Kazi ya kulitoa lori lililopinduka mnamo Septemba 9, 2024 ikimalizika, siku tatu baadaye majira ya saa 5:46 usiku, pembezoni mwa Soko la Maimoria mjini Moshi. (Picha zote na JAIZMELA) |
Lori hilo lenye namba za usajili KBJ 139 F na trela lenye namba na usajili ZD 9542 lilipinduka za 7:30 usiku wa kuamkia mnamo Septemba 9, 2024 wakati dereva wa lori hilo alipotaka kukunja kona baada ya kukutana na kibao kilichokuwa kikimtaka asiendelee na safari.
Zoezi la kulitoa lori hilo kutoka mtaroni na kusababisha huduma ya umeme kukatwa ilianza majira ya saa 1 usiku na kumalizika saa 5:46 usiku.
Winchi yenye namba za usajili T 629 EDR lilifika katika eneo hilo na kuanza shughuli ya kulitoa mtaroni ambapo Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) mkoa wa Kilimanjaro lilifika na kutoa msaada ikiwamo kukata umeme katika laini iliyokuwa imeegemewa na lori hilo.
Kikosi kazi cha Tanesco kilichokuwa na gari aina ya Land Cruiser su 44318 kilisimamia zoezi hilo kuhakikisha hakuna madhara ya umeme yanayoweza kujitokeza katika eneo la tukio.
Hata hivyo mashuhuda wa tukio hilo wametoa rai kwa madereva kuwa makini na uendeshaji wa vyombo vyao vya usafiri ili kupeusha madhara yanayojitokeza pindi ajali kama hizo zinapotokea.
Mwenyekiti wa Kituo cha Bodaboda eneo la Soko la Maimoria Jamal Hussein maarufu ‘Chawaaa’ alisema makossa yalianza kwa watengenezaji wa barabara Hari Singh & Sons ambao waliweka kibao cha kubadili uelekeo (Diversion) bila kutoa tahadhari kwanza kwani njia hiyo imekuwa ikitumiwa na malori.
0 Comments:
Post a Comment