Shule ya Msingi Matemboni katika Halmnashauri ya Wilaya ya Moshi ipo mbioni kubomolewa na kufanyiwa marekebisho kutokana na uchakavu wa majengo yake, hali ambayo imekuwa changamoto kwa wanafunzi wanaosoma shuleni hapo.
Taarifa ya Halmashauri ya Wilaya ya Moshi chini ya Mkurugenzi Kastori Msigala inaonyesha kuwa mpaka sasa kiasi cha shilingi milioni 60 kimeshatolewa kwa ajili ya ukarabati mkubwa wa vyumba vya madarasa pamoja na matundu ya vyoo.
Shule hiyo kongwe miongoni mwa shule za msingi mkoani Kilimanjaro iliyoanzishwa mnamo mwaka 1941 imekuwa katika changamoto ya uchakavu wa vyumba vya madarasa hali inayoshusha morali ya wanafunzi kufanya vizuri.
0 Comments:
Post a Comment