Friday, April 7, 2023

DC Mwaipaya aifukuza taasisi inayojihusisha na ushoga/usagaji

Mkuu wa Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro Abdallah Mwaipaya ameifungia taasisi ya Kilimanjaro Youth Centre kutojihusisha na shughuli zake katika wilaya yake kutokana na kubainika kuendesha vitendo vya ushoga kwa vijana wilayani humo.

Akizungumza katika kikao cha tathmini ya matokeo ya kidato cha pili na cha nne wilayani humo DC Mwaipaya alisema kwa muda sasa suala la ushoga na usagaji limekuwa likifanywa kwa kificho lakini tangu lilipoanza kupigiwa kelele siku za hivi karibuni mengi yameibuka.

“Sasa hivi nchi yetu inataka kuingia kwenye janga kubwa la masual;a ya ushoga na usagaji, kuna watu kwa nguvu za fedha zao wanataka kutulazimisha kuingia huko,” alisema DC Mwaipaya

DC Mwaipaya aliongeza kuwa katika wilaya yake taasisi hiyo ilikuja na kupata ruhusa ya kuendesha kampeni yake kwa vijana lakini baadaye ikaja kubainika ilichokuwa ikifanya sio ilichoruhusiwa kufanya.

“Hapa Wilaya ya Mwanga kulikuwa na NGO’s moja inaitwa (Kilimanjaro Youth Network Association) walikuja wakisema wanashughulika na kuhamasisha Vijana kuhusu kupima virusi vya Ukimwi, kupinga ukatili na matumizi bora ya kondomu, tulipowafuuatlia kwa undani zaidi walikuwa sio Wataalam,” alisema.

Mkuu huyo wa wilaya alisema taarifa zaidi zilizagaa baada ya taasisi hiyo iisiyokuwa ya kiserikali kuendesha tukio la kuvalisha pete kwa wanaume katika wilaya yake ndipo alipowaita na kufanya nao mahojiano kwa kina

“Nilikuwa likizo, niliporudi kutoka likizo nikasikia kuna taarifa kwamba kuna eneo ambapo NGO’S hiyo kuna tukio la kuvalishana pete wanaume kwa wanaume, tyulifuatlia na kuwaita watu hao na kuwahoji , kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni. Tulimhoji mmoja baada ya mwingine” alisema DC Mwaipaya ,

Hata hivyo DC Mwaipaya alisema mkurugenzi wa taasisi hiyo baada ya mahojiano ya kina ikabainika aliwahi kuwa mtumishi wa serikali katika wizara ya mambo ya ndani na alifukuzwa kutokana na kujihusisha na vitendo hivyo.

“Tulimuuliza tena swali huyu mkurugenzi kwa nini wewe ulifukuzwa kazi ndani ya Wizara ya mambo ya Ndani kwa sababu ya ushoga, baadae alikiri. Lakini pia huyu mkurugenzi wa taasisi hiyo, alitueleza pia aliwahi kufanya kazi Zanzibar  alikiri ni kweli na marafiki zake wengi walikuwa mashoga na kufukuzwa huko,” aliongeza.

Kwa msisitizo DC Mwaipaya alisema, “Hiyo Ngo’s tumeifukuza ndani ya wilaya yetu,  kwani hatuwezi kufumbnia macho vitendo viovu, kuendelea kutendeka ndani ya Wilaya yetu ya Mwanga.”

Hata hivyo DC amewataka pia Walimu wa shule za msingi na sekondari ndani ya wilaya hiyo kuacha kupokea misaada ya vitabu kwani kuna vitabu vingine vinakuwa vimeandikwa kuhamasisha masuala ya ushoga.




0 Comments:

Post a Comment