Mpaka wataalamu wanaandika habari juu ya watu hawa walifanikiwa kugundua kuwa lugha wanayoongea watu hao ambao ni Wamasai kwa sasa, ilifanana sana na kabila la Wadinka. Wadinka ni kabila linalopatikana nchi ya Sudani Kusini. hivyo kabila hili la wamaasai ilitokana namna ya mtindo wa lugha ulivyokuwa.
Kabla ya kuingia Sudan Kusini (Sidain) kwa ajili ya kutafuta Malisho ya mifugo walitokea nchi ya Misri (neno hilo lilitokana na ukame ambao ulifanya watu kukosa hata maziwa ya kuwapa watoto (Esiret, Misiru... Mesiri) ni maneno ambayo huonesha kutokuwepo hata na maziwa ya kuchanganya na maji.
Walikuwa wakiishi na kuutambua mto Nile (Nailiil) maji yanayoelea juu ya kingo bila kuvunja kingo... Walilazimika kuanza kutoka na kutafuta pa kwenda. Wakaulizana (Kailo ) maana yake wanakwenda wapi ndio asili ya neno Cairo... Ndipo wakaelekea Sudan (Sidain, Sidai... Mahali pazuri penye malisho... Wakaulizana.. Katum? Kitum? Maana yake... Tutapata? Nitapata? Asili ya mji Khartoum... Kwa kifupi ndivyo walivyoingia Sudan.
0 Comments:
Post a Comment