
Muhimbili kwa ajili ya matibabu kutokana na hospitali zote mkoani humo kukosa
suluhisho la watoto wao.
Aidha Mzee Mhagama amesema miongoni mwa watoto hao mmojawapo
alishafiriki dunia huku wengine wakiendelea kukumbwa na ugonjwa huo ambao
unawafanya wote magamba pindi wanapokuwa katika maeneo ya baridi na maumivu
makali na mifupa yao
kushindwa kuimarika hali inayosababisha ulemavu.
Akipokea msaada huo Mzee Mhagama ameishukuru jamii kwa kumjali kwani
hata nyumba anayoishi huko Boko jijini Dar es Salaam amepewa na msamaria mwema
ili aweze kujisitiri katika hali ngumu ambapo mkewe pia amepatwa na ugonjwa huo
ambao umemfanya ashindwe kuona.
Hata hivyo amesema changamoto bado ni kubwa kwani anapaswa kwenda kila
siku Muhimbii na watoto wake ili waweze kufanyiwa mazoezi lakini kuna wakati
anashindwa kutokana na ukosefu wa fedha za kuwasafirisha wagonjwa hao.
Kwa upande wake wakati akikabidhi msaada huo Mwenyekiti wa SAA Emmanuel
Urembo amesema wamekuwa wakisaidia jamii kwa mwaka mara moja lakini safari hii
waliiona familia hiyo inayopata mateso makubwa japokuwa ni kiasi kidogo lakini
wanaamini msaada huo utaweza kuwafariji.
0 Comments:
Post a Comment