Tanzania imepoteza takriban shilingi trilioni 188 katika kipindi cha
miaka 19 kati ya mwaka 1998 na mwaka 2017 kupitia usafirishaji wamakinikia ya
dhahabu na shaba.
Ripoti ya Tume iliyoundwa mwezi Machi mwaka huu na Rais John Magufuli iliyojikita
kueleza kiasi cha madini na fedha ambazo Tanzania hupoteza kutokana na
usafirishaji wa mchanga wenye madini imedai kuwa Kampuni ya madini yenye makazi
yake nchini Canada, Acacia ambayo ni kampuni kubwa zaidi ya madini haikuwahi
kusajiliwa nchini, hivyo imekuwa ikifanya kazi kinyume cha sheria.
Katika matangazo ya moja kwa moja ya Televisheni kutoka Ikulu, Rais
Magufuli amemtaka Waziri wa Sheria Profesa Paramagamba Kabudi kupitia mikataba
yote ya madini.
Ripoti iliyopita ilisababisha Waziri wa nishati na madini Prof.
Sospeter Muhongo kusimamishwa kazi.
0 Comments:
Post a Comment