Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na wakuu wa mikoa yote katika Ikulu jijini Dar es Salaam Juni 13, 2017. |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli amewaagiza Wakuu wa Mikoa kusimamia kwa ukaribu utekelezaji wa mpango
wa ujenzi wa viwanda katika maeneo yao ili kuwawezesha wananchi kuongeza
thamani ya mazao yao na kuzalisha ajira.
Magufuli ametoa agizo hilo jana Ikulu Jijini Dar es Salaam
alipokutana na kufanya mazungumzo na Wakuu wa Mikoa ya Tanzania Bara, kuwa kila Mkuu wa Mkoa anapaswa kufanyia kazi
fursa za uanzishaji wa viwanda katika eneo lake na kuhakikisha anashawishi
wawekezaji kuzitumia fursa hizo kama inavyofanyika katika Mkoa wa Pwani.
Aidha Magufuli amewaagiza Wakuu wa Mikoa kuongeza juhudi za
utatuzi wa migogoro ya ardhi ikiwa ni pamoja na kuharakisha mchakato wa
kuwanyang’anya hati za umiliki wa mashamba makubwa ambayo yanashikiliwa na watu
pasipo kuyaendeleza.
Hata hivyo amewatahadharisha Wakuu wa Mikoa hao dhidi ya
watu wanaofanya njama za kujimilikisha maeneo makubwa ya ardhi na kusababisha
wakulima na wafugaji kukosa maeneo ya kilimo na malisho na ametaka wote watakaobainika
kufanya njama hizo wafichuliwe na kunyang’anywa maeneo hayo.
0 Comments:
Post a Comment