Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Wilaya ya Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro, wameendelea kuutangaza utalii wa ndani ambapo sasa wameweka nguvu kubwa katika hifadhi ya Msitu huo kwa kampeni ya Tukacharu Rau-Mtoko Nyika.
Akizungumza na
waandishi wa habari jana ofisini kwake katika kampeni ya Tukacharu Ofisa Misitu
daraja la pili TFS Wilaya ya Moshi Zayana Mrisho Hashimu, amesema malengo
makubwa ya mpango kazi huo ni kuwafanya wakazi wa Moshi na viunga vyake
wafahamu zaidi kuhusu utunzaji wa mazingira na viumbe waliomio ndani ya hifadhi
hiyo.
Alisema hifadhi
ya Msitu Asilia wa Rau uliopo Kata ya Njoro Mjini
Moshi, umesheheni Vivutio mbalimbali vya Utalii ikiwemo mimea na miti ambayo ni
adimu inayopatikana katika eneo hilo pekee hivyo TFS Wilaya ya Moshi imeandaa
tukio la mbio za nyika ambalo wamelipa jina la Tukacharu Rau
Forest Mtoko Nyika ambalo litafanyika Agosti 20 mwaka huu kwa
kushirikisha wakimbiaji 200 ikiwa ni sehemu ya kuutangaza utalii.
Zayana
alisema Msitu wa Rau ni msitu wa kipekee ambao una wanyama wengi,
mimea na miti ambayo huwezi kuipata katika mahala pengine isipokuwa Msitu wa
rau, na kwamba unapofika katikati ya Msitu wa Rau utakutana panya wenye masikio
makubwa kama ya tembo ambao hawapatikani katika hifadhi yoyote hapa nchini pia
Kuna vinyonga weupe, pamoja na 'Mti wa mvule ambao unakisiwa kuwa na umri wa
miaka 200 na una urefu wa mita 51 na kipenyo Cha mita 3.
Alisema katika mbio
hizo kutakuwa na matukio mbalimbali ambayo yatafanyika siku hiyo ikiwemo
kuendesha baiskeli kwa kilometa 30, mbio za Joging, kutembea kwa miguu peku
pamoja na kujionea vivutio mbalimbali vilivyomo katika hifadhi hiyo.
Ofisa huyo alisema
Msitu wa Rau una vyanzo vya maji na hifadhi ya udongo ambao ni muhimu kwa
ukuaji wa viumbe hao, pia msitu wa Rau una chemichemi sita za maji safi
zinazotoka chini ya ardhi ambazo asili yake ni Mlima Kilimanjaro ambapo maji
hayo huifikia ikolojia ya msitu huo kupitia mito iliyopo chini ya
ardhi ambayo ilijitokeza kutokana na mlipuko wa volkano
iliyotengeneza mlima huo mrefu barani Afrika.
Kwa upande wake Askari
wa uhifadhi ndani ya Msitu wa Rau Shedrack Kilimba amesema Msitu huo una aina
mbalmbali za wanyama, wakiwemo Kima, Mbega, swala, Nyani, ndege aina
50 pamoja na miti wa Mvule wenye maajabu, ambao una miaka zaidi ya miaka 200,
ambapo wageni kutoka ndani na njeya nchi wamekuwa wakifika na kuutembelea msitu
huo.
Aidha Kilimba alisema
katika tamasha hilo kutakuwa na mbio za kuendesha baiskeli ikiwa ni
njia mojawapo ya kuondokana na magonjwa yasiyo y kuambukiza ambayo yamekuwa
yakiwakumba watu wengi kwa kushindwa kufanya mazoezi.
“Kadri tunavyozeeka
mifupa yetu inapungua uzito kwa asilimia 0.5 ya ukubwa wa mifupa kila mwaka,
kupungua huko huongezaka zaidi hada kwa wanawake wanapofikia umri wa kutoweza
kuzaa na kwa upande wa wanaume baada ya miaka 50,”alisema Kilimba.
Kwa mujibu wa Kilimba
alisema tafiti zinaonesha kuwa mazoezi yanaweza kupunguza hali hiyo au hata
kuizuia kupungua kwa uzito wa mifupa au udhafu wake kunatokana na umri mkubwa
hivyo mazoezi yanaaminika kusaidia kuitunza mifupa kwa kufanya kuwa imara
zaidi.
Vilevile Kilimba
alisema kutakuwa na matembezi ya kutembea peku bila kuvaa viatu hali ambayo
inasaiddia nyayo za miguu kuimarika zaidi sambamba na kutunza ikolojia yam situ
huo.
“Maisha yetu chimbuko
lake ni ardhini, tumetoka ardhini, viumbe na mimea tunayokula na maji
tunayokunywa, vyote vina asili ya ardhini na ardhini kuna madini,
chumvichumvi, antibiotics, antifugal na anti-viral chemicals na udongo ni
maisha na maisha ni udongo.
Aliongeza kusema kuwa
“Mitume yoote, manabii wote, wagunduzi na wafumbuzi woote wenye hadhi ya
Newton, Socrates, Avogadro, Eisten, Boyle, Archimedes na nk, mababu zetu,
maaskofu, mapope, masheikh, walioandika vitabu vya dini kama Bibilia na Msahafu
na wengine wengi ambao waliofanya mambo ya maana hapa duniani wote walikuwa
mara nyingi wakitembea kwa miguu ardhini, kushika udogo na kuibusu ardhi kwa
nyakati tofauti,”alifafanua.
Alisema magonjwa mengi
kuanzia vidonda hadi upunguvu wa damu vilikuwa vikitibiwa kwa udogo hadi sasa
wanyama, wadudu, ndege, samaki na mimea yote vinajipakaa mchangam kwa sababu
mbalimbali za kiafya kama sehemu ya matibabuhivyo utalii wa kutembea kwa miguu
ni sehemu ya kupunguza magonjwa kwenye nyayo za miguu.
0 Comments:
Post a Comment