Tuesday, August 8, 2023

Posta Kilimanjaro yajadili mipango iliyotekeleza 2022-2023

Wafanyakazi wa Posta mkoa wa Kilimanjaro katika picha ya pamoja baada ya kujadili waliyoyafanya kwa mwaka 2022-2023


Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania mkoa wa Kilimanjaro wamefanya kikao kwa ajili ya kujadili namna walivyotekeleza bajeti ya mwaka wa fedha uliopita 2022-2023 na kujipanga katika bajeti ya mwaka 2023-2024.

 

Meneja wa shirika la Posta mkoa wa Kilimanjaro Deodatus Ako, ameyasema  hayo Agost 8 mjini Moshi wakati  akisoma taarifa yake ya utendaji kazi ya mwaka 2022-2023 ambayo ilikuwa ikiangazia mafanikio na changamoto zake.

 

Katika hotuba hiyo Ako, amewasihi watumishi kufanyakazi kwa kuzingatia weledi na kuona namna gani wanaweza kutatua changamoto zilizopo ili sekta hiyo iweze kuchangia zaidi kwenye pato la taifa.

 

Meneja huyo amesema  kikao hicho ni muhimu kwa kuwa watumishi wanashirikishwa kwa uwazi kuhusu namna walivyotekeleza bajeti ya mwaka 2022-2023  na kujipanga katika bajeti ya mwaka 2023-2024.

 

Aidha amesema katika kikao hicho pia wamesainiana mikataba ya utendaji kati ya meneja wa mkoa na wafanyakazi wa shirika la Posta ili waweze kuwajibika katika maeneo yao ya kazi.

 

 

Kwa upande wake Meneja Masoko wa Shirika la Posta mkoa wa Kilimanjaro Mwanamkuu Mussa, amesema anuani za makazi zimesaidia kurahisisha utambuzi wa utoaji wa huduma za posta nchini

 

Amebainisha kuwa mfumo wa Misimbo ya Posta ya Tanzania imesaidia utoaji wa huduma sio tu kwa shirika la Posta  na ufikishaji wa vifurushi na vipeto katika maeneo ya makazi, ofisi na sehemu za biashara.

 

Naye Posta Master  Wilaya ya Mwanga Ally Kilemile, amesema mikataba ya kazi ambayo wameisaini itawasaidia kuongeza ari ya utendaji kazi mahapa ka kazi ili malengo waliyojiwekea katika kipindi cha mwaka 2023-2024 yaweze kufanikiwa  ufanisi mkubwa.

 

Katika semina hiyo pia zilitolewa mada mbalimbali ikiwemo mada ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza zilizotolewa na Wauguzi kutoka KCMC  kitengo cha Afya ya Jamii na ambapo pia walipatiwa mafunzo ya Biashara na Masoko kutoka kwa mtaalamu kutoka Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi. 









 

0 Comments:

Post a Comment