Chama cha Mapinduzi (CCM)
kimeendelea kuwawezesha vijana kushiriki katika shughuli za ujasiriamali, ikiwemo
kuwapatia fursa za kiuchumi hatua ambayo inadhihirisha ukuaji wa uchumi.
Hatua muhimu ya uzinduzi wa New
Lumumba Restaurant, mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro chini ya mkurugenzi wake
Athuman Ally Mfutu inadhihirisha namna CCM kinavyotoa fursa kwa vijana wake
waliopo ndani ya chama hicho kuwekeza katika maeneo mbalimbali ikiwamo
biashara.
New Lumumba Restaurant imeanza
kwa kasi mpya baada ya uzinduzi wake wa nguvu ambao umetiwa chachu na viongozi
wa chama hicho na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo Mkuu wa
Wilaya ya Moshi Mjini Zephania Sumaye amekata utepe wa kuacha kwa utoaji wa
huduma ya chakula na vinywaji wa mgahawa huo.
Akizungumza na wageni waalikwa wa hafla hiyo fupi mnamo Julai 19, 2024 katika viwanja vya Makao Makuu ya CCM Moshi Mjini DC Sumaye Mkuu amesema nia njema ya taifa kwa ujumla katika suala la maendeleondio chachu kubwa ya kuruhusu uwekezaji wa ndani pale wanapokidhi vigezo.
“CCM kwa nia njema kabisa yenye kuleta maendeleo ya nchi na watu wake imetoa fursa za uwekezaji kupitia chama hicho, ni vyema watu wakachangamkia fursa hizo ili waweze kukuza vipato vyao na hata kipato cha taifa kupitia kodi mbalimbali”, alisema DC Sumaye.
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya, alimpongeza Mwekezaji aliyefungua Mgahawa huo Athuman Ally Mfutu, ambapo amesema Serikali itaendelea kushirikiana naye pamoja na wawekezaji wengine katika kuhakikisha maendeleo yanapatikana Wilayani humo.
Akiongea katika hafla hiyo Naibu Mstahiki Meya Manispaa ya Moshi Stuwart Nathael, amesema uwekezaji huo utasaidia kukuza uchumi wa Manispaa ya Moshi kupitia njia mbalimbali kutokana na kukua kwa mzunguko wa fedha.
“Tatizo kubwa katika nchi
yetu ni ukosefu wa ajira, inapotokea kijana anaamua kuwa Mwekezaji Serikali
itamuunga mkono kwa kuwa atachangia kukua kwa uchumi”, amesema Nathael.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Moshi Mjini Faraji Swai, amesema chama Wilayani humo, kitaendelea kushirikiana na Wawekezaji mbalimbali ili kuongeza fursa za uwekezaji Wilayani Moshi.
“Moja wapo ya yale yaliyomo ndani ya ilani ya CCM ni kwa serikali kutengeneza
fursa za ajira; hili ndilo lililopelekea uongozi wa CCM wilaya kuja na wazo la
kutafuta mwekezaji ambaye uwekezaji wake pia umebadilisha madhari ya ofisi kuwa
nzuri”, amesema.
Awali akizungumza Mkurugenzi wa New Lumumba Food Restaurant Athuman Ally,
amekishukuru Chama kwa kumpa ushirikiano katika uwekezaji alioufanya, ambapo
amesema umetoa ajira kwa zaidi ya 15 wengi wao wakiwa ni vijana.
0 Comments:
Post a Comment