Michuano ya Soka ya Zuberi Cup 2023 imezinduliwa rasmi leo katika dimba la Railway mjini Moshi huku Bingwa mtetezi Kaloleni akifungua dhidi ya Moskisa Academy.
Mgeni rasmi
katika ufunguzi huo ni Katibu wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro
Jonathan Mabhiya ambaye aliongoza na viongozi wengine wa chama chake.
Mabhiya
amezitaka timu zote zinazoshiriki mwaka huu kujituma huku akisisitiza waamuzi
kutenda haki kwa kila timu ili kuyafanya mashindano hayo kuwa mazuri na bora.
Akizungumza
kabla ya mchezo wa Kaloleni dhidi ya Moskisa Academy kuanza Mstahiki Meya wa
Manispaa ya Moshi Mhandisi Zuberi Kidumo amesema mwaka huu ameboresha zawadi na
kwamba hakutakuwa na malalamiko kwani zawadi zote zipo.
Katika
kuhakikisha suala la usalama litakuwa vizuri Inspekta Manyasi
amewahakikishia washiriki na mashabiki
wote kuwa hali itakuwa nzuri huku akisisitiza mashabiki kuwa na subira pindi
wanapoona timu yao haifanyi kama mategemeo yao.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa Kamati ya Michuano hiyo mwaka huu Mwalimu Mpande
amewahakikishia utulivu na soka safi kwa timu zote zinazoshiriki.
Katika
michuano ya mwaka huu timu 25 zitashuka dimbani kuwani taji hilo ambalo kwa
sasa linashikiliwa na vijana wa kutoka kata ya Kaloleni.
0 Comments:
Post a Comment