Thursday, September 12, 2024

Mlima Kilimanjaro, Pride of Tanzania and Africa

 

Kilimanjaro ni mlima mrefu kuliko yote Afrika, pia ni wa pili kwa urefu Duniani. Mlima huu uko nchini Tanzania katika Mkoa wa Kilimanjaro. Una urefu wa futi 19,340 (mita 5,895). Hali halisi Kilimanjaro ni zaidi kuliko mlima tu ni kama safu ndogo ya milima mitatu: Kibo, Mawenzi na Shira. Hii mitatu inaonekana kama vilele vitatu vya mlima mmoja hivyo si vibaya kusema Kilimanjaro ni mlima. 

Mlima huu ambao ni mrefu kuliko yote katika Bara la Afrika na wenye barafu katika kilelele chake ingawa, upo kwenye eneo la joto karibu na Mstari wa Ikweta. Mathalani, Kibo ina theluji na barafu  kadhaa ndogo.

Kilimanjaro ni volkeno iliyolala kwa sasa. Kwenye kilele cha Kibo gesi bado inatoka. Kumbukumbu ya wenyeji ina habari ya mlipuko takriban mnamo mwaka 1730.
Kilele cha juu cha Kibo kinaitwa Uhuru Peak. Mtu wa kwanza wa kufika kileleni hapo alikuwa Johannes Kinyala Lauwo kutoka Marangu aliyewaongoza Wajerumani Hans Meyer na Ludwig Purtscheller mnamo tarehe 6 Oktoba, 1889 wakati wa ukoloni wa Ujerumani. Wakati ule waliita ncha ya juu "Kaiser-Wilhelm-Spitze" (kijer.:Kilele cha Kaisari Wilhelm) kwa heshima ya Kaisari wa Ujerumani.

0 Comments:

Post a Comment