Friday, July 12, 2024

Sherehe za Irmegolik zafanyika Mandila, Mserekia

 

Wamaasai ni moja ya kabila ambalo linapatikana katika nchi ya Tanzania na Kenya hasa upande wa kaskazini. 

Kabila hili lina historia ndefu sana katika bara la afrika. na kama inavyofahamika kuwa wamasai wanapatikana kwenye familia lugha ya Nailotiki( Nilotic language family). 

Kiasili kabila hili linatoka upande wa kusini mwa nchi ya sudani(Sudani Kusini) hasa maeneo ya Bahr el Ghazal, Jonglei na Kordufan na kaskazini mwa nchi ya kenya kwenye maeneo ya ziwa Turkana. 

Kabila la Wamasai walipata kuishi huko tangu zama za mawe, wakiishi maisha ya mfumo wa Ujima, kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na kutokana na mrundikano wa watu, Kabila la wamasai waliamua kuhama na kusambaa sehemu mbalimbali hasa upande wa Afrika mashariki. 

Wamasai walifika pwani ya Afrika mashariki hasa maeneo ya kusini mwa Kenya na Tanzania kwenye miaka ya 1600-1700; Na wakati huo ikumbukwe kuwa Wabantu walishafika pwani ya Afrika mashariki. hivyo kulikuwa na mapigana baina ya Wamasai na makabila mbalimbali ya kibantu kama Wapare na Wachaga.









0 Comments:

Post a Comment