Friday, July 12, 2024

Je, utajiri ni nini, kwa Kabila la Wamasai?

 

Kabla ya wamasai kufika Tanzania, walikaa sana maeneo ya Kenya hasa maeneo yale ya mbuga ya Masai Mara. Historia iliyoandikwa na wanaikolojia na wanaanthriopolojia inasema kuwa neno maasai linatokana na aina ya lugha iliyofahamika kama Maa. lugha hii ya Maa ilikuwa ikiongelewa na watu waliokuwa wakipatikana sana kusini mwa nchi ya Sudan, watu hao walikuwa Wadinka. 

Kwa kuwa asilimia kubwa Wadinka waliokuwa wakiongea lugha ya Maa walikuwa wakiishi kwenye Jagwa la Sahara, ndipo wataalamu waliamua kuweka lugha hii kwenye kundi la Nilo- Sahara, wakimaanisha aina ya lugha inayopatikana kwenye familia lugha ya Nilotiki ila inaongelewa na watu wanaopatikana maeneo ya Jangwa la Sahara. 







0 Comments:

Post a Comment